Dkt. Slaa Afuatiliwa na watu wasiojulikana kutoka Iringa hadi Dar Es Salaam

Bandiko hili limefungwa hadi pale Kiongozi anaetambulika wa Chadema atakapotuma habari kuthibishitisha tukio hilo kuwa la kweli. Pole kwa usumbufu utakaokuwa umejitokeza kwa maamuzi haya.

Wasalam.

Shukrani sana Moderator kwa kulifungua bandiko hili
 
Last edited by a moderator:
kaka kama vip tumia tu kiswahil utaeleweka vizur zaid loose confidence ndo nin? ulitaka kusema lose confidence? hayo ni maneno mawil tofaut.
 
Upuuzi tu!

Habari kama hizi sio nzuri sana kwa mipango miovu inayopangwa na chama chako kipya.Ndiyo maana uzi huu ulipofungwa waliotoa 'likes' hapo juu ni wale wasiopenda mabadiliko na wanaounga mkono vitendo viovu vinavyofanywa na watawala tu
kaka kama vip tumia tu kiswahil utaeleweka vizur zaid loose confidence ndo nin? ulitaka kusema lose confidence? hayo ni maneno mawil tofaut.
lonesome,

Nilikosea nikaweka double 'O'.Sorry!
 
Last edited by a moderator:
kaka kama vip tumia tu kiswahil utaeleweka vizur zaid loose confidence ndo nin? ulitaka kusema lose confidence? hayo ni maneno mawil tofaut.

Kama GT pokea msg. Unataka kutuaminisha kuwa hujaelewa msg kwasababu tu ya kosa hilo? Siyo kweli bhaana
 
hao c kwamba ni watu wasiojulikana lahasha
NI WATU WANAOJULIKANA
KAMA WALIVYOTAJWA HAPO JUU
 
Spinning at the highest order.

Hivi wewe kwa akili zako kama kweli kuna watu wanataka kuwadhuru viongozi wa CHADEMA watahangaika kwa jinsi unavyoelezea hapa.

Siyo kila jambo ni siasa siasa siasa. Siku hizi mwanasiasa hata akikumbana na vibaka anadai wanasiasa wanamfanyizia.

Jifunzeni kutokuwa wepesi wa kupata majibu kabla ya uchunguzi makini.

Cha kushangaza hao hao watu wa usalama mnaowatuhumu kwa matukio mbali mbali yanayowahusu, ndiyo hao hao mnaotueleza mlienda kulipoti tukio.

Yaani umeamua kuja na ID mahususi kwa ajiri ya SPINNING za kiulinzi.

Kweli tutasikia mengi.

WanaJF,

Mimi Dr Slaa ambaye kwa siku 4 nimekuwa na ziara ya mkoa wa Iringa,Mbeya na Njombe nilikuwa narudi Dar jana baada ya kulala Iringa mjini kutokea Njombe.

Tukio linaloelezwa ni la kweli na nimelishuhudia mwenyewe. nimeingia kwa jina langu na ID yangu ili kuondoa dhana ya Spinning.
Namshukuru sana aliyetoa Taarifa, na kuliwasilisha kama ilivyotokea bila kuongeza wala kupunguza kitu.

Tuliondoka Iringa majira ya saa 3.30 hivi. Kwa mwanzo hatukutambua kitu, ila mara ya kwanza tuliona gari hilo likitupita kwa kasi km kama 20 hivi baada ya kupita junction ya Ipogolo. Tuliona kawaida. katika hatua hiyo tulijua ni wasafiri wenzetu. baadaye tukawa tunawapita, wanatupita kasi na kupotea, lakini baada ya muda tunawakuta na kutupisha. hatukustuka sana, japo kuanzia Ilula tukaanza kuulizana.

Mlima Kitonga wakatipita kwa kasi sana japo mbele yetu kulikuwa na semitrela kama 4 zikiteremka pole pole sana na nabasi 2 kwenye kona moja basi lililpkuwa mbele yetu kikakwaruzwa na lori lililokuwa lunapanda. Tukachukua tahadhari sana.

Tulipovuka daraja la Mtp Ruaha tukalikuta Lcruiser hiyo imesimama pembeni lakini abiria wake wote walikuwa ndani. tulipolikaribia likaondoka kwa kasi. kidogo tulistuka. sisi tukaamua makusudi kusimama na kununua vitunguu. Tulipofika Mikumi mjini tukalikuta tena likienda taratibu. kuanzia hapo tukawa makini sana hasa kwenye kona na au vichaka vikubwa. kimsingi tukajiweka kwenye hali ya tahadhari kubwa.

Moro tuliingia Petrol Station nao pia wakaingia nyuma yetu lakini hawakujaza mafuta. Punda wakaondoka direction ya Dodoma. Ikumbukwe sisi tumetoka Njombe tumetangaza tunaenda Kongwa ,Jimbo la Ndugai. mimi nikakapata dharura nikapaswa kurudi Dar. hivyo baada ya mufuta tukafuata direction ya Dar. Punde likatokeza tena na kutupita. Tukalipita kidogo kabla ya Chalinze. Baada ya Chalinze hatukuliona tena mpaka tulipolikuta Junction ya Tamko limepaka. mata nyibgine huwa natumia hiyo junction badala ya kuingia Jijini. Na kweli driver akapiga indicator nyingie hapo. nikaagiza tuelekee jijini Dar. ndipo ghafla nao wakaingia barabarani nyuma ya gari langu kabisa. ndipp nikaagiza afisa wangu apande juu ya gari letu -roof top na kulipga picha. kuona hivyo ghafla likatoka pembeni na kupaki. sisi tukaendelea, ndipo mbele kidogo tukakuta askari walioko zamu yao ya kawaida wakatusimamisha na tukawapa taarifa ya halu hiyo.

Sasa katika mazingira hayo kuna mtu bado anafikiria ni spinning anaweza kuamini hivyo hatuwezi kumlazimisha.

Natumaini nimefafanua ya kupotosha. Nawashukuru wote waliotupa pole. Tunaanza na Mungu tunabaki na Mungu. Hatumwogopi Binadamu na mapambano ya ukombozo hayatakoma kwa vitisho vya aiina hiyo, ndiyo kwanza vinatupa ari na mori.
 
Hizi mbinu za kifedhuli zinazotumika kukabiliana na Chadema na viongozi wake ni za kulaaniwa kwa nguvu zote.

Niwapongeze maofisa hao waliocharuka na kunakili namba za gari pamoja na kupiga picha gari hilo

Tumeshabihiana sasa na utawala wa makaburu.Ni jambo la hatari sana
Hawa watu wanafikiri hii nchi ni yao peke yao. Hakika hawatafanikiwa, kwa Mungu huweka watu wema ndani ya watu wabaya. (Gamaliel).
 
Taarifa hizi zinakufurahisha sana wewe na wasiopenda mabadiliko.Mbinu hizi za vitisho na majaribio mabaya kwa viongozi wa upinzani hazitafanikiwa kamwe.

Sasa jeshi la polisi litoe taarifa kuhusu watu hawa ni akina nani na malengo yao ni nini hasa.Kauli zebu huku hazisaidii bali jeshi la polisi sasa linalojigamba kutenda kwa weledi litoke hadharani

Kwani kutokupenda mabadiliko ni kuvunja sheria ya nchi au ya Mungu (dhambi)?
 
What are you talking about?
Hayo ya EPA, RICHMOND unayosema yameletwa hapa jf na kuwa backed up by hard evidence.

Jf siyo kijiwe cha kahawa kama unataka habari yako watu wenye fikra pevu waiangalie kwa macho mawili na waichukue serious.

Ulicholeta hapa ni kama udaku ambao unaweza kuokota sehemu yoyote ile.
Nimefurahi sana hapo kwenye red,halafu Rais wako akasema hao wezi warudishe pesa.
 
Spinning at the highest order.

Hivi wewe kwa akili zako kama kweli kuna watu wanataka kuwadhuru viongozi wa CHADEMA watahangaika kwa jinsi unavyoelezea hapa.

Siyo kila jambo ni siasa siasa siasa. Siku hizi mwanasiasa hata akikumbana na vibaka anadai wanasiasa wanamfanyizia.

Jifunzeni kutokuwa wepesi wa kupata majibu kabla ya uchunguzi makini.

Cha kushangaza hao hao watu wa usalama mnaowatuhumu kwa matukio mbali mbali yanayowahusu, ndiyo hao hao mnaotueleza mlienda kulipoti tukio.

Yaani umeamua kuja na ID mahususi kwa ajiri ya SPINNING za kiulinzi.

Kweli tutasikia mengi.
...Wangesubiri uchunguzi makini kama tunavyoendelea kusubiri uchunguzi makini wa Ramadhani Ighondu na Dr Ulimboka eeh!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Karibu sana mkuu. Ila siku nyingine ukitumwa kuandika propaganda waambie wawe makini na wanachukutuma. Hiyo namba uliyoandika ni namba ya gari la chadema ambayo hutumika maalum wakatiwa misafara ya viongozi wa chama hicho. Ni namba ambayo hubadilishwa pindi safari ikifika. Aghalabu hutumika kwa nadara sana hasa pale ambapo kunajengeka hisia kuwa viongozi wapo hatarini

Mkuu usitufanye wana JF wote ni hamnazo kama wewe na walio kutuma; Yaani Katibu mkuu na viongozi waandamizi wa CHADEMA wameshindwa kuitambua ghari ya chama chao ? Akili yako haina tofauti na ya hao walio kuagiza kuandika post zisizo eleweka; Mwigulu, Mulongo, Mulugo, Wassira, Lusinde Matusi, Ndugai, Makinda na Serukamaba.
 
CCM wanatumia mbinu za kizamani kuwakabili CDM wakati tatizo lao sio CDM bali shida za wananchi, hata wakiwang'oa kucha & meno kina Slaa, Mbowe na wengineo kama hawa deal na matatizo ya wananchi wataibuka wengine watakaoitaji kung'olewa kucha na meno.
 
WanaJF
Mimi Dr Slaa ambaye kwa siku 4 nimekuwa na ziara ya mkoa wa Iringa,Mbeya na Njombe nilikuwa narudi Dar jana baada ya kulala Iringa mjini kutokea Njombe.
Tukio linaloelezwa ni la kweli na nimelishuhudia mwenyewe. nimeingia kwa jina langu na ID yangu ili kuondoa dhana ya Spinning.
Namshukuru sana aliyetoa Taarifa, na kuliwasilisha kama ilivyotokea bila kuongeza wala kupunguza kitu.
Tuliondoka Iringa majira ya saa 3.30 hivi. Kwa mwanzo hatukutambua kitu, ila mara ya kwanza tuliona gari hilo likitupita kwa kasi km kama 20 hivi baada ya kupita junction ya Ipogolo. Tuliona kawaida. katika hatua hiyo tulijua ni wasafiri wenzetu. baadaye tukawa tunawapita, wanatupita kasi na kupotea, lakini baada ya muda tunawakuta na kutupisha. hatukustuka sana, japo kuanzia Ilula tukaanza kuulizana.
Mlima Kitonga wakatipita kwa kasi sana japo mbele yetu kulikuwa na semitrela kama 4 zikiteremka pole pole sana na nabasi 2 kwenye kona moja basi lililpkuwa mbele yetu kikakwaruzwa na lori lililokuwa lunapanda. Tukachukua tahadhari sana.
Tulipovuka daraja la Mtp Ruaha tukalikuta Lcruiser hiyo imesimama pembeni lakini abiria wake wote walikuwa ndani. tulipolikaribia likaondoka kwa kasi. kidogo tulistuka. sisi tukaamua makusudi kusimama na kununua vitunguu. Tulipofika Mikumi mjini tukalikuta tena likienda taratibu. kuanzia hapo tukawa makini sana hasa kwenye kona na au vichaka vikubwa. kimsingi tukajiweka kwenye hali ya tahadhari kubwa.
Moro tuliingia Petrol Station nao pia wakaingia nyuma yetu lakini hawakujaza mafuta. Punda wakaondoka direction ya Dodoma. ikumbukwe sisi tumetoka Njombe tumetangaza tunaenda Kongwa ,Jimbo la Ndugai. mimi nikakapata dharura nikapaswa kurudi Dar. hivyo baada ya mufuta tukafuata direction ya Dar. Punde likatokeza tena na kutupita. Tukalipita kidogo kabla ya Chalinze. baada ya Chalinze hatukuliona tena mpaka tulipolikuta Junction ya Tamko limepaka. mata nyibgine huwa natumia hiyo junction badala ya kuingia Jijini. Na kweli driver akapiga indicator tyingie hapo. nikaagiza tuelekee jijini Dar. ndipo ghafla nao wakaingia barabarani nyuma ya gari langu kabisa. ndipp nikaagiza afisa wangu apande juu ya gari letu -roof top na kulipga picha. kuona hivyo ghafla likatoka pembeni na kupaki. sisi tukaendelea, ndipo mbele kidogo tukakuta askari walioko zamu yao ya kawaida wakatusimamisha na tukawapa taarifa ya halu hiyo.
Sasa katika mazingira hayo kuna mtu bado anagikiria ni spinning anaweza kuamini hivyo hatuwezi kumlazimisha.

Natunaini nimefafanua ya kupotosha. Nawashukuru wote waliotupa pole. Tunaanza na Mungu tunabaki na Mungu. Hatumwogopi Binadamu na mapambano ya ukombozo hayatakoma kwa vitisho vya aiina hiyo, ndiyo kwanza vinatupa ari na mori.qw
Dr.W.Slaa tunakushukuru sana kwa kutoa comment kuhusiana na hili.Hata nilipopata habari hii nilisita kuiweka humu na MODS walifunga huu mjadala huu kulinda Credibility ya JF.

Poleni sana kwa haya yaliyotokea.Mjadala huu upo kwenye mitandao mingi sana

Taifa linaelekea kubaya kweli kweli.Sisi wananchi tutasimama nanyi siku zote

CC:Molemo Shardcole, Mzito Kabwela, Matola, Mzee Mwanakijiji Mohamedi Mtoi Ben Saanane Mikael P Aweda Nicas Mtei TIMING, Lwesye, Froida Magesi, King'asti FirstLady1 Crashwise Mungi, LiverpoolFC Tumaini Makene Suzie Josephine03 Waberoya , jmushi1 Kichuguu n.k
 
Last edited by a moderator:
WanaJF
Mimi Dr Slaa ambaye kwa siku 4 nimekuwa na ziara ya mkoa wa Iringa,Mbeya na Njombe nilikuwa narudi Dar jana baada ya kulala Iringa mjini kutokea Njombe.
Tukio linaloelezwa ni la kweli na nimelishuhudia mwenyewe. nimeingia kwa jina langu na ID yangu ili kuondoa dhana ya Spinning.
Namshukuru sana aliyetoa Taarifa, na kuliwasilisha kama ilivyotokea bila kuongeza wala kupunguza kitu.
Tuliondoka Iringa majira ya saa 3.30 hivi. Kwa mwanzo hatukutambua kitu, ila mara ya kwanza tuliona gari hilo likitupita kwa kasi km kama 20 hivi baada ya kupita junction ya Ipogolo. Tuliona kawaida. katika hatua hiyo tulijua ni wasafiri wenzetu. baadaye tukawa tunawapita, wanatupita kasi na kupotea, lakini baada ya muda tunawakuta na kutupisha. hatukustuka sana, japo kuanzia Ilula tukaanza kuulizana.
Mlima Kitonga wakatipita kwa kasi sana japo mbele yetu kulikuwa na semitrela kama 4 zikiteremka pole pole sana na nabasi 2 kwenye kona moja basi lililpkuwa mbele yetu kikakwaruzwa na lori lililokuwa lunapanda. Tukachukua tahadhari sana.
Tulipovuka daraja la Mtp Ruaha tukalikuta Lcruiser hiyo imesimama pembeni lakini abiria wake wote walikuwa ndani. tulipolikaribia likaondoka kwa kasi. kidogo tulistuka. sisi tukaamua makusudi kusimama na kununua vitunguu. Tulipofika Mikumi mjini tukalikuta tena likienda taratibu. kuanzia hapo tukawa makini sana hasa kwenye kona na au vichaka vikubwa. kimsingi tukajiweka kwenye hali ya tahadhari kubwa.
Moro tuliingia Petrol Station nao pia wakaingia nyuma yetu lakini hawakujaza mafuta. Punda wakaondoka direction ya Dodoma. ikumbukwe sisi tumetoka Njombe tumetangaza tunaenda Kongwa ,Jimbo la Ndugai. mimi nikakapata dharura nikapaswa kurudi Dar. hivyo baada ya mufuta tukafuata direction ya Dar. Punde likatokeza tena na kutupita. Tukalipita kidogo kabla ya Chalinze. baada ya Chalinze hatukuliona tena mpaka tulipolikuta Junction ya Tamko limepaka. mata nyibgine huwa natumia hiyo junction badala ya kuingia Jijini. Na kweli driver akapiga indicator tyingie hapo. nikaagiza tuelekee jijini Dar. ndipo ghafla nao wakaingia barabarani nyuma ya gari langu kabisa. ndipp nikaagiza afisa wangu apande juu ya gari letu -roof top na kulipga picha. kuona hivyo ghafla likatoka pembeni na kupaki. sisi tukaendelea, ndipo mbele kidogo tukakuta askari walioko zamu yao ya kawaida wakatusimamisha na tukawapa taarifa ya halu hiyo.
Sasa katika mazingira hayo kuna mtu bado anagikiria ni spinning anaweza kuamini hivyo hatuwezi kumlazimisha.

Natunaini nimefafanua ya kupotosha. Nawashukuru wote waliotupa pole. Tunaanza na Mungu tunabaki na Mungu. Hatumwogopi Binadamu na mapambano ya ukombozo hayatakoma kwa vitisho vya aiina hiyo, ndiyo kwanza vinatupa ari na mori.qw
...Tunazidi kukuombea Dr, usihofu Mungu wa watanzania yupo upande wako na atazidi kukulinda kwa njia zote. Walitaka wakuue kisha waseme "TUMECHUNGUZA ILIKUWA AJALI YA KAWAIDA" Wameishiwa mbinu maana hata ya Ugaidi watanzania waeshaishtukia, kukifuta chama wanajua muziki wake hawataumudu - sasa mbinu waliyobaki nayo ni kusababisha accident kama ya Sokoine.
 
Back
Top Bottom