Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Njaa mbaya sana, mzee anafukuzia kauteuzi laki anakosea step, kuegemea Sukumagang kunamkosesha teuzi
Yaani mzee ameshindwa kutambua kuwa atumie njia ipi kupata uteuzi? Si kweli ila anaouongea ndio ukweli kwa sababu anaongea wakati anajua kabisa hakuna anayemfurahisha hapo.
 
Hii aya hii...!Eeheeeee!
 
Jamani mbona watanzania hatujui hata tunachokitaka? Mfano yeye ameelezea swala la sheria wewe unasema mtazamo wake. Hivi watanzania tunataka katiba ya nini sasa wakati hatutaki sheria zifuatwe?
 
Alikuwa sehemu ya uhuni kama wahuni wenzake!

Je, aliripoti wapi!?
Alikaa kimya akichumia tumbo lake!
Shame. Huyu ndiyo angekuwa eti raisi!
Huyu na huyo mwenzake wakamatwe kwa kuhusika na utekajo .katujakikishia kuwa alijua hilo na akanyamaza na pia muhusika ni mlinzi wake
Ndo maana chadema ya kipindi chake ilikuwa ma matukio kuliko hii ya sasa
 
Jamani mbona watanzania hatujui hata tunachokitaka? Mfano yeye ameelezea swala la sheria wewe unasema mtazamo wake. Hivi watanzania tunataka katiba ya nini sasa wakati hatutaki sheria zifuatwe?

..Tunataka sheria nzuri, sio sheria zinazolinda watawala wabadhirifu.

..Watanzania wanadai Katiba mpya kwasababu iliyopo ni mbaya na imepitwa na wakati.
 
Ni kama vile sina uhakika nani alimpiga risasi Lissu lakini baada ya kumsikiliza Lissu na Slaa, najua Slaa ni muongo au disingenious.
Slaa anapotosha pale anapotoa mfano wa redbrigade akionyesha huenda limefanywa na Chadema. Fair enough! Slaa huyo huyo hajaeleza kwanini walinzi waliondolewa siku ya tukio na wapi Camera zilipelekwa. Walinzi na Camera ndizo zingetupa jibu ni akina nani.
Tena anakiri swali hilo anaulizwa sana, sijui kama hajui kwanini anaulizwa! na kwanini ana majibu yasiyo na mashiko
Slaa anaelewa taratibu zilikukwa kwa ushahidi. Kwanza, walisema hawakupokea barua, Chadema wakaonyesha ''dispatch'' na kuzima uongo wa Job Yustino Ndugai

Chadema wakakana hawakupeleka majina.
Katika utawala bora ilitosha Spika kujiridhisha vyombo vya dola vingehusishwa, halikutokea.
J Y Ndugai akawaita Wanawake uani akawazawadia ubunge kwa kukiuka taratibu na ubabe tu akijua yeye ni msaidizi wa 'mungu'

Tuhuma za kughushi nyaraka ni nzito tena ikifanywa na TUME ya Uchaguzi.
Serikali ingeingilia lakini haikufanya hivyo. Slaa anasema waende Mahakamani! come on!
Anasema kuwa wawekezaji walikuwepo wakati wa awamu ya tano lakini viongozi wa chama chake kila kukicha wanatuambia kuwa wawekezaji wanaRUDI baada ya milango kufunguliwa tena.
Mawaziri wanasema hali ilikuwa mbaya sana. Rais SSH anasema wawekezaji ' Wanarudi'
Wanarudi kutoka wapi? Siyo wanakuja bali wanarudi ina maana waliondoka

Slaa muongo ongo tu ! maisha haya ya uongo ni ya kudhalilika sana
Slaa wa sasa haaminiki kabisa. Which is a shame maana kuna wakati tulimuamini sana. Kama ilivyokuwa kwa Mrema
Siyo kwamba haaminiki tu sijui kama ana heshima nyingine iliyobaki.

Anachokifanya ni ' kutaka kusikika' ili teuzi za bodi n.k. asiachwe.
Maisha ya dhalili sana

Waliomdhuru TL wanataka maridhiano hata CCM wanalaani!

Slaa anajipaka damu za watu bila sababu ! ni njaa gani hii?

Kwamba ana tupa principles , values na heshima kwa njia za hoovyo!
Anaonekana kituko mbele ya dunia!
 
Nimeconcentrate kwenye loss ili kuua upotoshaji wa makusudi wa Jpm aliokuwa anaufanya kwa shirika la ndege..
Again nimerefer procurement process ili kuuleta uwanja wa ndege wa chato
Specifically nimerebutt claims na matendo ya mwendazake
But tunaweza kwenda query kwa query ya ripoti ya CAG kuonesha kuwa misappropriation nyingi hoja zake zipo conclusive ukichukulia walipewa siku 21 kujibu hoja..
By the way CAG anatoa opinion either qualified,unqualified au disclaimer.
Nisaidie ripoti ya taasisi yoyote aliyosema kuna ubadhirifu.
 
Naanza kuona mbadala wa jpm kwa mbali
Nahitaji watu wa kweli na wawazi
 
Jamani mbona watanzania hatujui hata tunachokitaka? Mfano yeye ameelezea swala la sheria wewe unasema mtazamo wake. Hivi watanzania tunataka katiba ya nini sasa wakati hatutaki sheria zifuatwe?
sheria gani aliyosema?
 
sheria gani aliyosema?
mimi si mtaalamu wa sheria lakini Dr Slaa ametaja kitu hapo. Kama ni mtaalamu wa sheria ndiyo fuatilia.

“Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu."
 
“Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu."
Kuandika sheria haijibu hoja ya Zitto
Slaa anapaswa kueleza upotoshaji upo wapi na ajibu hoja kwa mantiki si general
 
CHADEMA NJOONI MJIBU
 
"2015 vyama vya siasa vilisimamisha wagombea kila mahali lakini bado CCM ilipita bila kupingwa"

Hiyo nukuu yako hapo juu inaonesha hujui unachoandika, unajifurahisha tu, sioni sababu ya kukujibu.
 

Hivi kweli tunahitaji kuumiza kichwa kujua kwanini propaganda hizi zinakuja sasa tena kwa kumtumia Dr Slaa ambaye amewahi kuwa mtendaji mkuu wa CHADEMA..?

Jibu ni moja au mawili tu kuhusu hili;

MOSI; Hii yote ni kujaribu kuipotezea ishu ya TL kupigwa risasi na bila wahusika kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria..

Lakini kulipotezea hili haiwezekani kwa sasa kwa sababu calculation ya namna ya kuutekeleza uuaji huo ulikosewa na kuvurugika kabisa beyond reparable kiasi cha tukio zima limekuwa Zimwi linalowawinda na kutaka kuwatafuna wahusika wenyewe...!!

MBILI; Kuuineza propaganda hii kwa namna anavyofanya Dr Slaa (kama kweli wameamua kumtumia) ni ujinga na upumbavu usioweza kueleweka kirahisi kwa watu...

Maana kama jaribio la kuuwawa Tundu Lissu ni INSIDE JOB ya CHADEMA yenyewe, kwanini mpaka leo vyombo vya uchunguzi na kisheria - polisi wasiingie huko CHADEMA na kuwachunguza na kuwafikisha ktk vyombo vya sheria wahusika? Je, wanawaogopa CHADEMA? If so, why waogope?

Pamoja na yoyote, lakini kwa hatua na muda ambao ishu hii imefikia, hakuna mjinga yeyote anayeweza kumwamini yeyote asemaye kuwa, eti Tundu Lissu alitaka kuuwawa na CHADEMA wenyewe...!

Ingekuwa hivi kweli, Mwendazake Magufuli aliyekuwa na chuki na hiki chama, nakuhakikishia angelishalala mbereee na CHADEMA kwa kuiondolea mbali ktk uso wa dunia kabla yeye mwenyewe hajafutiliwa mbali kwa kifo cha aibu katika Zahanati ya Mzena, DSM March 17, 2021...!!!!

Waliojaribu kumuua Tundu Lissu wanajulikana na ni haohao wanaopaswa kuchunguza tukio hili. Na wa kwanza wao tayari, hukumu ya kifo ilishapitishwa juu yake. Si mwingine bali ni aliyekuwa Rais wa Tanzania (2015 - March 17, 2021) Hayati, Mwendazake na Dikteka Uchwara John Pombe Magufuli...!!
 
Kama vile nakuona unavyogugumia kwa maumivu😂😂😂 Amesha lala mwenzako Mungu aliamua apumzike asije dhalilika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…