mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
CCM inatafuta sababu za kuvuruga tena chaguzi za 2024 na 2025. Wanatambua kuwa mpeperusha bendera waliyekuwanaye endapo atashindanishwa na mwingine mwenye nguvu kutoka upinzani basi biashara itakwisha mapema sana.Muda mchache uliopita kavamiwa nyumbani kwake, polisi hawajasema wametoka kituo gani na haijajulikana anapelekwa wapi.
---
Kupitia mtandao wa X, Martin Maranja anahabarisha kuwa Dkt. Slaa amekamatwa...
Nimepata taarifa muda huu kwamba Dr. Wilbroad Peter Slaa amekamatwa na watu waliojitambulisha ni jeshi la Polisi muda huu akiwa nyumbani kwake Mbweni, Kawe, Dar es Salaam. Dr. Peter Slaa ni mmoja kati ya wakosoaji wa mkataba wa uuzwaji bandari kwa waarabu wa Dubai, DP WORLD.
View attachment 2716202
Pia Askofu Mwamakula amethibitisha taarifa hivyo kupitia mtandao wa X
BALOZI DKT. SLAA AKAMATWA NA POLISI!
Ndugu Watanzania!
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa Balozi Dkt. Willibrod Slaa amekamtwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake muda huu.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
View attachment 2716213
Kwa sasa ni lazima tutegemee tena ufedhuli na udhalimu wao kama ilivyokuwa katika chafuzi za 2019 na 2020. Wamezoea vya kunyonga, vya kuchinja wataviwezea wapi! Wakina Wambura na Kingai wanaanza tena kutekeleza kazi zao chafu.