PreGE2025 Dkt Slaa akanusha kurejea Chadema ili agombee Urais 2025

PreGE2025 Dkt Slaa akanusha kurejea Chadema ili agombee Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731
Akihojiwa na redio ya Kyela FM, ya wilayani Kyela, ambako anashiriki kampeni Tukufu ya No Reform No Election inayoendelea Nchi nzima, Dkt Slaa amesema kwamba lengo la kujiunga na Makamanda wa Chadema ni kwa faida za vizazi vijavyo, na kwamba kwa umri alionao hana haja ya kugombea Urais.

Zaidi soma hapa

------
Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na mwanachama wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa, amewataka watanzania kuacha kudanganyika na propaganda za kitoto kuhusu kuhusishwa kwake kurejea Chadema ili kuwa mgombea urais.

Dk. Slaa ameyasema hayo hii leo tarehe 24 Machi 2025, wakati akiwa ameambatana na makamu mwenyekiti wa Chadema Bara John Heche, kwenye mahojiano na Kyela Fm, jijini Mbeya.

“Niwaambie watanzania, wasiwe rahisi kudanganyika na propaganda za kitoto kama hizi, Dk Slaa nina miaka 76 nina tafuta nini zaidi ya kujenga maisha na maslai ya vijana wangu, ambao nimewatumikia miaka yote.”

”Nimekuwa kwenye utumishi sehemu mbalimbali nilizopita kwa miaka zaidi ya 30, Chadema tu nimeka zaidi ya miaka 20, leo mtu anakuja na propaganda nyepesi, hizo ni za kupuuza, tuna hitaji vijana mtu kama heche akigombea urais leo, hawezi kuikoa Tanzania?"

"Kwanini tunamfikilia Dk. Slaa ambaye amefikia mwisho wake, yeye kazi yake ya sasa ni kusaidia wajukuu zake, nimerudi kwa sababu nina uchungu, serikali tuliyonayo imeshindwa kwa kuangamiza yale yote ambayo Mwalimu aliyaweka kwa ajili ya utajili wa Taifa hili."

"Nimerudi sasa ili nisaidiane wakina Heche, Lissu na vijana wengine wa Chadema ambao wanania njema na nchi hii."

“Tuna muhitaji Mussa nchi hii, wakulitoa taifa hili liende kwenye nchi ya raha, asali na maziwa na uwezekano huo tunao.” Alisema Dk. Slaa

Viongozi hao wanatarajia kufanya mikutano ya hadhara kwenye majimbo ya Kyela, Busokelo na Rungwe, katika muendelezo wz kampeni ya No reforms, No election
 
Nguvu ya umma inakuhitaji Dr. Slaa uwe Rais wetu, tutachangishana tukuchukulie form!
# Dr slaa for president 2025.
°°Lissu ni mropokaji hatauweza urais, urais unahitaji akili za utulivu na hekima za hali ya juu kabisa.
 
Nguvu ya umma inakuhitaji Dr. Slaa uwe Rais wetu, tutachangishana tukuchukulie form!
# Dr slaa for president 2025.
Raisi mtarajiwa ni Tundu Lissu, ndiye anelayetakiwa na Watanganyika wote ili arejeshe rasilimali zilizouzwa bila huruma, Dr.Slaa anafaa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje ni mwanadiplomasia mzuri tu.
 
Akihojiwa na redio ya Kyela FM, ya wilayani Kyela, ambako anashiriki kampeni Tukufu ya No Reform No Election inayoendelea Nchi nzima, Dkt Slaa amesema kwamba lengo la kujiunga na Makamanda wa Chadema ni kwa faida za vizazi vijavyo, na kwamba kwa umri alionao hana haja ya kugombea Urais.

Zaidi soma hapa

View attachment 3281756View attachment 3281757
mtu mwenye laana ya tamaa na usaliti wa kanisa, vyama vya siasa, familia na uporaji wa wake za watu anaweza kua kiongozi kweli?

si atapora wake za waTanzani wote sasa?

hata wewe ukitazama historia chafu ya hicho kizee, unaweza kusimama mbey za watu kuwashawishi wamchague na uchafu wake wote huo wa kijamii eti awe kiongozi wa kitaifa?

au unaweza kujivunia kweli kwamba hicho kizee ndio role model wako katika maisha na siasa, na kwamba chadema imelamba dume kumrejesha chamani? :pedroP:
 
Ile Propaganda ya Ebola imeshtukiwa na Wananchi na hii ya Slaa imeshtukiwa tena na Slaa mwenyewe sasa mtakuja na Proaganda gani tena?😆😆😂
Dr. Slaa for president her upstairs are so well for presidential post, #2025-2030, don't do a mistake for choosing madman.
 
Ile Propaganda ya Ebola imeshtukiwa na Wananchi na hii ya Slaa imeshtukiwa tena na Slaa mwenyewe sasa mtakuja na Proaganda gani tena?😆😆😂
Dr. Slaa for president his upstairs are so good for presidential post, #2025-2030, don't do a mistake for choosing madman. Your mistake could cost you heavily!
 
Ile Propaganda ya Ebola imeshtukiwa na Wananchi na hii ya Slaa imeshtukiwa tena na Slaa mwenyewe sasa mtakuja na Proaganda gani tena?😆😆😂
Hata lissu alisema hivyo hivyo kwamba hagombei mwenyekiti
 
mtu mwenye laana ya tamaa na usaliti wa kanisa, vyama vya siasa, familia na uporaji wa wake za watu anaweza kua kiongozi kweli?

si atapora wake za waTanzani wote sasa?

hata wewe ukitazama historia chafu ya hicho kizee, unaweza kusimama mbey za watu kuwashawishi wamchague na uchafu wake wote huo wa kijamii eti awe kiongozi wa kitaifa?

au unaweza kujivunia kweli kwamba hicho kizee ndio role model wako katika maisha na siasa, na kwamba chadema imelamba dume kumrejesha chamani? :pedroP:
Mkuu Talapalalataalatakapa tulia uandike vizuri..
 
mtu mwenye laana ya tamaa na usaliti wa kanisa, vyama vya siasa, familia na uporaji wa wake za watu anaweza kua kiongozi kweli?

si atapora wake za waTanzani wote sasa?

hata wewe ukitazama historia chafu ya hicho kizee, unaweza kusimama mbey za watu kuwashawishi wamchague na uchafu wake wote huo wa kijamii eti awe kiongozi wa kitaifa?

au unaweza kujivunia kweli kwamba hicho kizee ndio role model wako katika maisha na siasa, na kwamba chadema imelamba dume kumrejesha chamani? :pedroP:
Acha ujinga.
 
Back
Top Bottom