Dkt. Slaa akatalika kila mahali na kutengwa na kila mtu

CCM ilikuwa haihitaji Dr Slaa kuidhoofisha Chadema maana watanzania ndio walioidhoofisha chadema kwa kuikataa na kutoiunga mkono, kutokana na kukosa kwake sera na ajenda za kugusa maisha ya watanzania. CCM inaungwa mkono na kuendelea kupigiwa kura za ndio kila uchaguzi kutokana na sera na ajenda zake zinazogusa maisha yao.
Acha ujinga basi tofautisha kupigiwa kura na kuiba kura.
 
CCM huwa inapigiwa kura za ndio na watanzania na siyo kuiba kura. Vyama vya upinzani hata navyo vinatambua namna ilivyo vigumu kwa watanzania wenye akili Timamu na wanaojitambua kuwapigia kura wapinzani hasa Chadema.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika Dr Slaa anapitia wakati Mgumu Sana, wakati wa majuto, mateso ya moyo na nafsi na upweke wa hali ya juu sana. Kwa sasa haaminiki na yeyote wala kukubalika na kundi lolote lile, hasikilizwi na yeyote wala kupewa muda na yeyote. Amepuuzwa na kila mtu na kudharaulika na kila mtu. Haaminiki kwa yeyote wala kupewa faraja na yeyote.

Hakuna anayetaka kusimama na Dr Slaa kwa sasa, wala kuzungumza na Dr Slaa wala kupanga mipango au mikakati au ajenda au kuandaa sera na Dr Slaa, kwa sasa kila mtu na kila kundi au kila Taasisi au jumuiya inamuona Dr Slaa Kama mtu msaliti na mwenye ndimi mbili, Anaonekana kama mtu mwenye kujali maslahi yake binafsi, mtu mwenye uchu wa madaraka na mroho wa mamlaka,mtu mwenye chuki na mnafiki.

Hakuna anayetaka kujishughulisha na habari za Dr. Slaa wala kufuatilia habari zake wala kumtetea kwa lolote.Amekatalika na vijana, wazee,akina mama, wajane na watu wa makundi yote. Dr Slaa aliyekuwa akisimama mahali anaitwa Rais Rais kwa mbwembwe na madoido sasa Hakuna anayetaka hata kumuona mbele yake wala kusikia maneno yake. Ufalme wake umedondoka na kuvunjika vunjika,haelewi ashike wapi au asimame wapi maana hakuna anapoaminika wala kupokeleka.

Vijana waliokuwa wakimpa jeuri ,kumuamini,kumpenda,kumpigania,kujitoa mhanga kwa ajili yake,kupoteza masomo na kufukuzwa vyuo kwa ajili yake,kukosana na watu kwa ajili yake kwa sasa hawana habari naye wala kutaka hata kumsikia wala kumuona machoni pao,hawataki kusikia sauti yake wala maneno yake,wanamuona kama msaliti na asiyefaa kabisa hapa Duniani.

wanajuta kumfahamu,wanajuta kupoteza na kupotezewa muda wao na Dr Slaa hasa wakikumbuka walivyopigwa mabomu ya machozi kwa ajili yake,kulala mahabusu kwa ajili yake,kupigwa mijeledi kwa ajili yake,kufilisiwa mali kwa ajili ya kumuunga mkono yeye,kutengwa na ndugu kwa ajili yake na kupoteza ndoto zao kwa ajili yake.kwa hakika wakikumbuka haya madhira wanamlaani sana Sana Dr Slaa,wanaona uchungu sana mioyoni mwao ,hawataki hata kumsikia na wanafurahi sana kwa uamuzi wa kijasiri na kishujaa aliouchukua mh Rais wetu mama Samia Suluhu Hasssan wa kumvua hadhi ya Ubalozi.

Kwa sasa Dr Slaa Hakuna anapokaribishwa kuweka hata miguu yake. Haelewi arudi nyuma au aende mbele,haelewi amuombe nani msamaha na ampigie nani magoti maana kila mahali anaona alishaharibu na kusaliti, kila mahali alishapoteza heshima yake,kila mahali alishapoteza uaminifu,kila mahali alishapoteza nguvu yake ,kila mahali alishaoonyesha kuwa siyo wa kuaminika wala kuaminiwa na kila mahali alishawaumiza na kuwajeruhi watu na mioyo yao inatiririka machozi na Damu ya mateso aliyoyawapatia na kuwasababishia .

Anamaliza uzee kwa majuto na maumivu ya hali ya juu sana,anamaliza kwa masononeko,anamaliza kwa kuiona Hadithi yake ikiwa mbaya na kitabu chake cha matendo yake kikitupwa chini na kusiginwa na kila mtu. Alioanza nao wote hawamtaki maana wote wanaona amekiuka viapo vyote alivyoapa na kuwasaliti.

Mtu na kiongozi pekee aliyekuwa amemsitiri na kumtunzia heshima alikuwa ni Amiri jeshi mkuu wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama mh Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hasssan.sasa Dr Slaa kwa chuki zake Binafsi akajiona kuwa yeye ni mwamba,Jemedari na komandoo.akaanza vituko hadi vya kuwaza habari za kutaka kumpindua Rais wetu na Serikali yake. Akaanza kuhamasisha machafuko na lugha za kuhatarisha usalama wa Taifa letu na umoja na mshikamano wetu kama Taifa,akaanza kuleta dharau na ubaguzi kwa mh Rais.Akaanza kutaka kuleta utani na mchezo na mboni na Nembo ya Taifa letu .

sasa amepigiwa baada ya kubipu.Simu moja tu imempa pigo la maisha ambalo hata lisahau,kwa kuwa alidhani watanzania wapo upande wake kumbe walishamtoa katika mioyo yao na kumpuuza siku nyingi sana.Sasa amekatalika kila sehemu na kuzomewa kila mahali, na kila mtu hayupo Tayari kumsemea wala kumtetea wala kumuunga mkono wala kusimama upande wake.

Namshauri tu kuwa Aende kanisani akapige magoti na kunyenyekea mbele za mwenyezi Mungu na kuomba msamaha Hadharani kwa Taifa letu.Bila kufanya hivyo kwa hakika Dr Slaa ataishi kwa mawazo na msongo wa mawazo mkubwa sana maana Hakuna kitu kibaya Duniani kama kukosa Amani ya moyo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Andishi refu la kuchosha, kumbe ni utopolo wa chuki na udini mtupu!

Umefanyia utafiti wapi kuconclude kuwa Dr. Slaa hakubaliki kwenye mioyo ya watu na katengwa?

Ishu sijui kukisaliti chama, nk nk ni za kitoto sana kutolewa na mtu wa kariba yako.

Alitoka Chadema kwa maelezo yenye kujitosheleza ambayo hajawahi kuyakiuka mpaka leo ("mnyonge mnyongeni...").

Waliokisaliti chama ni wenzake kwa kununuliwa na Lowasa, jambo hilo kila mtu analielewa hatupo kuanza kukumbushana mambo ya juzi juzi ambayo hata muongo hayajatimiza.

Magufuli kumpatia Ubalozi haikumfanya arudi Ccm na mpaka leo hajajiunga na chama chochote.

Na katika mahojiano yake ya juzi aliulizwa hilo na akaeleza wazi kwamba hana mpango wa kujiunga na chama chichote na maoni yake hayatoi kwa kukisemea chama chochote bali hiyo ni haki yake ya kikatiba kama raia kutoa mawazo yake na msimamo wake.

Kumefumuka kundi la watu walionunuliwa kuchafua watu wema kwenye mitandao ikiwa chanzo ni mkataba wa DPW ukiwemo wewe.

Ulishamsikia huyo mzee akizungumzia udini ama uChadema zaidi ya kulaani mikataba ya kimagumashi ambayo kila mwenye kuitakia mema nchi analaani?

Muda ni mwalimu mkuu ipo siku utakuja kujuta sana kufanya kazi za uchawa wako usio na kichwa wala miguu kuchafua watu.

Ninalaani sana kuchafua watu ambao angalau wamebakia kuleta faraja na matumaini kwa raia wanyonge wasio na wa kuwatetea wala kuwasemea.
 
Huyo ni special case...kanisa lilimshindwa duniani mtamuweza?
 
Wenye akili thabiti hatumtengi tunaskiliza hoja alafu tunahitimisha Kwa akili. Mwenye akili ndogo huogopa wenye hoja tofauti maana hawana akili ya kuchambua wanajua watashawishika kwakila atachoambiwa!!!
 
Kuna watu kwenye hii dunia mmechagua maisha ya kunyenyekea watu ili muweze kupata chochote kitu,ila wengi wenu ni mapapai
 
Alijidai eti kuukimbia ule mchezo pendwa wa maaskofu na mapadri.

Hivi josefina nae kamtema mzee?
Hizo si ndio tabia pendwa za waarabu, huo walivyotuharia kanda ya pwani[emoji2], unakutana na binti wa kipwani anakwambia "kambare lake tope babu wewe huku amekuwekea vidole hivi [emoji108][emoji108]"
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika Dr Slaa anapitia wakati Mgumu Sana, wakati wa majuto, mateso ya moyo na nafsi na upweke wa hali ya juu sana. Kwa sasa haaminiki na yeyote wala kukubalika na kundi lolote lile, hasikilizwi na yeyote wala kupewa muda na yeyote. Amepuuzwa na kila mtu na kudharaulika na kila mtu. Haaminiki kwa yeyote wala kupewa faraja na yeyote.

Hakuna anayetaka kusimama na Dr Slaa kwa sasa, wala kuzungumza na Dr Slaa wala kupanga mipango au mikakati au ajenda au kuandaa sera na Dr Slaa, kwa sasa kila mtu na kila kundi au kila Taasisi au jumuiya inamuona Dr Slaa Kama mtu msaliti na mwenye ndimi mbili, Anaonekana kama mtu mwenye kujali maslahi yake binafsi, mtu mwenye uchu wa madaraka na mroho wa mamlaka,mtu mwenye chuki na mnafiki.

Hakuna anayetaka kujishughulisha na habari za Dr. Slaa wala kufuatilia habari zake wala kumtetea kwa lolote.Amekatalika na vijana, wazee,akina mama, wajane na watu wa makundi yote. Dr Slaa aliyekuwa akisimama mahali anaitwa Rais Rais kwa mbwembwe na madoido sasa Hakuna anayetaka hata kumuona mbele yake wala kusikia maneno yake. Ufalme wake umedondoka na kuvunjika vunjika,haelewi ashike wapi au asimame wapi maana hakuna anapoaminika wala kupokeleka.

Vijana waliokuwa wakimpa jeuri ,kumuamini,kumpenda,kumpigania,kujitoa mhanga kwa ajili yake,kupoteza masomo na kufukuzwa vyuo kwa ajili yake,kukosana na watu kwa ajili yake kwa sasa hawana habari naye wala kutaka hata kumsikia wala kumuona machoni pao,hawataki kusikia sauti yake wala maneno yake,wanamuona kama msaliti na asiyefaa kabisa hapa Duniani.

wanajuta kumfahamu,wanajuta kupoteza na kupotezewa muda wao na Dr Slaa hasa wakikumbuka walivyopigwa mabomu ya machozi kwa ajili yake,kulala mahabusu kwa ajili yake,kupigwa mijeledi kwa ajili yake,kufilisiwa mali kwa ajili ya kumuunga mkono yeye,kutengwa na ndugu kwa ajili yake na kupoteza ndoto zao kwa ajili yake.kwa hakika wakikumbuka haya madhira wanamlaani sana Sana Dr Slaa,wanaona uchungu sana mioyoni mwao ,hawataki hata kumsikia na wanafurahi sana kwa uamuzi wa kijasiri na kishujaa aliouchukua mh Rais wetu mama Samia Suluhu Hasssan wa kumvua hadhi ya Ubalozi.

Kwa sasa Dr Slaa Hakuna anapokaribishwa kuweka hata miguu yake. Haelewi arudi nyuma au aende mbele,haelewi amuombe nani msamaha na ampigie nani magoti maana kila mahali anaona alishaharibu na kusaliti, kila mahali alishapoteza heshima yake,kila mahali alishapoteza uaminifu,kila mahali alishapoteza nguvu yake ,kila mahali alishaoonyesha kuwa siyo wa kuaminika wala kuaminiwa na kila mahali alishawaumiza na kuwajeruhi watu na mioyo yao inatiririka machozi na Damu ya mateso aliyoyawapatia na kuwasababishia .

Anamaliza uzee kwa majuto na maumivu ya hali ya juu sana,anamaliza kwa masononeko,anamaliza kwa kuiona Hadithi yake ikiwa mbaya na kitabu chake cha matendo yake kikitupwa chini na kusiginwa na kila mtu. Alioanza nao wote hawamtaki maana wote wanaona amekiuka viapo vyote alivyoapa na kuwasaliti.

Mtu na kiongozi pekee aliyekuwa amemsitiri na kumtunzia heshima alikuwa ni Amiri jeshi mkuu wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama mh Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hasssan.sasa Dr Slaa kwa chuki zake Binafsi akajiona kuwa yeye ni mwamba,Jemedari na komandoo.akaanza vituko hadi vya kuwaza habari za kutaka kumpindua Rais wetu na Serikali yake. Akaanza kuhamasisha machafuko na lugha za kuhatarisha usalama wa Taifa letu na umoja na mshikamano wetu kama Taifa,akaanza kuleta dharau na ubaguzi kwa mh Rais.Akaanza kutaka kuleta utani na mchezo na mboni na Nembo ya Taifa letu .

sasa amepigiwa baada ya kubipu.Simu moja tu imempa pigo la maisha ambalo hata lisahau,kwa kuwa alidhani watanzania wapo upande wake kumbe walishamtoa katika mioyo yao na kumpuuza siku nyingi sana.Sasa amekatalika kila sehemu na kuzomewa kila mahali, na kila mtu hayupo Tayari kumsemea wala kumtetea wala kumuunga mkono wala kusimama upande wake.

Namshauri tu kuwa Aende kanisani akapige magoti na kunyenyekea mbele za mwenyezi Mungu na kuomba msamaha Hadharani kwa Taifa letu.Bila kufanya hivyo kwa hakika Dr Slaa ataishi kwa mawazo na msongo wa mawazo mkubwa sana maana Hakuna kitu kibaya Duniani kama kukosa Amani ya moyo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Siasa bwana haina Heshima kabisa

Yan mpaka ww kutoka mashimoni huko unaweza kuja kumsema mtu ambae serikali ilikaa ikamwamini na akafanya kazi yake Kwa weledi mkubwa

Mpaka akaondoka chadema, na bado serikali ilikuwa inampa backup

Mpaka akapewa inchi ya ulaya kwenda kuwakilisha tanzania

Then Leo mtu mmoja just because ana bando la buku na smart phone basi anaweza kuja kuandika anything anachojisikia
 
Mm na family yangu pamoja na ukoo wangu tumemkubali n kumpokea kwa mikono miwili.
 
Dr Slaa Ni msaliti na mnafiki sana ndio maana hakuna wa kumuunga mkono wala habari naye

Kila mtu anaetoa mawazo yake ni msaliti?

Ww haya unayoandika si mawazo yako? So ww tukuitaje? Chawa kupe au Nani?
 
Kumbuka alikuwa padri wa kikatoliki, sio mnafiki ila mkweli. Ukweli ndio unaomfanya aonekane mbaya. Siku akishika dola mtashangaa na maneno yenu yasiyokuwa na ukweli.
 
Back
Top Bottom