Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Kwaiyo unaamini maneno ya lissu yalikuwa yakweli ili ya Dk Slaa ni uongo, wakati wote ni wanasiasa,Slaa hajawi kuwa mwongo ndio maana alisumbua sana CCM maana yote aliyokuwa akiyasema ulikuwa ukweli mtupu wakashindwa hata kumpeleka mahakamani,sasa nyie Chadema kama mnasema amewachafua kafungueni kesi, tujue mbivu na mbichi.
Aliyeisumbua ccm ni Lowassa hadi wabunge waliongezeka.
Slaa aliahidi kumfunga jpm lakini badae akannuliwa akawa mtetezi wake!!
 
Hajasema hivyo! Amesema ile rasimu ya Warioba ilichakachuliwa zaidi na ndio mbovu kuliko hata hii ya sasa! Facts hata kama humpendi,

Hapana kaka, tusubiri majibu ya hoja baada ya ukaguzi kupitia kamati ya bunge ili zile ambazo hazina majibu ndio ziwe mjadala.

Auditor anapotoa findings report huwezi kutuhumu mpaka wahusika watoe majibu! Mfano figure tunayoambiwa ni ufisadi ukichunguza kwa makini ni queries wanapaswa kuzitolea maelezo with evidence na si ufisadi!

Mfano kama kuna viambatanisho havijawa presented hadi Auditor ameondoka itabaki pending hadi umpatie! How report ya CAG ambayo inakwenda Bungeni kwaajili ya kamati za Bunge kuhoji wahusika then mandumilakuwili waitumie kutuhumu watu? Purely politics! Hii imewahi kuikumba Chadema na kutumika kwa propaganda hadi walipopeleka vithibitisho!

Audit findings zitageuka tuhuma zikikosa majibu kwa kamati ya Bunge. Tuwe fair, majibu yakikosekana wahusika wote wachukuliwe HATUA! Ikiwemo waliokuwa mawaziri. Kwa kiasi kikubwa hii taarifa jinsi inavyojadiliwa ni kisiasa tu! Muda utaongea.
Hapa unaongelea attachments
Swala la kukiuka taratibu za ununuzi,kampuni kupata hasara ni hoja ambazo hazihitaji hiyo kamati
Majibu unamalizana na auditor hapo hapo
 
HEBU TUJADILI HII STATEMENT YA @drslaa

[emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541]

SIZUNGUMZII SUALA LA LISSU KUPIGWA RISASI SABABU UTEKAJI ULIKUWEPOA CHADEMA
“Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

“Nitoe mfano iliwahi kutokea huko nyuma nikiwa Katibu Mkuu CHADEMA, nililetewa taarifa za mtu wangu anaitwa Joseph, huyu alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, alitekwa saa sita usiku. Kesho yake saa sita mchana nikahitisha mkutano na waandishi wa habari nikaisema sana Serikali na Usalama wa Taifa.

“Saa nane mchana siku hiyohiyo Joseph akapatikana, alikutwa ametupwa maeneo ya Ununio ameumia sana usoni.

“Mwezi mmoja baadaye kijana wangu wa Red Brigade anakuja kwangu kuniambia yeye ndiye aliongoza kukosi cha kwenda kumteka nyara huyo mwenyekiti huyo.

“Nikauliza kwa nini hakuja kwangu akasema ‘wapo viongozi wanaojua’, nikaamua kunyamaza, ndiyo maana ninapoulizwa suala la Lissu ninasema hapana, CHADEMA kwanza wajiangalie wao ndani.

“Huyo kijana (Joseph) walivyomtupa ufukweni walijua amekufa, kumbe alikuwa hajafa labda upepo ulimpiga akaamka. Miaka kadhaa baadaye tukaanza kusikia watu wanaokotwa wamekufa ufukweni, unadhani inatoa pcha gani!

“Ukiwa kiongozi lazima uwe kunasema ukweli hata kama unaona watu wako wanakosea.
Kauli inafikirisha sana hii.
 
Hapa unaongelea attachments
Swala la kukiuka taratibu za ununuzi,kampuni kupata hasara ni hoja ambazo hazihitaji hiyo kamati
Majibu unamalizana na auditor hapo hapo
Sio attachments tu, unaweza kupata Audit findings hata 50 pages zenye figures za kutisha lakini hadi hoja inafungwa zimebaki page 2 tu. Yanayoendelea ni purely politics!
 
Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

Angeishia hapo ingekuwa amefanya Busara sana...
 
Chadema punguzeni kujipa matarajio na matumaini hewa, fanyeni kwanza chama/chadema assessment kwa wananchi mpate maoni kamili kuliko kutegemea mitandao tu ambayo penetrations yake ni kidogo, mwaka 2010-2015 hamasa ya mageuzi ilikuwa kubwa sana kutoka na jitihada kubwa zilizofanywa na upinzani wakati huo Dk slaa, Lissu, Zitto, Mkumbo, Prof safari, Lipumba, Maalim seif , mwamuko ulikuwa mkubwa na agenda kubwa ilikuwa ni rushwa na kuwatetea wananchi walio chini, kuja kwa Lowasa pamoja na hamasa iliyokuwepo iliongeza hamasa hivyo kupata wabunge wengi mwaka 2015 lakini bado CCM ilishinda, siasa zilibadilika ghafla kuanzia mwaka 2015 baada ya agenda karibu zote tulizokuwa tuna pigania kuanza kufanyiwa kazi, CCM ikakubalika tena, ndugu zangu mimi sijawahi penda ccm maisha yangu yote ila speed ya mwaka 2015 hadi 2020 chini ya msukuma yule ( Magufuli) haikuwa ya kawaida, upinzani agenda ikafa tukabakiwa na matukio na matusi mitandaoni, kwa ufupi tukapoteana, tukaja na conclusions kuwa tuliibiwa kura mwaka 2020, lakini ukweli halisi tulishindwa vibaya sana mwaka 2020 , wananchi walio wengi waliamini tena ccm, watu wanasomeshewa watoto wao bure ulitegemea wata mpigia kura nani?

Mimi nimeshiriki mikutano mingi ya Tundu Lissu Dar na mikoani, walikuwa wana msikiliza tu lakini baada ya hapo majority wengi walidai kura za uraisi ni Magufuli, sijui Magufuli aliwafanyia nini, sasa chadema kama chama kikubwa cha upinzania kifanye assessment kwanza na kipate report ya matukioa yote kuanzia mwaka 2015 hadi leo, kitapata picha halisi na kuja na sera mbadala, maana dunia inabadilika hivyo sera pia zina badilika kulingana na mabadiliko ya dunia na uongozi wa sasa.
 
Nampenda Dr. Slaa. Yeye husema ukweli. Anatufaa sana kuwa Rais wetu.
Pengine Rais wa MATAGA, lakini siyo Rais wa nchi hii. Aliharibikiwa akili baada ya kununuliwa na mwendazake. Mshumbusi akamalizia hata ile akili kidogo aliyokuwa anasimamia ubalozi. Sasa hivi ni kopo tupu.
 
Dr. Slaa asaidie polis kumbe anajua maovu mengi Sana kwa nini anyamaze visa vya utekaji?mwanasheria gani ananyamazia uvunjaji wa Sheria?
 
Sasa mbona hawachukuliwi hatua na vyombo husika? Slaa tushamzarau yeye zito lipumba afadhali lungwe anajua kusimamia anachokiamini.
Hamchukuliwi hatua kwa sababu tu mnavumiliwa kisiasa ili kubalance mambo
 

Mwanasiasa Willbrod Peter Slaa amefanya mahojiano na kuzungumza mambo mengi kuhusu siasa, mahojiano haya ni mwendelezo ya interview aliyofanya wiki iliyopita.

TAARIFA YA CAG INAPOTOSHWA
“Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu.

“Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.

“Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG.

CAG AMESABABISHA TAHARUKI KWA RIPOTI YAKE
“Kwanza hata CAG mwenyewe amechangia kuleta hii taaruki kwa kuwa huwa ni ya awali tu na analijua hilo, inatakiwa irudi kwa akaunti ofisa wa Serikali ijadiliwe, pia CAG wakati anatoa taarifa zake hadharani hatakiwi kuingia ndani kutoa ufafanuzi zaidi kama anavyofanya.

“Unaweza kukuta ripoti hiyo ikifika kwenye Kamati ya Bunge vitu vingi vikawekwa sawa, mfano labda kulikuwa na upotevu fulani wa mambo madogomadogo ambayo kwa nje yanaonekana kama ni wizi lakini details zikiwekwa sawa kunakuwa hakuna tatizo.

UBUNGE WA KINA MDEE SPIKA HANA KOSA, NITAZUNGUMZA CHADEMA WAKISHAKAA KIKAO
“Nimeona kwenye vyombo vya habari kuwa watajadiliwa na chama chao katika rufaa yao, naona lawama zimepelekwa kwa mtu ambaye hausiki (Spika).

“Chama kilitakiwa kufungua kesi Mahakamani kuhoji Tume ya Uchaguzi kwa kupitisha majina hayo lakini sijaona kesi. Mimi nitazungumza baada ya rufaa yao kupitiwa na CHADEMA, nimesikia wanakaribia kuwajadili kwenye kikao chao.

HOJA YA KATIBA SIYO MAHITAJI MUHIMU YA WANANCHI
“Mabosi wa vyama vya siasa ni wananchi, wanatakiwa kujiuliza wanayoyafanya yanawagusa vipi wananchi, kwa sasa kuna mambo mengi ya muhimu lakini hivyo vyama vimekuwa bize kuzungumza habari za ajenda ya Katiba.

“Hawana ajenda ambazo mwananchi anaweza kujiuliza kama inaweza kuweka chakula mezani, hakuna katiba ambayo inaweza kuzungumzia kila kitu.

“Katiba yetu ina vipengele vingi vya muhimu lakini havitekelezwi, japo sijasema kuwa katiba siyo muhimu.

“Mimi ni kati ya watu waliozunguka Tanzania kukusanya maoni lakini tusipotoshe kuwa katiba ndiyo jibu la kila kitu, siyo kweli.

“Leo hii Marekani ina katiba tunayoisifu lakini Donald Trump si alishutumiwa anataka kufanya mageuzi.

KATIBA PENDEKEZWA NI MBOVU KULIKO KATIBA YA SASA
Sisi tuna maoni ya Jaji Warioba, licha ya kuwa kulikuwa kuna mambo yamekosekana lakini yapo mazuri ambayo tunaweza kuyatumia.

“Baada ya maoni hayo kupelekwa Bungeni ikachujwa ikatoka inayoitwa Katiba Pendekezwa, ni mbovu kuliko hata katiba tuliyonayo sasa hivi.

SIZUNGUMZII SUALA LA LISSU KUPIGWA RISASI SABABU UTEKAJI ULIKUWEPOA CHADEMA
“Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

“Nitoe mfano iliwahi kutokea huko nyuma nikiwa Katibu Mkuu CHADEMA, nililetewa taarifa za mtu wangu anaitwa Joseph, huyu alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, alitekwa saa sita usiku. Kesho yake saa sita mchana nikahitisha mkutano na waandishi wa habari nikaisema sana Serikali na Usalama wa Taifa.

“Saa nane mchana siku hiyohiyo Joseph akapatikana, alikutwa ametupwa maeneo ya Ununio ameumia sana usoni.

“Mwezi mmoja baadaye kijana wangu wa Red Brigade anakuja kwangu kuniambia yeye ndiye aliongoza kukosi cha kwenda kumteka nyara huyo mwenyekiti huyo.

“Nikauliza kwa nini hakuja kwangu akasema ‘wapo viongozi wanaojua’, nikaamua kunyamaza, ndiyo maana ninapoulizwa suala la Lissu ninasema hapana, CHADEMA kwanza wajiangalie wao ndani.

“Huyo kijana (Joseph) walivyomtupa ufukweni walijua amekufa, kumbe alikuwa hajafa labda upepo ulimpiga akaamka. Miaka kadhaa baadaye tukaanza kusikia watu wanaokotwa wamekufa ufukweni, unadhani inatoa pcha gani!

“Ukiwa kiongozi lazima uwe kunasema ukweli hata kama unaona watu wako wanakosea.

SINA TATIZO LA LOWASSA
“Mimi na Lowassa tulipishana kwenye principal siyo maisha, mimi niliwahi kufanya fund rising na Jakaya Kikwete siku moja baada ya kupanda jukwaani na kumsema tena kwa mambo mazito.

“Nimeishi Ulaya, nimeona mambo ya kwenye mabunge, kuna muda inafika hatua wabunge wanapigana ngumi lakini wakitoka wanaenda kunywa bia. Unatakiwa kutofautisha maisha binafsi na siasa. Hivyo sikuwa na tatizo binafsi na Lowassa.

AWAMU YA TANO HAIKUFELI DIPLOMASIA YA KIMATAIFA
“Watanzania tuwe wakweli, tumefeli wapi, mimi nimekutana na wafanyabiashara wengi, wapo walioniambia wamchoshwa na Tanzania yenye ufisadi.

“Wapo walioamua kuondoa biashara zao huko nyuma lakini katika awamu ya tano waliamua kurejesha biashara hapa nchini, kwa nini? Ni kwa sababu kulikuwa kuna mambo mengi yanaenda vizuri, nazungumza kwa kuwa najua zaidi kilichokuwa kinaendelea.”

Chanzo: Dar24
This is a voice of a destitute. It is a struggle for survival. He is in the cold.
 
Dr. Slaa asaidie polis kumbe anajua maovu mengi Sana kwa nini anyamaze visa vya utekaji?mwanasheria gani ananyamazia uvunjaji wa Sheria?
Huyu mzee amshukuru sana Mbowe kmuwekea bondi ili kulinda image yake demu wake (mama junior) angekuwa magereza kwa kufoji sahihi ya huyo mzee kukwapua milioni 200 za umma
 
Sio attachments tu, unaweza kupata Audit findings hata 50 pages zenye figures za kutisha lakini hadi hoja inafungwa zimebaki page 2 tu. Yanayoendelea ni purely politics!
Nakubali kwenye attachments lakini hasara ya kampuni ni kitu kipo wazi kwenye financisl statements.
Ukiukwaji wa procurement process hakuhitaji kamati ya bunge..
Kufoji viza uhamiaji hakuhitaji kamati ya bunge..
Kukiuka mkataba na wakandarasi wa bwawa la nyerere na kusababisha mradi kuchelewa hakuhitaji kamati ya bunge.
So on and so forth..
Kumbuka pia audit ni rule based na principle based
Rules ni siasa lakini principles ni standard za ukaguzi ambazo ni universal.
 
Lissu Ile siku amesema walivyomteua Lowassa kua mgombea wao kupitia CHADEMA walivyoenda nyumbani kwa Dr. Slaa walikuta mkewe amemfungia nje ya mlango amemtupia na mashuka,Slaa akawa analala kwny Noah yake 😁😁😁,mpk leo Dr. Mihogo hataki kabisa kumsikia Lissu
Na alitamani afe siku Ile alipopigwa risasi.
 
Back
Top Bottom