Sijawahi kufikiria kama Dr. Slaa anaweza kuwa mnafiki kiasi hiki! Kwa umri wake, hastahili kuwa hivyo. Lazima kuna kitu hakipo sawa kichwani au moyoni mwake.
Kama CHADEMA walijaribu kumwua kiongozi wao, yeye Dr. Slaa alikuwa kiongozi kwenye Serikali ya awamu ya 5, tena Serikali iliyouchukia sana upinzani, serikali iliyokuwa tayari hata kuyatengeneza makosa dhidi ya wapinzani ili kuwakomoa/kuwakomesha, alishindwa nini kuitoa hiyo taarifa? Jinai huwa haifi.
Polisi wanatakiwa kumkamata Dr. Slaa na kumhoji kuhusika kwake na utekaji na kukusudia kumwua mtu aliyemtaja. Yeye alikuwa mtendaji mkuu wa chama. Kama kuna uovu uliofanywa, yeye aliyekuwa mtendaji mkuu, ndiyo mahali sahihi pakuanzia. Hata kama hakushiriki, bado ana hatia. Maana kujua kuwa kuna uovu umetendeka halafu ukakaa kimya, ni hatia.
Lakini pia tujiulize, aliyetekwa na kujaribu kuuawa ni mzima, alinusurika, kwa nini hakwenda kushtaki, wakati watekaji walikuwa wanafahamika?