Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Uneandika usichokiamini, au huujui labda ukweli.

CCM kuanzia 2015 haikuwahi kukubalika kwa wananchi, walilazimisha kukubalika kwa kutegemea mauaji, utekaji, nk.

Kama kweli unaamini agenda za upinzani zilianza kufanyiwa kazi na CCM from 2015, kwanini wakalazimisha wagombea wao wengi wapite bila kupingwa kwa sababu za kitoto kama kutokujua kujaza form?

Na kwanini wale wapinzani waliofanikiwa kugombea waliishia kuibiwa kura zao kwa namna ya aibu bila hofu yoyote na ushahidi ulikuwepo wa kila aina?
 
Acha ujinga. Kwani kuwaona ndiyo lazima uwatambue. Kuamini hii sababu ya kijinga ni kuonyesha jinsi gani ulivyo mjinga.

Kazi ya kutafuta wajuaji ni ya jeshi la police. Na kama hiyo ndiyo sababu yao ya kushindwa kuwapata basi kazi hawawezi na itabidi jeshi lipewe training upya.
 
Dr. Slaa na apologists wake wanataka tusiizungumzie ripoti ya CAG mpaka Kamati za Bunge zitoe blessing zao kwa sababu tutaingiza siasa!

Wanataka kutuaminisha kuwa hizo Kamati za Bunge ni apolitical na watakuwa neutral kwenye hoja za CAG!

Kutowasilisha majibu ya audit queries katika wakati muafaka ni sababu tosha ya jamii kutilia mashaka na integrity yako na ni lazima uhojiwe katika mahakama ya umma. Ukiweza kuzijibu hapo baadae, bado utabakiza tuhma ya uzembe wako.

Seriously, Slaa anataka tuamini Kamati ya Bunge iliyoundwa na Ndugai kuliko CAG ambae analindwa na Katiba ili kuhakikisha yuko above politics! Tusihoji kwa nini ATCL inaendeshwa kihasara mpaka wakina Tulia watupe kibali! Mzee kweli amechanganyikiwa.

Amandla...
 
Hasara ( Loss) si kigezo cha ufisadi ni metrics zinazohitaji professional opinion after Audit queries response. Ukiukwaji wa procurement process inaweza kuwa ni upindishaji wa taratibu lakini usio na hasara!

Kwenye ukaguzi Auditor anafata muongozo ulivyopaswa kufanyika alafu anaangalia taratibu zilizofatwa. Kama utaratibu haukufatwa lazima iwe query na risks zake. Wakati wa kufunga hoja inaweza kubaki na sura hii 1) Utaratibu umekiukwa lakini haukuleta hasara 2 ) Utaratibu umekiukwa na kuleta hasara. Vyote ni tatizo na hapo ndio tunapaswa kuhukumu.

Kwasasa CAG ameona jambo ambalo hajapata jibu na ameainisha risks za hilo aliloona! Sasa kabla hatujaanza siasa tungesubiri kuona serikali wamefungaje hiyo hoja then tuanze kelele!

Kwasasa wanasiasa mandumilakuwili wamebeba findings na figures zake wanahukumu watu kuwa ni mafisadi kuliko wakati wowote nchi hii imepata kushuhudia! Purely cheap politics kwa watu ambao wanajua facts ila wanatumia ufahamu wao kudanganya umma! Ni dhambi hii!
 
Hivi huyu Jamaa anapozungumzi haya yote, Ana Mke au kaachwa?? Sababu za kuachwa ni zipi?? Nimepata mashaka sana alipojaribu kujiingiza kwenye sakata la Mh Lissu.

Huyu Mzee kama aliweza kumsaliti Mungu Muumba wake kwenye Upadri atashindwaje Kwa Chadema?? Apambane na Laana zake huko.
 
Hapana! Huwezi kuzungumzia hoja ambazo hazijafungwa. Kama report hii ya CAG ndio final report sasa inakwenda Bungeni kufanya nini? Kuhukumu?

Nimetoa mfano mdogo sana, Chadema imewahi kupata Audit findings za CAG ambazo zilitumika kipropaganda lakini mwisho hizo findings zilikuja kuwa closed.

Auditor akiomba details au kiambatanisho asipopata kwa wakati maana yake utaenda kujibu kwenye kamati what happened! Why mnahukumu watu mafisadi tena kwa numbers ambazo bado hoja hazijafungwa?

Mkitaka kuenjoy kuita watu mafisadi kwa short cut kama hizi basi msilalamike baadae mambo yameishaje. Tusipende kudandia hoja za kisiasa bila kuzipima sababu anayesemwa humpendi au si mlengo wako.
 
Weka evidence hapa za serikali kutoa amri ya kuua na kuteaka raia , sio evidence zenu za fulani kapotea, duniani kote watu wanapotea na wanapatikana, sio kitu kizuri lakini sio mara ya kwanza kutokea nchini, haya ni matukio ya uhalifu ambayo yako miaka yote Tanzania na yataendelea kuwepo.

Chaguzi zote Tanzania miaka yote kumekuwa na wagombea wa ccm kupita bila kupingwa, ni mwaka 2015 tu ndio vyama vya siasa vilisimamisha wagombea kila mahali, lakini bado ccm wabunge wengi walipita bila kupingwa. Chadema tuache hizi tabia za kuomba kuhurumiwa, chama kikubwa tunakuwa na maandalizi hafifu, watu hata kujaza form hawajui, kama sisi tunatambua hilo kujaza form kimakosa unakuwa nullified ni hseria kali ambayo tunatakiwa twende bungeni tukapige kelele ibadilishwe sio kusubiri huruma , tuko kwenye upinzani tunatakiwa tujiandae kikamilifu sio kutegemea huruma ya mtawala.

Shida kubwa ya chadema imejikita kwenye tetesi, tuliiniwa kura, ushahidi uko wapi? twendeni basi mahakamani wapi, kuna kesi nyingi za watu kuibiwa kula zingine tumewahi shinda, zingine tuna shindwa ni kawaida katika mfumo huu wa siasa, tetesi haiwezi kuwa sera au suluhisho, tuna kesi nyingi tumeibiwa kura ziko wapi? zinatambulika nani?, hata mimi naweza simama nikasema nimeibiwa kura hata kama nimeshindwa its normal katika siasa, kwani si DONAL TRUMP anazunguka USA nzima anadai aliibiwa kura lakini ushahidi uko wapi?, je wew unadhani ni kweli aliibiwa kura? hiyo ndio politics sio kila kitu kisemwacho ni kweli.
 
haya mahojiano ameyafanyia nyumbani kwake mbweni? Nyumba aliyojengewa na Mbowe?
 
Tunakushukuru sana Mungu kwa kutuondolea huyu Mamluki Chadema
Mamluki ni wale waliozunguka miaka nane kutuaminisha kuwa lowasa hafai hata kuwa katibu kata, na mafuta ya chopa wakatuchangisha. Halafu ndani ya wiki wanatuambia kama tuna ushahidi wa ufisadi wa lowasa twende mahakamani kha!
 
Ipo siku ukweli utajulikana tu,si umeona wameanza kutajana kwa majina na vyeo.

Khalid Kagenzi pia alitekwa na kupigwa na wanaCDM wenzake.

Mtangazaji wa Uhuru FM aliwahi kutekwa na kuvunjiwa vifaa akireport maandamano hapo Ufipa.

Ben Saanane alikuwa haaminiki kwa Mbowe na mara zote akigombea ndani ya chama alikuwa akikatwa ghafla kawa msaidizi wake then kapotea!.

Uwezekano wa CDM kufanya hayo ili wapate cha kuisimangia serikali upo.

Haijalishi itakuwa baada ya muda gani ila ukweli utakuja kudhihiri.
 

..kama ni hivyo basi hiyo ripoti isiwe public mpaka pale waliotajwa watakapotoa majibu mbele ya kamati ya bunge.

..kutoa ripoti public halafu kutukataza kuijadili nadhani ni kutunyima uhuru wa kutoa maoni.
 
..kama ni hivyo basi hiyo ripoti isiwe public mpaka pale waliotajwa watakapotoa majibu mbele ya kamati ya bunge.

..kutoa ripoti public halafu kutukataza kuijadili nadhani ni kutunyima uhuru wa kutoa maoni.
Kuna watu wamepata access ndio wanafanya political spinning. Lakini hii inakwenda Bungeni na kupitia kamati zake facts zote zitafahamika.
 
Huyu kama aliusaliti upadri leo anashindwa nini KUONGEA upuuzi na ujinga huu!!.
 
MIE NILIMPENDA DKT SLAA PINDI AKIWA CHADEMA,NI MWANASIASA MWEREVU,MKWELI,NA MZALENDO HALISI WA TAIFA LETU,MPK MDA HUU MIE NINAMWAMINI NA KUMKUBALI,
 
Kupigwa risasi Lisu sio jambo la ajabu Bwana tuacheni! Kila siku jambo lile lile!
Kuna mshkaji alikuwa anasema kama wewe, juzi juzi hapa kaka yake wa damu kauawa kwa kupigwa risasi na polisi, kwa kumdhania kuwa ni jambazi, jamaa akawa analalamika sana kuwa kaka yake ameuliwa bila hatia, akapiga kelele sana kwamba kwanini hawakumpeleka mahakamani, baada ya kumaliza kulia nikamwambia "Matukio ya kupigwa risasi ni yakawaida sana" hata Marekani yanatokea sana, jamaa alifura hasira mara dufu...
 
Ni final in the sense kuwa inatoa hali aliyoiona wakati anafanya uchaguzi na baada ya kupewa ufafanuzi na wahusika . Wabunge na Rais wanapewa kama taarifa ambazo wanaweza kuzifanyia kazi kama wakitaka. Kamati hazina mamlaka ya kufunga hoja za mkaguzi. Wanachoweza kufanya ni kumshinikiza mhusika amalizane na CAG. CAG akiridhika ndio hoja inafungwa na sio otherwise.

Chadema ilikutwa na mapungufu ambayo ilikuwa haki yao kusulubiwa. Wao walifanya manunuzi bila kufuata utaratibu na CAG ndio aliwastua wakajirekebisha.

Hivi unataka kutuaminisha kuwa hizi Kamati za Bunge la Tullia zinaweza kuwa na uthubutu wa kunyooshea vidole ujenzi wa kiwanja cha Chato na ununuzi wa ndege? Zina uwezo wa kupitisha taarifa inayotoa mathlan hati chafu kwa CCM au hati safi kwa Chadema?

Tunapozungumzia ufisadi ni pamoja na uzembe. Na mara nyingi uzembe huo mara nyingi haziwezi kutatuliwa kwa risiti za kama mnavyosema. Inabidi iangaliwe mikataba, taratibu za ununuzi, uidhinishaji wa malipo n.k.

Kuibuliwa hoja za ufisadi hazimnyimi haki mhusika ya kujitetea. Msimamo wenu ni kama mtu kusema makosa anayoshutumiwa mtu yasiwekwe wazi mpaka mahakama itakapotoa hukumu! DPP atoe ushahidi wake kwa siri ili watu wasimhukumu mtuhumiwa kabla ya Jaji kutoa hukumu.

Hamna mtu atakayelalamika kama waliotuhumiwa watasafishwa hapo baadae. Labda nyie ambao pamoja na Chadema kusafishwa mliendelea kuwatuma wakina Takukuru kwenye fishing expedition.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…