KWELI Dkt. Slaa alitoa kauli ya kuipindua Serikali wakati wa mahojiano

KWELI Dkt. Slaa alitoa kauli ya kuipindua Serikali wakati wa mahojiano

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Salaam

Ndugu zangu, katik pitapita zangu mitandaoni hasahasa kwenye mjadala unaomuhusu Dkt Slaa nimekuwa nikikutana na clip fupi ya Sekunde zipatazo 15 ikimuonesha anatamka kuhusu kupindua Serikali. Kwa namna Clip hiyo ilivyokatwa nashindwa kuelewa muktadha wa kauli hiyo.

Naombeni mtusaidie kutafuta ukweli wa tukio hilo au Interview hiyo kwa kirefu zaidi.

Clip niliyokutana nayo na inayosambaa ni hii hapa chini:

1692205023774.png

Picha: Dkt Slaa


Video 1: Kipande (clip) inachosambaa kwenye mitandao ya kijamii


Video 2: Sehemu ya kipande cha Dkt. Slaa kwa urefu zaidi
Chanzo: Star TV
 
Tunachokijua
Tangu kukamatwa kwa Dkt. Slaa mnamo Agosti 13, 2023 kumeibuka mijadala mbalimbali kumhusu. Wakili wake Adv. Dickson Matata katika ukurasa wake wa X (zamani Twitter) alitoa taarifa zinazodai kuwa Dkt. Slaa amehojiwa kuhusu kosa la uchochezi kinyume na Sheria na baada ya muda tuhuma zikabadilika na kuwa uhaini.

Tangu kutolewa taarifa hiyo ya Wakili mijadala imeibuka katika mitando mbalimbali ya kijamii kuhoji sababu ya Dkt. Slaa kuhusishwa na kosa la uhaini. Baadhi ya watu katika mitandao wamekuwa wakisambaza video yenye Sekunde 15 ikimuonesha Dkt. Slaa akitamka kuhusu kupindua Serikali.

Je, ni kweli Dkt. Slaa alitoa kauli ya kuipindua Serikali?
JamiiForums imefanya uchunguzi na kubaini kuwa kauli hiyo ya Dkt. Slaa aliitamka katika mahojiano yake aliyofanyiwa kwenye kipindi cha Medani za Siasa kinaendeshwa na Star TV. Mahojiano hayo yaliwekwa katika ukurasa wa YouTube wa Star TV Habari mnamo Julai 1, 2023 yakiwa na urefu wa 01:30:53 (Saa moja dakika thelathini na sekunde hamsini na tatu).

JamiiForums baada ya kutazama mahojiano yote ambayo kwa kiasi kikubwa Dkt. Slaa aliongelea Mkataba wa Bandari na harakati zake za kisiasa. Imebaini kuwa kauli ya kuhusu kuipindua Serikali aliitoa kuanzia 1:06: 40. Sehemu ya mahojiano hayo Dkt. Slaa anasema:
Tunaishinikiza Serikali mpaka iondoke kwa sababu Serikali ibara ya nane ya katiba inasemaje?
Ni Serikali ya ajabu ambayo imeingia kwenye mkataba bila kushirikisha watu wake, tatizo lipo kwenye katiba yetu na ndiyo maana tunataka katiba mpya sasa, sio jana Wala si kesho Ili upuuzi usitokee tena.
Upuuzi imetokea, tazama Marekani Rais anapelekwa mahakamani. Donald Trump sasa hivi yupo mahakamani kwa kesi ya ngapi? Juzi amepelekwa na kushitakiwa kwa makosa 37 kwenye kesi Moja.
Sisi tumekinga Marais wa kwetu hii ni nchi ya aina gani? Tunaishi Dunia ipi? Afadhali Dunia ya kina Mangungo waliodanganywa kwa kupewa shanga na kioo Cha kujitazamia Hadi inauzwa ni kwa sababu ameletewa kitu Cha kujitazama, ndiyo kitu muhimu sana kwake.
Hatuko huko tena, tutapiga kelele, tutaishinikiza Serikali na Matokeo yake kama hawataona leo wataona karibuni sana.
Mwandishi: Hoja ya msingi hapa kwa sababu mmeshafikia kwenye hii hatua, Watanzania hawana Cha kufanya.
Dkt. Slaa: Sio hawana Cha kufanya Serikali inaweza, kwani Serikali zinapopinduliwaga sasa kwanini zinapinduliwa? Huwezi kuniambia hamna Cha kufanya.
Mwandishi: Tufanye nini sasa hapo?
Dkt. Slaa: The extreme ni kuipindia Serikali. Serikali ibara ya nane inasema mamlaka yake yote yanatoka kwa Wananchi, Serikali inayofanya vitu bila kujali mamlaka ya Wananchi na inafanya vitu kwa kejeli inatuona Sisi watoto wadogo.
Inasema kwamba itarekebisha wakati tunajua hakuna njia. Jana nilimsikiliza Shivji. Shivji katika nchi hii ni kama Dictionary ya Sheria. Amesema njia pekee ni Bunge likae chini na wajitambue kwamba walikosea, wajishushe, wabatilishe kwasababu ndiyo njia pekee iliyobaki kufuta huo mkataba mbaya na huyo ndiyo Mwalimu ambaye Dunia inamtambua kama mtaalaum wa sheria. Halafu Serikali inakuja inapiga piga machenga.

Hivyo, kutokana na chanzo hiki kilichopitiwa na JamiiForums, hoja inayodai kuwa Dkt. Slaa alitamka kuhusu kuipindua Serikali ni ya kweli.
Jaman JF jiepusheni na kusema jambo ni Kweli au Sio Kweli.

Ukweli ni kitu kigumu sana kuthibitisha.

Yohana 18:38.
Pilato akamwambia, Kweli ni nini? Naye akiisha kusema neno hilo akawatokea Wayahudi tena, akawaambia, Mimi sioni hatia yo yote kwake.
uongo ndo una nguvu kuliko ukweli
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kutafsiri neno moja katika maelezo ya jambo zima na kutafsiri jambo zima. Kwa mimi nilivyomuelewa Dr. Slaa kuhusu namna ya kuondokana na mkataba wa bandari ni kuwa serikali inaweza kufanya jambo, na isipofanya wananchi watafanya jambo dhidi ya serikali kisheria na hilo likishindikana wananchi wanaweza kufanya hata nje ya kisheria!

All in all, MAPINDIZI sio sawa na MAPINDUZI, ikiwa tutataka kumhukumu Dr. Slaa kwa kila neno alilolisema.
 
Polisi buana sasa hapo ndiyo anaenda kuipindua serikali? Si mwandishi kamuuliza hapo hakuna cha kufanya ,akasema cha kufanya kipo mamlaka yanatoka kwa wananchi ,wananchi wanaweza kuipindua serikali siyo kama yeye ndiyo ataipindua.
 
Polisi buana sasa hapo ndiyo anaenda kuipindua serikali? Si mwandishi kamuuliza hapo hakuna cha kufanya ,akasema cha kufanya kipo mamlaka yanatoka kwa wananchi ,wananchi wanaweza kuipindua serikali siyo kama yeye ndiyo ataipindua.
Kama taifa hatuwezi kuchekea viashiria vya uhaini hata kidogo. Uhaini/mahaini washughulikiwe kwa mujibu wa sheria
 
Kwa hasira zangu za karibu ningewageza Babu seya kwenye uongozi wangu.
 
Naona tangu jana mitanadoani kumemwagwa maroboti yanayosambaza viclip vya kuhalalisha makosa ya kuwakamata watu kisa wanakosoa mkataba!!
 
Salaam

Ndugu zangu, katik pitapita zangu mitandaoni hasahasa kwenye mjadala unaomuhusu Dkt Slaa nimekuwa nikikutana na clip fupi ya Sekunde zipatazo 15 ikimuonesha anatamka kuhusu kupindua Serikali. Kwa namna Clip hiyo ilivyokatwa nashindwa kuelewa muktadha wa kauli hiyo.

Naombeni mtusaidie kutafuta ukweli wa tukio hilo au Interview hiyo kwa kirefu zaidi.

Clip niliyokutana nayo na inayosambaa ni hii hapa chini:

View attachment 2718624
Video 1: Kipande (clip) inachosambaa kwenye mitandao ya kijamii

View attachment 2718676
Video 2: Sehemu ya kipande cha Dkt. Slaa kwa urefu zaidi
Chanzo: Star TV
I see!
 
Kama taifa hatuwezi kuchekea viashiria vya uhaini hata kidogo. Uhaini/mahaini washughulikiwe kwa mujibu wa sheria

Unaujua uhaini? Unaweza kunitajia mtu hata mmoja aliyeshitakiwa kwa uhaini na alifanya kitu gani ili tujenge msingi wa uhaini wa mdude/slaa/mwabukusi.
 
NAWAPONGEZA JF KWA KUWEKA MAMBO HADHARANI KWENYE NYEUPE NI NYEUPE SI HABARI ZA RANGI YA MAZIWA.
UKWELI NI KWAMBA CHADEMA WAMETISHIA AMANI YA NCHI NA KUPANGA MAPINDUZI YA KIGAIDI
 
Wavunje mkataba wa dpw kisaha wamshitaki.wavunjee
 
Back
Top Bottom