Dkt. Slaa akamatwa na watu waliojitambulisha kama Polisi

Dkt. Slaa akamatwa na watu waliojitambulisha kama Polisi

Muda mchache uliopita kavamiwa nyumbani kwake, polisi hawajasema wametoka kituo gani na haijajulikana anapelekwa wapi.

---
Kupitia mtandao wa X, Martin Maranja anahabarisha kuwa Dkt. Slaa amekamatwa...

Nimepata taarifa muda huu kwamba Dr. Wilbroad Peter Slaa amekamatwa na watu waliojitambulisha ni jeshi la Polisi muda huu akiwa nyumbani kwake Mbweni, Kawe, Dar es Salaam. Dr. Peter Slaa ni mmoja kati ya wakosoaji wa mkataba wa uuzwaji bandari kwa waarabu wa Dubai, DP WORLD.

View attachment 2716202


Pia Askofu Mwamakula amethibitisha taarifa hivyo kupitia mtandao wa X

BALOZI DKT. SLAA AKAMATWA NA POLISI!

Ndugu Watanzania!
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa Balozi Dkt. Willibrod Slaa amekamtwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake muda huu.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula


View attachment 2716213
vizuri sana watambue nchi hii ina utawala halali. Babu mzima amejaa ubaguzi, chuki, uzushi, upotoshaji. Historia ya huyu babu yenyewe ni mbovu, ni katili, aliacha upadre akaoe, baadaye tena akaitelekeza familia na kwenda kuoa mke wa mtu. Ni mchafu, akapumzishwe gerezani asiendelee na uchochezi na uposhaji wake wa kipuuzi
 
Back
Top Bottom