Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Munachukia wasema ukweli. Dr Slaa ni mmoja wa viongozi bora Tanzania. Mumezowea opportunists kama Zitto Kabwe na puppets kama Tundu Lissu. Hampendi ukweli. Viongozi njaa bila siasa hawali
Sijui watumia vigezo gani ndugu? Tundu Lissu ndie mkweli wa kweli.
Aliwindwa na kumiminiwa marisasi kama swala, kwa kusema na kuwaambia ukweli. Mwendazake aliambiwa hadharani kuwa ni dikteta Aliyowaambia kwenye sakata la makinikia yaliwauma lakini kimya kimya waliyafuata.
Kwa maana halisi ya puppet kaangalie tena kwa hao wengine.
 
Umaskini ni mbaya na akuna kitu kibaya dunian km kua maskini umaskin unapoteza utu, akili , fikla, mawazo, hekima na mengneyo
Vijana tutafteni pesa tuje kulinda utu wetu tukikua
 
Mwanasiasa Willbrod Peter Slaa amefanya mahojiano na kuzungumza mambo mengi kuhusu siasa, mahojiano haya ni mwendelezo ya interview aliyofanya wiki iliyopita.

TAARIFA YA CAG INAPOTOSHWA
“Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu.

“Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.

“Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG.

CAG AMESABABISHA TAHARUKI KWA RIPOTI YAKE
“Kwanza hata CAG mwenyewe amechangia kuleta hii taaruki kwa kuwa huwa ni ya awali tu na analijua hilo, inatakiwa irudi kwa akaunti ofisa wa Serikali ijadiliwe, pia CAG wakati anatoa taarifa zake hadharani hatakiwi kuingia ndani kutoa ufafanuzi zaidi kama anavyofanya.

“Unaweza kukuta ripoti hiyo ikifika kwenye Kamati ya Bunge vitu vingi vikawekwa sawa, mfano labda kulikuwa na upotevu fulani wa mambo madogomadogo ambayo kwa nje yanaonekana kama ni wizi lakini details zikiwekwa sawa kunakuwa hakuna tatizo.

UBUNGE WA KINA MDEE SPIKA HANA KOSA, NITAZUNGUMZA CHADEMA WAKISHAKAA KIKAO
“Nimeona kwenye vyombo vya habari kuwa watajadiliwa na chama chao katika rufaa yao, naona lawama zimepelekwa kwa mtu ambaye hausiki (Spika).

“Chama kilitakiwa kufungua kesi Mahakamani kuhoji Tume ya Uchaguzi kwa kupitisha majina hayo lakini sijaona kesi. Mimi nitazungumza baada ya rufaa yao kupitiwa na CHADEMA, nimesikia wanakaribia kuwajadili kwenye kikao chao.

HOJA YA KATIBA SIYO MAHITAJI MUHIMU YA WANANCHI
“Mabosi wa vyama vya siasa ni wananchi, wanatakiwa kujiuliza wanayoyafanya yanawagusa vipi wananchi, kwa sasa kuna mambo mengi ya muhimu lakini hivyo vyama vimekuwa bize kuzungumza habari za ajenda ya Katiba.

“Hawana ajenda ambazo mwananchi anaweza kujiuliza kama inaweza kuweka chakula mezani, hakuna katiba ambayo inaweza kuzungumzia kila kitu.

“Katiba yetu ina vipengele vingi vya muhimu lakini havitekelezwi, japo sijasema kuwa katiba siyo muhimu.

“Mimi ni kati ya watu waliozunguka Tanzania kukusanya maoni lakini tusipotoshe kuwa katiba ndiyo jibu la kila kitu, siyo kweli.

“Leo hii Marekani ina katiba tunayoisifu lakini Donald Trump si alishutumiwa anataka kufanya mageuzi.

KATIBA PENDEKEZWA NI MBOVU KULIKO KATIBA YA SASA
Sisi tuna maoni ya Jaji Warioba, licha ya kuwa kulikuwa kuna mambo yamekosekana lakini yapo mazuri ambayo tunaweza kuyatumia.

“Baada ya maoni hayo kupelekwa Bungeni ikachujwa ikatoka inayoitwa Katiba Pendekezwa, ni mbovu kuliko hata katiba tuliyonayo sasa hivi.

SIZUNGUMZII SUALA LA LISSU KUPIGWA RISASI SABABU UTEKAJI ULIKUWEPOA CHADEMA
“Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

“Nitoe mfano iliwahi kutokea huko nyuma nikiwa Katibu Mkuu CHADEMA, nililetewa taarifa za mtu wangu anaitwa Joseph, huyu alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, alitekwa saa sita usiku. Kesho yake saa sita mchana nikahitisha mkutano na waandishi wa habari nikaisema sana Serikali na Usalama wa Taifa.

“Saa nane mchana siku hiyohiyo Joseph akapatikana, alikutwa ametupwa maeneo ya Ununio ameumia sana usoni.

“Mwezi mmoja baadaye kijana wangu wa Red Brigade anakuja kwangu kuniambia yeye ndiye aliongoza kukosi cha kwenda kumteka nyara huyo mwenyekiti huyo.

“Nikauliza kwa nini hakuja kwangu akasema ‘wapo viongozi wanaojua’, nikaamua kunyamaza, ndiyo maana ninapoulizwa suala la Lissu ninasema hapana, CHADEMA kwanza wajiangalie wao ndani.

“Huyo kijana (Joseph) walivyomtupa ufukweni walijua amekufa, kumbe alikuwa hajafa labda upepo ulimpiga akaamka. Miaka kadhaa baadaye tukaanza kusikia watu wanaokotwa wamekufa ufukweni, unadhani inatoa pcha gani!

“Ukiwa kiongozi lazima uwe kunasema ukweli hata kama unaona watu wako wanakosea.

SINA TATIZO LA LOWASSA
“Mimi na Lowassa tulipishana kwenye principal siyo maisha, mimi niliwahi kufanya fund rising na Jakaya Kikwete siku moja baada ya kupanda jukwaani na kumsema tena kwa mambo mazito.

“Nimeishi Ulaya, nimeona mambo ya kwenye mabunge, kuna muda inafika hatua wabunge wanapigana ngumi lakini wakitoka wanaenda kunywa bia. Unatakiwa kutofautisha maisha binafsi na siasa. Hivyo sikuwa na tatizo binafsi na Lowassa.

AWAMU YA TANO HAIKUFELI DIPLOMASIA YA KIMATAIFA
“Watanzania tuwe wakweli, tumefeli wapi, mimi nimekutana na wafanyabiashara wengi, wapo walioniambia wamchoshwa na Tanzania yenye ufisadi.

“Wapo walioamua kuondoa biashara zao huko nyuma lakini katika awamu ya tano waliamua kurejesha biashara hapa nchini, kwa nini? Ni kwa sababu kulikuwa kuna mambo mengi yanaenda vizuri, nazungumza kwa kuwa najua zaidi kilichokuwa kinaendelea.”

Chanzo: Dar24
Kuna kitu kaongea hapa kuhusu kuteka na Red brigade then kuna kifo Cha CHACHA WANGWE hapa kuna kitu ndani ya hivi vyama vya siasa
 
HEBU TUJADILI HII STATEMENT YA @drslaa

[emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541]

SIZUNGUMZII SUALA LA LISSU KUPIGWA RISASI SABABU UTEKAJI ULIKUWEPOA CHADEMA
“Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

“Nitoe mfano iliwahi kutokea huko nyuma nikiwa Katibu Mkuu CHADEMA, nililetewa taarifa za mtu wangu anaitwa Joseph, huyu alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, alitekwa saa sita usiku. Kesho yake saa sita mchana nikahitisha mkutano na waandishi wa habari nikaisema sana Serikali na Usalama wa Taifa.

“Saa nane mchana siku hiyohiyo Joseph akapatikana, alikutwa ametupwa maeneo ya Ununio ameumia sana usoni.

“Mwezi mmoja baadaye kijana wangu wa Red Brigade anakuja kwangu kuniambia yeye ndiye aliongoza kukosi cha kwenda kumteka nyara huyo mwenyekiti huyo.

“Nikauliza kwa nini hakuja kwangu akasema ‘wapo viongozi wanaojua’, nikaamua kunyamaza, ndiyo maana ninapoulizwa suala la Lissu ninasema hapana, CHADEMA kwanza wajiangalie wao ndani.

“Huyo kijana (Joseph) walivyomtupa ufukweni walijua amekufa, kumbe alikuwa hajafa labda upepo ulimpiga akaamka. Miaka kadhaa baadaye tukaanza kusikia watu wanaokotwa wamekufa ufukweni, unadhani inatoa pcha gani!

“Ukiwa kiongozi lazima uwe kunasema ukweli hata kama unaona watu wako wanakosea.
Police wanatakiwa wamkamate mara moja huyu paroko aliyeasi, ni mnafiki wa viwango vya juu
 
Nafikiri Slaa anaamini anamjua Magufuli kuliko Rais Samia au Dr. Mpango!
Watu waliofanya kazi pamoja,wakiongea karibu kila siku, kwamba yeye alivyoitwa na kupewa ubalozi na kutudanganya eti alimpa masharti asimlazimishe aingie ccm!! Magufuli ni mtu wa kumpa masharti kweli.
Kwa umashuhuri gani aliokuwa nao? Kwamba yeye alikuwa ni mwanadiplomasia saana kiasi cha kumtishia Magufuli!!
Umesikia viongozi wenzako walitaka kuua,umeambiwa ukanyamaza kimya,mbona hiyo ilikuwa sababu nzito sana ya kuondoka Chadema kuliko ya Lowasa.
Au anataka kutuambia uliridhishwa na sababu za kutaka kumuua,ukaona ukae kimya!!
Kwamba tofauti zake na Lowasa ni principals.
Unasema Chadema kwa nini wasiende mahakamani kwa issue ya kina Mdee, yeye kumng'a ng"ania Lowasa ni fisadi kuna mahakama yoyote imewahi kuthibitisha hizo tuhuma? Pamoja na rafiki yake Magu kwa mbwembwe kumjengea na mahakama eti ya mafisadi,lini alimshauri Magufuli ampeleke Lowasa mahakamani,ili ithibitishe tuhuma zake na uzuri na yeye angekuwa sehemu ya mashahidi!!
Kwa nini hakumpa masharti Magu kuwa ukitaka niwe balozi mpeleke mahakamani Lowasa ndo tungeona kweli kidume.
 
Ipo siku ukweli utajulikana tu,si umeona wameanza kutajana kwa majina na vyeo.

Khalid Kagenzi pia alitekwa na kupigwa na wanaCDM wenzake.

Mtangazaji wa Uhuru FM aliwahi kutekwa na kuvunjiwa vifaa akireport maandamano hapo Ufipa.

Ben Saanane alikuwa haaminiki kwa Mbowe na mara zote akigombea ndani ya chama alikuwa akikatwa ghafla kawa msaidizi wake then kapotea!.

Uwezekano wa CDM kufanya hayo ili wapate cha kuisimangia serikali upo.

Haijalishi itakuwa baada ya muda gani ila ukweli utakuja kudhihiri.
Kwanini usubiri ukweli uropokwe na mtu wakati hii ni nchi yenye vyombo vinavyoweza kufanya uchinguzi vikaleta majibu.tofauti na hapo ni unafiki tu.
 
Mwanasiasa Willbrod Peter Slaa amefanya mahojiano na kuzungumza mambo mengi kuhusu siasa, mahojiano haya ni mwendelezo ya interview aliyofanya wiki iliyopita.

TAARIFA YA CAG INAPOTOSHWA
“Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu.

“Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.

“Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG.

CAG AMESABABISHA TAHARUKI KWA RIPOTI YAKE
“Kwanza hata CAG mwenyewe amechangia kuleta hii taaruki kwa kuwa huwa ni ya awali tu na analijua hilo, inatakiwa irudi kwa akaunti ofisa wa Serikali ijadiliwe, pia CAG wakati anatoa taarifa zake hadharani hatakiwi kuingia ndani kutoa ufafanuzi zaidi kama anavyofanya.

“Unaweza kukuta ripoti hiyo ikifika kwenye Kamati ya Bunge vitu vingi vikawekwa sawa, mfano labda kulikuwa na upotevu fulani wa mambo madogomadogo ambayo kwa nje yanaonekana kama ni wizi lakini details zikiwekwa sawa kunakuwa hakuna tatizo.

UBUNGE WA KINA MDEE SPIKA HANA KOSA, NITAZUNGUMZA CHADEMA WAKISHAKAA KIKAO
“Nimeona kwenye vyombo vya habari kuwa watajadiliwa na chama chao katika rufaa yao, naona lawama zimepelekwa kwa mtu ambaye hausiki (Spika).

“Chama kilitakiwa kufungua kesi Mahakamani kuhoji Tume ya Uchaguzi kwa kupitisha majina hayo lakini sijaona kesi. Mimi nitazungumza baada ya rufaa yao kupitiwa na CHADEMA, nimesikia wanakaribia kuwajadili kwenye kikao chao.

HOJA YA KATIBA SIYO MAHITAJI MUHIMU YA WANANCHI
“Mabosi wa vyama vya siasa ni wananchi, wanatakiwa kujiuliza wanayoyafanya yanawagusa vipi wananchi, kwa sasa kuna mambo mengi ya muhimu lakini hivyo vyama vimekuwa bize kuzungumza habari za ajenda ya Katiba.

“Hawana ajenda ambazo mwananchi anaweza kujiuliza kama inaweza kuweka chakula mezani, hakuna katiba ambayo inaweza kuzungumzia kila kitu.

“Katiba yetu ina vipengele vingi vya muhimu lakini havitekelezwi, japo sijasema kuwa katiba siyo muhimu.

“Mimi ni kati ya watu waliozunguka Tanzania kukusanya maoni lakini tusipotoshe kuwa katiba ndiyo jibu la kila kitu, siyo kweli.

“Leo hii Marekani ina katiba tunayoisifu lakini Donald Trump si alishutumiwa anataka kufanya mageuzi.

KATIBA PENDEKEZWA NI MBOVU KULIKO KATIBA YA SASA
Sisi tuna maoni ya Jaji Warioba, licha ya kuwa kulikuwa kuna mambo yamekosekana lakini yapo mazuri ambayo tunaweza kuyatumia.

“Baada ya maoni hayo kupelekwa Bungeni ikachujwa ikatoka inayoitwa Katiba Pendekezwa, ni mbovu kuliko hata katiba tuliyonayo sasa hivi.

SIZUNGUMZII SUALA LA LISSU KUPIGWA RISASI SABABU UTEKAJI ULIKUWEPOA CHADEMA
“Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

“Nitoe mfano iliwahi kutokea huko nyuma nikiwa Katibu Mkuu CHADEMA, nililetewa taarifa za mtu wangu anaitwa Joseph, huyu alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, alitekwa saa sita usiku. Kesho yake saa sita mchana nikahitisha mkutano na waandishi wa habari nikaisema sana Serikali na Usalama wa Taifa.

“Saa nane mchana siku hiyohiyo Joseph akapatikana, alikutwa ametupwa maeneo ya Ununio ameumia sana usoni.

“Mwezi mmoja baadaye kijana wangu wa Red Brigade anakuja kwangu kuniambia yeye ndiye aliongoza kukosi cha kwenda kumteka nyara huyo mwenyekiti huyo.

“Nikauliza kwa nini hakuja kwangu akasema ‘wapo viongozi wanaojua’, nikaamua kunyamaza, ndiyo maana ninapoulizwa suala la Lissu ninasema hapana, CHADEMA kwanza wajiangalie wao ndani.

“Huyo kijana (Joseph) walivyomtupa ufukweni walijua amekufa, kumbe alikuwa hajafa labda upepo ulimpiga akaamka. Miaka kadhaa baadaye tukaanza kusikia watu wanaokotwa wamekufa ufukweni, unadhani inatoa pcha gani!

“Ukiwa kiongozi lazima uwe kunasema ukweli hata kama unaona watu wako wanakosea.

SINA TATIZO LA LOWASSA
“Mimi na Lowassa tulipishana kwenye principal siyo maisha, mimi niliwahi kufanya fund rising na Jakaya Kikwete siku moja baada ya kupanda jukwaani na kumsema tena kwa mambo mazito.

“Nimeishi Ulaya, nimeona mambo ya kwenye mabunge, kuna muda inafika hatua wabunge wanapigana ngumi lakini wakitoka wanaenda kunywa bia. Unatakiwa kutofautisha maisha binafsi na siasa. Hivyo sikuwa na tatizo binafsi na Lowassa.

AWAMU YA TANO HAIKUFELI DIPLOMASIA YA KIMATAIFA
“Watanzania tuwe wakweli, tumefeli wapi, mimi nimekutana na wafanyabiashara wengi, wapo walioniambia wamchoshwa na Tanzania yenye ufisadi.

“Wapo walioamua kuondoa biashara zao huko nyuma lakini katika awamu ya tano waliamua kurejesha biashara hapa nchini, kwa nini? Ni kwa sababu kulikuwa kuna mambo mengi yanaenda vizuri, nazungumza kwa kuwa najua zaidi kilichokuwa kinaendelea.”

Chanzo: Dar24
kweli CHADEMA ni chama cha magadi! Na mwenyekiti wake alikutwa na mahakama kuwa ana kesi ya kujibu japo baadaye wakamshit!
 
Kwanini usubiri ukweli uropokwe na mtu wakati hii ni nchi yenye vyombo vinavyoweza kufanya uchinguzi vikaleta majibu.tofauti na hapo ni unafiki tu.
Ila akiropoka Lisu ni sawa.

Vyombo vyenyewe haviaminiki ndiyo maana tunasubiri ku-hear from the horse's mouth.
 
Chadema wamlete dreva wa lissu maana ndiye aliyewaona waliomshambulia, sasahivi wamemficha ubeligiji, kama kweli Chadema wanataka tujue ukweli kwanini wasimlete?haiwezekani mtu hapigwe risasi zote hizo alafu kuna mtu pembeni asipate hata mchubuko.Hapa kuna kitu kimefichwa.
Tunajadili hoja za Dr Slaa
 
Mtu gani amiminiwe risasi zote hizo alafu atoke?kingine mbona dreva wa lisu mbona hakupata hata mchubuko wakati walikuwa wote,na sasahivi wamemficha ubeligiji,kama kweli Chadema wanataka tujue ukweli wamlete dreva wa lissu maana ndiye aliyewaona wapigaji.
Tunajadili hoja ya Dr Slaa
 
Mi nadhani mlijipoteza wenyewe! Haiwezekani Lowasa mliyeshutumu na wizi wote ule, halafu anasimikwa kuwa rais wa nchi, hatukuona sehemu mlipomsafisha akang'ara maana alishachafuka, mkamweka pembe Dr Slaa!, leo nanyi anawaweka pembeni mnamwona mbaya!
Mkuki kwa nguruwe!
Elewa hoja, jadili hoja jikite katika hoja
 
"Kuna kipindi Mwenyekiti wetu @ChademaTz Wilaya alitekwa saa 6 usiku na kuumizwa akatupwa ununio. Mimi nikaita vyombo vya habari kukemea vyombo vya Usalama kuteka watu.Baada ya mwezi mmoja mmoja wa walinzi wetu wa chama akaniambia yeye alihusika kumteka" Dkt. Slaa
source😀ar24 https://t.co/hPjWe6288V
20220427_163040.jpg
 
Back
Top Bottom