Dkt. Slaa kurejea CHADEMA? Tume ya Warioba ilitugharimu vikao vingi vya ndani

Dkt. Slaa kurejea CHADEMA? Tume ya Warioba ilitugharimu vikao vingi vya ndani

Rasterman

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
33,894
Reaction score
44,117
Dr Slaa leo tar 13 Dec 2022 akiwa ktk Mtandao wa Club house kwenye mjadala unaoendelea kuhusu mahitaji na Katiba Mpya, na Demokrasia nchini.

Dr Slaa anasema wanaisemea sana CHADEMA kwa kuwa ndio Chama chenye Nguvu.

Hata hivyo amesema madai ya Katiba Mpya bado yanahitaji maridhiano kati ya vyama vya siasa, wananchi na serikali kwa kuwa serikali na ccm ndio wenye mpini.

Anadai kwa kusema kihistoria hata mafanikio ya kuundwa Tume ya Katiba Mpya chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba ilichukua hatua mbali mbali za Dr Salaa pamoja na wenzake kwenda kufanya mazungumzo Ikulu ya Rais miaka ya 2012.

Mkutano huo unaofatiliwa na Maelfu ya Watanzania na kuungwa mkono na wanasiasa nguli kama
Dr. Lwaitama
Dr Slaa
Mh Lema
Na wadau wengi.

Naye Dr Lwaitama amemsifu na kumpongeza Dr Slaa kwa maoni yake mazuri yanayoonesha mwelekeo mzuri ambao unaonesha kweli Katiba Mpya ni hitaji la watanzanua wengi.

Akiongea moderator wa Mjadala ambaye hakufahamika jina lake haraka, alisema inawezekanaje Mh Rais wa Tanzania ameenda Marekani kimya kimya tofauti na ziara zingine?
 
Kuna tesisi anaandaliwa kumrithi Mbowe ingawa Chadema Kindakindaki na Chadema Wakuja wanavutana wakati Chadema Kindakindaki wanadai ni wakati sasa Mwenyekiti Taifa kutoka Mkoa wa Mara na chapuo anapigiwa Heche. Kundi la Chadema Wakuja wao wanapinga nafasi ya Mwenyekiti wa chama kutoka nje ya Kaskazini na ndio wanapambana kumrejesha Rais wa Mioyo ya Wadanganyika Daktari Slaa.
 
Leo yupo kwenye ubora wake aisee hizo nondo noma
Pia ameongeza kuwa hayuko tayari kukalia kimya mambo ambayo hayana faida kwa Taifa. Anataman8 katiba mpya ili kuepusha watu wanaong'ang'ania kutawala na kulipeleka taifa kwenye machafuko.
 
Back
Top Bottom