Dkt. Slaa akamatwa na watu waliojitambulisha kama Polisi

Dkt. Slaa akamatwa na watu waliojitambulisha kama Polisi

Muda mchache uliopita kavamiwa nyumbani kwake, polisi hawajasema wametoka kituo gani na haijajulikana anapelekwa wapi.

---
Kupitia mtandao wa X, Martin Maranja anahabarisha kuwa Dkt. Slaa amekamatwa...

Nimepata taarifa muda huu kwamba Dr. Wilbroad Peter Slaa amekamatwa na watu waliojitambulisha ni jeshi la Polisi muda huu akiwa nyumbani kwake Mbweni, Kawe, Dar es Salaam. Dr. Peter Slaa ni mmoja kati ya wakosoaji wa mkataba wa uuzwaji bandari kwa waarabu wa Dubai, DP WORLD.

View attachment 2716202

Pia Askofu Mwamakula amethibitisha taarifa hivyo kupitia mtandao wa X

BALOZI DKT. SLAA AKAMATWA NA POLISI!

Ndugu Watanzania!
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa Balozi Dkt. Willibrod Slaa amekamtwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake muda huu.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

View attachment 2716213
Hili Taifa mda si mrefu kivile kijiti kitashika moto.
 
Malipo ya kupigania haki za watu weusi ni kifo.

Hutaungwa mkono, uta achwa peke yako ufe.

Waafrika na watanzania sio watu wa kuwapigania ni kuwaacha na shida zao.

Ukikuta mtu mweusi na nyoka wanapigwa muokoe nyoka.
Nakataa siyo swala la watu weusi Bali makondoo ya Tanganyika tu, hata hapo Zanzibar hawapo hivi.

Wakenya nadhani mziki wao unaouona, ni kuwakosea heshima kuwafananisha wakenya na makondoo ya Tanganyika yaliyopumbazwa na ushirikina wa Mwenge.
 
Kwaio Serikali imeshindwa kujibu kwa hoja wanaanza kuumiza wanao wakosoa sio.
serikali haijibu matusi, uchochezi na uhaini, serikali inatakiwa isimamie ulinzi na usalama wa nchi yetu kwa gharama yoyote ile, yakitokea yakutokea ni watu km wewe watakuja tena huku kuuliza serikali ilikuwa wapi mpaka wamewaacha hawa watu kufanya uchochezi na kuhubiri chuki. Wacha serikali ifanye kazi yake amani yetu itamalaki
 
uchochezi, uzushi, upotoshaji na uwongo siyo maoni.
makuwadi ya dpworld baada ya kujaribu kuhadaa watu kupitia chongolo na makuwadi wenzake wakagundua kuwa watanzania sio wapumbavu kama wao matokeo yake wakasanda maana hata huku mwanza pale kirumba waliishia kupata watu wachache wa kusomba kutoka busega,magu,sengerema,geita na misungwi na sasa hawana nyimbo kilichobaki ni kukamata watu baada ya kushindwa kujibu hoja ambayo ni last resort na mkishindwa hio njia jiandaeni kukimbilie kwa mabwana zenu mliyoyapa bandar.
 
Muda mchache uliopita kavamiwa nyumbani kwake, polisi hawajasema wametoka kituo gani na haijajulikana anapelekwa wapi.

---
Kupitia mtandao wa X, Martin Maranja anahabarisha kuwa Dkt. Slaa amekamatwa...

Nimepata taarifa muda huu kwamba Dr. Wilbroad Peter Slaa amekamatwa na watu waliojitambulisha ni jeshi la Polisi muda huu akiwa nyumbani kwake Mbweni, Kawe, Dar es Salaam. Dr. Peter Slaa ni mmoja kati ya wakosoaji wa mkataba wa uuzwaji bandari kwa waarabu wa Dubai, DP WORLD.

View attachment 2716202

Pia Askofu Mwamakula amethibitisha taarifa hivyo kupitia mtandao wa X

BALOZI DKT. SLAA AKAMATWA NA POLISI!

Ndugu Watanzania!
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa Balozi Dkt. Willibrod Slaa amekamtwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake muda huu.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

View attachment 2716213
Waarabu na mawakala wao wameamua liwalo naliwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
serikali haijibu matusi, uchochezi na uhaini, serikali inatakiwa isimamie ulinzi na usalama wa nchi yetu kwa gharama yoyote ile, yakitokea yakutokea ni watu km wewe watakuja tena huku kuuliza serikali ilikuwa wapi mpaka wamewaacha hawa watu kufanya uchochezi na kuhubiri chuki. Wacha serikali ifanye kazi yake amani yetu itamalaki
makuwadi ya warabu yameshindwa kujibu hoja pamoja na kumtuma chongolo na genge lake kuhadaa watanganyika lakin wamempuuza na hao makuwadi wanaokamata watu hovyo ni swala la muda tu.
 
Ubinafishaji Kwa nguvu! Mh. Rais Kwa Nini asingesikiliza mawazo ya wanaopinga halafu wakaboresha mapungufu. Kwa Tanzania si ni ya watanzania ikiwemo yeye? Kuna ulazima was kuaza kukamata watu kisa kupi ga hoja ya selikari?
we ndio umeamka usingizini? Walivyokuwa wanatukana, wanaeneza chuki, wanafanya uchochezi ulikuwa wapi. Hayo ndiyo maoni? Acha ulofa
 
Season two imeanza baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatime season two imeanza kurindima...
Yaliyomo katika season two ni pamoja na.
Kamata Kamata bambikia kesi.
Viroba vya maiti.
Wasiojulikana.#police
Utekwaji na kubwa zaidi Ubakwaji..
Usikose kufatilia kupitia channel yako pedwa Tz Dp world...
 
Back
Top Bottom