Dkt. Slaa Afuatiliwa na watu wasiojulikana kutoka Iringa hadi Dar Es Salaam

Dkt. Slaa Afuatiliwa na watu wasiojulikana kutoka Iringa hadi Dar Es Salaam

Mkuu Ritz; argument zako hazina tofauti na za muishiwa dhaifu anaye amini foleni za magari jijini Dar es Salaam is an indicator of economic growth; Foleni kutoka Iringa hadi Dar es Salaam ? Like father, like son.
Master Peace:
Kichaa mara zote hujiona yupo sawa na huona walio wazima ni vichaa,hivi wewe kwa akili yako fupi ulitaka Dr Slaa atoke Iringa bila kufuatana na Magari Mengine?? Angepanda helicopta basi kama hataki kuona gari yoyote nyuma yake
 
Taarifa hizi zinakufurahisha sana wewe na wasiopenda mabadiliko.Mbinu hizi za vitisho na majaribio mabaya kwa viongozi wa upinzani hazitafanikiwa kamwe.

Sasa jeshi la polisi litoe taarifa kuhusu watu hawa ni akina nani na malengo yao ni nini hasa.Kauli zebu huku hazisaidii bali jeshi la polisi sasa linalojigamba kutenda kwa weledi litoke hadharani

My Dear Brother ("You're living in cloud cuckoo land.")Unazungumzia Polisi wa Tanzania na Vyombo vya Dola vya Tanzania Pole sana Ndugu yangu ,and God Bless you.
 
Taifa hili liwe makini sana.
Kama walishindwa kuidhibiti CHADEMA kabla ya 2005 basi watulie. Sasa hivi CHADEMA hakishikiki ni chama pendwa na viongozi wake wanapendwa sana na watanzania. Siyo siri. Kiongozi kama Dr Slaa hawezi kuwasingizia. Naomba ndugu zangu watanzania, muelewe kwamba kumdhuru Dr Slaa au kiongozi yeyote yule wa kitaifa kutoka CHADEMA ,kwa vyovyote vile utakuwa ni msiba mkubwa na mwanzo wa machafuko makubwa sana. CCM wajue na ninaamini wanalijua hilo. Kuanzia hapo ni lazima vyombo vya dola vitagawanyika, taifa litapasuka kabisa. CCM wasijidanganye huo mpango una hatari kubwa sana. Mungu aepushie mbali.
 
Pole Dr Willy Slaa,hao panya hawatafanikiwa.walikuwa wasababishe ajali kama hamjadhurika wawamiminie risasi watoweke.
 
ccm kuondoka wataondoka tu madarakani, ila lazima waondoke na damu za watu, believe it! watakaofaidi na mabadiliko ni watoto wetu!!
 
Anachofanya sasa hivi Dr Slaa na wenzake pamoja na Bavicha ni kutafuta huruma kutoka kwa wananchi kusingizia mambo kuwa wanawindwa na Usalama wa Taifa wauawe.

Madai ya Dr Slaa kuwa walikuwa wanafuatiliwa na gari ambayo wameipiga picha si wawake hiyo picha basi kuliko kuja na porojo.

Madai ya aina hii mbali ya kuwa madai ya uongo, pia yanaonyesha upeo mdogo wa viongozi wa Chadema.
 
Wenye hila wote siku moja wataumbuka. Ni kwa nini CDM iogopewe kiasi hiki? Ina maana utekelezaji wa majukumu yenu ni hafifu ndiyo maana mnawaogopa wasema kweli. Kama kweli mlikuwa na mambo mazuri kiutendaji basi kusingekuwa na ulazima wa kununua wauaji au watesaji au wanaofuatilia nyendo za viongozi wa Upinzani. Tushindane kwa hoja na si katika kupanga maangamizi. Nasikia vurungu za kusini zinahusishwa na CUF!!! Yaani hata mapungufu kiutendaji ambayo yanaleta life uncertainity bado mnalaumu upinzani? Lakini pia CUF=CCM!!! Kwa hiyo CCM imeamua kuanzisha fujo yenyewe kusini? What a joke!! Watanzania wamechoka!! Na kwa mantiki hii ache na vyama vingine vipate nafasi ya kuhudumia wananchi kwa kuwa nyie mmesha prove failure!!! Mungu akupe ulinzi wake Dr. Slaa, wao wanatumia nguvu ya dola ila wewe unatumia nguvu ya Mungu.
 
Master Peace:
Kichaa mara zote hujiona yupo sawa na huona walio wazima ni vichaa,hivi wewe kwa akili yako fupi ulitaka Dr Slaa atoke Iringa bila kufuatana na Magari Mengine?? Angepanda helicopta basi kama hataki kuona gari yoyote nyuma yake

Ritz-one acha kutokwa povu ninaufahamu vizuri sana uwezo wako wa kufikiri kutoka pale UDSM na huwezi kunipindisha katika hilo; Tatizo familia yenu nzima ni vilaza na wavivu wa kufikiria, na hakuna wa kumshauri mwenzie, possibly wote mmelewa madaraka na ulinzi wa hayo mageti ya ikulu;

Post yako imedhihirisha wazi, familia yenu nzima ni wavivu wa kusoma; Umeshindwaje kusoma post ya Dr.Slaa ili uweze kuelewa tukio zima lilivyo kuwa, cha kushangaza unaandika utumbo utadhani umekurupuka kutoka usingizini, post kama hizi uwe unamuandikia muishiwa dhaifu ndo atakubaliana na wewe;

Dr. Slaa ameeleza wazi, walipo kuwa Njombe waliaga wanaelekea Kongwa- Dodoma kwenye jimbo la Ndugai, walipo fika mjini Morogoro wakaingia Shell kuongeza mafuta na wale jamaa wakawafuata hapo shell, cha kusikitisha wao hawakuongeza mafuta, ghafla wakaondoka kwa kufuata Dodoma road bila kujua Dr. Slaa alipata dharura ya kuja Dar immediatelly na hivyo kusitisha safari ya kwenda Kongwa, wakiwa njiani kuelekea Dar es Salaam, TISS hao hao waliokuwa wakielekea Dodoma ghafla wakaipita ghari ya Dr. Slaa iliyokuwa ikielekea Dar es Salaam. Hizo scenarios zinadhihirisha pasipo shaka kuna mchezo mchafu ulikuwa unaendelea, cha kusikitisha msomi mwenye Bachelor ya Sheria ya kudesa unataka kutuaminisha ati ni foleni. Narudia ushauri kama huo uwe unaishauri familia yako ambayo uwezo wa kufikia umefika ukomo.

Probably unafahamu mchezo mzima ulivyokuwa ndo maana unataka kutupotosha, kumbuka kwenye tamko la Mabere Marando na wewe umo ndani ya nyumba, it is just a matter of time kila kitu kitakuwa hadharani.

Jiandaeni psychologically kuwa wapinzani ifikapo 2015; na sehemu pekee inayowafaa ni the Hegue.
Hakuna utawala dhalimu uliyodumu Milele; Hakuna awaye yeyote awezae kuzuia mabadiliko nchini Tanzania.
M4C ni mithili ya Tsunami hakuna wa kuizuia.

Mungu Ibariki CHADEMA;
Mungu mbariki Dr. Slaa.
 
Anachofanya sasa hivi Dr Slaa na wenzake pamoja na Bavicha ni kutafuta huruma kutoka kwa wananchi kusingizia mambo kuwa wanawindwa na Usalama wa Taifa wauawe.

Madai ya Dr Slaa kuwa walikuwa wanafuatiliwa na gari ambayo wameipiga picha si wawake hiyo picha basi kuliko kuja na porojo.

Madai ya aina hii mbali ya kuwa madai ya uongo, pia yanaonyesha upeo mdogo wa viongozi wa Chadema.
Katika madai yake hajataja SSM wale Usalama wa Taifa ila amesema habari ni ya kweli. Na mleta mada ameweka hadi namba za gari. Acha mwenye gari aje hapa abishe ndipo na picha iwekwe. Nina hakika magazeti wataandika hii issue na namba itakuwa hadharani. Kama kuna ameonewa na hii habari aende kushitaki polisi maana picha zipo.

CDM haijawahi na wala haitawahi kutaka sympathy kwa wananchi, ila wananchi kwa sasa si mbumbu tena, wanajua chuya na mchele, tofauti yake!! Miaka ya 47 ya siasa za 47 zimeisha!! Lumbaneni kwa hoja na kutekeleza at the expectations na si kutafuta mbinu za kumaliza wanaowasonga!!! Dr. Slaa yuko katika mioyo ya watanzania wengi kwa sasa na wewe na chama chako mnafahamu hilo ndio maana kila siku mnabuni mbinu mpya. Weekend njema mkuu Ritz.
 
Hii inatisha sana kusema kweli, labda nia yao ilikuwa ni kusababisha gari alilokuwemo Dr Slaa lipate ajali na wao baada ya hiyo ajali wamalize kazi yao waliyotumwa na magaidi wenzao.
 
Vipi wale watu wake wa Usalama hawakumtaarifu mapema?
 
Sishangai kabisa hata kidogo kwani Wasira amelitangazia taifa kuwa wanaoweza kuwindwa ni Dr Slaa na Mbowe.sas ni jambo ambalo tunajua iko hivyo,maana wasira kama waziri na alitamka maneno hayo bungeni akiwakilisha kauli ya serikali.ila wametusaidia kuja lolote baya litakalowakuta viongozi wetu ni Serikali.hasa Wasira na watu wake anaowaongoza.
 
Hii thread imeingiliwa na waganga njaa na vibaka wa magamba!!!
 
Af kwa kwann slaa ana tabia ya kuandika makosa mengi hivi katika maelezo yake, katibu mkuu gani wa chama anakosa umakini katika uandishi, yaani typing errors kibao pamoja na udhaifu wa kimantiki wa maelezo yake. Arekebishe hili
 
Anachofanya sasa hivi Dr Slaa na wenzake pamoja na Bavicha ni kutafuta huruma kutoka kwa wananchi kusingizia mambo kuwa wanawindwa na Usalama wa Taifa wauawe.

Madai ya Dr Slaa kuwa walikuwa wanafuatiliwa na gari ambayo wameipiga picha si wawake hiyo picha basi kuliko kuja na porojo. Madai ya aina hii mbali ya kuwa madai ya uongo, pia yanaonyesha upeo mdogo wa viongozi wa Chadema.
Ni wapi Dr Slaa ametaja neno Usalama wa taifa? Alichosema ni kwamba alikuwa akifuatiliwa. Sasa wewe umekurupuka mithili ya mtu aliyefumaniwa na mke wa mtu! Au wewe ndiye co-ordinator wa tukio hilo nini!!
 
Bavicha akili zao vituko sana. Hivi habari sensitive kama hii ni ya kuletwa na ID ambayo siyo verifies kweli?

Kesho utasikia kiongozi mmoja wa chadema anasema hiyo namba ya gari lililotajwa lilikuwa lake na kwamba habari imelengwa kumchafua.

Wewe mleta mada kwa vile unajua mambo tokea Iringa mpaka Dar es Salaam maana yake ulikuwa na Dr. Slaa sasa kwanini usichukue responsibility ya kusema kilichotokea?

Kinachochekesha zaidi vijana wa bavisha hapa washaingia line tayari. Yaani mlaghaika kilaiiiiiiiiini...

Vua Gamba kwanza,ndiyo utaweza kusema vizuri na kueleweka.
 
Poleni sana Dr Slaa.Wao na Ibilisi wao Chadema na Mungu wake.
 
Af kwa kwann slaa ana tabia ya kuandika makosa mengi hivi katika maelezo yake, katibu mkuu gani wa chama anakosa umakini katika uandishi, yaani typing errors kibao pamoja na udhaifu wa kimantiki wa maelezo yake. Arekebishe hili

Possibly wewe ni miongoni mwa vijana msiojitambua mlio ajiriwa pale Lumumba kwa ajili ya kupost pumba hapa jamvini; Wewe unacho kiangalia ni content au ni spealing ? Check kwanza details zako, ndo twende sawa;
 
Back
Top Bottom