Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Sikutarajia Slaa aongee tofauti na hivyo, eti wawekezaji walikuja awamu ya tano. Slaa anadhani kwakuwa aliwahi kuaminika hapo nyuma basi na sasa ataaminika.
Tumboni hakuna kitu anajua teuzi zinapatikana kwa kupiga yowe tumpuuze tu....
 
Siku hizi humu baada ya uzi ni matusi tu. Kwani mnaomtukana huyu mzee mnakosoa hoja ipi? Zamani watu wali quote sentensi na kupangua hoja! Mbona mambo mengi kaongea kwa ushahidi mzuri tu? Au mnataka kusikia yanayowasha masikio yenu tu!
Ushahidi wa kwamba aliletewa taarifa? kwanini hakuwaripoti polisi Msadieni Mzee wenu njaa itamuua Mtaani
 
Huyu mzee nitamtetea maeneo mengi bila kupepesa. Anaishi kwa principles kitu ambacho wanasiasa wetu wengi hawana. Hata umchukie vipi, facts zake hazibadilishwi kipropaganda.
Eti anaishi kwa principal huyu alieltewa habari za kutekwa kijana wake lkn akakaa kimya mpaka alipomaliza muda wake wa Ubalozi
 
Kuna watu wamepata access ndio wanafanya political spinning. Lakini hii inakwenda Bungeni na kupitia kamati zake facts zote zitafahamika.
..hoja kama hasara ktk mashirika ya umma nazo zinahitaji kusubiri wahusika wakajitetee ktk kamati ya bunge?

..binafsi ningefurahi kama mijadala ya kamati za bunge ingekuwa inaonyeshwa live au recorded.
 
Yaonekana, Dr Mihogo alipumbazwa na misifambuzi aliokuwa akimiminiwa na HASA mamluki wenzie/wahuni wa kijani.
Alikuja akaamini kuwa CDM bila ya yeye wangekwama. Sasa kakwama yeye mpaka nyumbani mwake.
Ana hasira sana HAYAMINI MACHO YAKE.....
 
Huyu atagombea urais ccm 2025. Mtakuja kuniambia wakiuu.
 
Na serikali wanafungaje hoja za CAG?
Hiyo platform ya kuongea na umma sio ya hao unaowashutumu kwa ulaghai wa kisiasa peke yao. Hamna anayeizuia serikali na chama chake kutolea ufafanuzi pale wanapoona wameonewa na CAG.
Na kama facts zipo ila zimepindishwa tu na watu wenye nia ovu, hiyo itakuwa sahihi. Ila kuwazuia watu kuongea mpaka mtakapokuwa na narrative mnayoipenda nyinyi sio haki. Hizo ndio cheap politics za kutumia ubabe kuzuia mjadala.

Amandla...
 
Ujua wao wanaamini Mbowe ni malaika na wanachadema wote ni wema! Nakuambia ukianikwa ubaya na maovu ya Mbowe watashika kichwa! Hata Sumaye aliambiwa sumu haionjwi!

Sirro alisema hivyo hivyo. Ajabu DPP akaondoa mashtaka ya ugaidi mahakamani wakati mahakama imeshathibitisha kuwa Mbowe ana kesi ya kujibu! Kama sio “uswahili” huo ni nini?

Hii ni serikali ya ajabu. Yaani ishindwe kumshughulikia Mbowe kisheria, itegemee sisi tushike vichwa kwa ubaya na maovu yake kuanikwa! Halafu akishasutwa ndio basi! Tangu lini nchi ikaendeshwa kwa mipasho na taarab?
 
Huyu mzee nitamtetea maeneo mengi bila kupepesa. Anaishi kwa principles kitu ambacho wanasiasa wetu wengi hawana. Hata umchukie vipi, facts zake hazibadilishwi kipropaganda.
Kama kweli nawe wayaamini hayo kutoka moyoni mwako, yafaa BASI uungane nae mkiwa na Madeluu muwapitie Dr Mollel, Mwita Waitara, Lijualikali, Ndugai na Suzana Masele, muyapeleke kwa Kingai, muanzishe kesi nyingine ya ugaidi.
 
Lissu hana haja ya kumjibu Slaa. Ila Slaa anazeeka vibaya. Pole mzee baba.

Au tumepata Msiba namba mbili?
 
Huyu mzee nitamtetea maeneo mengi bila kupepesa. Anaishi kwa principles kitu ambacho wanasiasa wetu wengi hawana. Hata umchukie vipi, facts zake hazibadilishwi kipropaganda.
Kama kweli nawe wayaamini hayo kutoka moyoni mwako, yafaa BASI uungane nae mkiwa na Madeluu muwapitie Dr Mollel, Mwita Waitara, Lijualikali, Ndugai na Suzana Masele, muyapeleke kwa Kingai, muanzishe kesi nyingine ya ugaidi.
 
..hoja kama hasara ktk mashirika ya umma nazo zinahitaji kusubiri wahusika wakajitetee ktk kamati ya bunge?

..binafsi ningefurahi kama mijadala ya kamati za bunge ingekuwa inaonyeshwa live au recorded.
Zipo hoja za CAG zinastahili mjadala maana hazistahili utata na zina direct impact na results zake ni hasara, hata ikipewa majibu ni sababu ya hasara iliyokwishatokea. Ila tatizo ukifatilia kwa makini report ya CAG inavyojadiliwa imejaa hatari ya kutumika kisiasa kuliko uhalisia.

JF huko nyuma watu walileta hadi screen shot ya sections za CAG report kujadiliana. Sasa hivi mtu anakuja na note book anaitisha press au kuandika JF na kutuhumu tu. Alafu hapa tunaangalia aliyesema au kuandika na kama ni mizania tofauti na yako ni kupinga au kuruka nayo kama vile tayari tuna facts.

Siasa za nchi yetu haziko kwenye hali nzuri maana kuna makundi yaliyotawala na kusigana ikijumuisha vyama vyote na kubakiza vyama kama vivuli tu. Sisi huku tunalishwa na hiyo misigano na kama tusipokuwa watu wa kutulia na kufatilia facts tutakaangana sana.
 
Siku hizi humu baada ya uzi ni matusi tu. Kwani mnaomtukana huyu mzee mnakosoa hoja ipi? Zamani watu wali quote sentensi na kupangua hoja! Mbona mambo mengi kaongea kwa ushahidi mzuri tu? Au mnataka kusikia yanayowasha masikio yenu tu!
Ushahidi mzuri ni upi hapo?.au mtu kueleza mtazamo wake ambao unaweza kua sio kweli kwako ndo ushaidi mzuri?
 
We unafikiri KWA heshima ya Dr.slaa enzi na enzi angeamua kuuza utu wake KWA pesa angekua wapi?Mmezoea wanasiasa malaya malaya ndo Tatzo,leo mnamuita Fisadi kesho ndo apeperushe bendera ya chama
Msimuache basi, mchukueni huko kwenye vyama vyenu, ili akili yake itulie.
 
AMEN
 
Facts gani unazozingumzia? Report yeyote inaweza kutumika kisiasa maana hizo unazoita facts zinategemea anaezitafsiri ni nani. Wanasiasa kutumia ripoti ya CAG kisiasa sio dhambi. Sisi wananchi tutafaidika kwa kuona pande mbili au tatu za hizo "facts" na kujifanyia maamuzi yetu maana sisi ndio maboss wao.

Usituambie kuhusu hizo JF za huko nyuma maana tulikuwepo. Na kilichokuwa kinafanyika ni hiki kinachofanyika hivi sasa. Mjadala wa wazi kuhusu taarifa bila upande mmoja kutuambia tusubiri mpaka tutafuniliwe kwanza. Unadhani watu wangegoja Kamati za Bunge zijadili masuala ya IPTL na shutuma nyingine ndio wajadili kuna kitu kingefanyika? Huyo Slaa mwenyewe alisimama Mwembe Yanga na aliwashutumu watu bila kungoja taarifa ya kamati za Bunge. Leo amehamia upande wa pili ndio anataka na sisi tumfuate! Ukigeu geu wake abaki nao. Sisi tutampinga kila anapotaka kutupotosha bila kujali kuwa kuna wakati alisimamia upande wa haki.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…