Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Hawa wazee MUNGU awasaidie sn wanapigania taifa letu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbarawa anatakiwa anyongwe harakaWatu walitanguliza asali mbele bila kujali wanaingiza nchi kwenye utumwa.......IGA ya kimchongo.
Watu wengine Huwa mnatafutwa kutukanwa bila sababu ya msingiIvi vikosi maalum kwann hawa mbwa koko amuwapigi risasi ,wanaleta taaruki kwenye ardhi ya amani
Fuatilia yanayojiri kwenye mkutano wa waandishi wa habari unaoendelea muda huu ambapo Dkt. Slaa, Mwabukusi na Mbatia wanazungumza.
Wakili Mwabukusi anazungumza
Juzi walitaka kubadilisha makubaliano ya Mkataba huu kati ya Taifa letu na kikampuni ambacho sidhani hata kama BRELA kipo.
Sisi hatushughuliki na Dubai Emirates wala DPW, sisi tunashughulika na Bandari yetu. Wengi wanasema mkataba ule wa kimataifa hivyo una defeat sheria za ndani. Kwa makusudi hawataki kusoma Geneva law of treaty ambayo inafafanua kuwa kwenye hali kama hizi mkataba huu hauwezi kuzidi sovereignty ya nchi. Walitusingizia uhaini wakatutoa, tunaanzia hapo tulipoishia.
Hili tunamkabidhi Mungu upande wa kushughulika na yaliyo nje ya mipaka ya binadamu, lakini yale ya kisheria hatumuachii yeye, tutakabiliana nao.
Kama walidhani wananitisha walifanya kosa kubwa sana, mimi sitishwi. Kama unafuata sheria za nchi nitakuheshimu, kama unatumia cheo sitakuheshimu. Kama nimekosea niadhibu kisheria pasipo kutunga makosa.
Sijui hata kutumia manati, ugaidi nitaifanya nini? Hii IGA nitaipinga, na Mungu atatupa uhai hadi tutakaposherekeka kufutwa kwa IGA. Hatutaruhusu laana hii katika malango ya nchi. Hoja za Bandari hazihitaji risasi, Serikali itujibu kwa hoja.
Sisi tukivunja mkataba watakamata ndege zetu, wao wakivunja mkataba wanaondoka bure. Wenzetu wakatoliki walitoa waraka, tumekubaliana wakati RC wakisoma waraka huu na kujuzana, tuipe Serikali na Bunge siku 30 ili lishughulikiwe.
Wastaafu kama hawawezi kuishauri kwa haki Serikali wakae kimya. Tumetoa siku 30, tunaanza kufanya kazi kubwa ya kufika mikoani, tutakuwa na mikutano 3 kwenye mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya kueleza madhara ya huu mkataba.
Polisi kama wanapenda sana siasa wastaafu, sisi tunazungumza hoja za kisiasa wao wanataka kutuua. Vyombo vya usalama vimsaidie Rais kumuonesha madhira ya mkataba huu, wakae nae kitaalamu wampitishe. Kama wao wanashindwa wasitumie Bunduki, watuite tuzungumze.
Baada ya siku 30 tutaitisha maandamano ya amani na sitojificha, hatutaacha kuandamana hadi IGA iondoke, isipoondoka tutaandamana milele, tutawataarifu Polisi.
IGP Wambura, kama una hoja niite, kaa na wataalamu wako nije tuzungumze, usitume vijana kutukamata usiku kutuweka korokoroni, ukiniita nitafika ili kama ni uchochezi nikuchongee wewe. Hatutaki cheo wala upendeleo wowote.
Quran na Biblia zote zinakemea ufisadi, tukemee mafisadi yote.
Dkt. Slaa anazungumza
Tunawashukuru kwa jitihada za kutotoa japo sisi tulitamani tuendelee kubaki.
Kama uhaini huwa unafanywa kwa namna hii basi tutaufanya sana. Yesu Kristu aliuawa, mimi ni nani nipelekeni tu mnakotaka kama ni kukata shingo nikateni.
Hatuogopi kifo, ilimradi tunajua tunasimamia nini. Hakuna kifo chenye heshima kama kufia ukisimamia maslahi ya nchi yako.
Serikali, wananchi, vyama vya siasa hawaelewi kuhusu katiba. Wakizungumza wanazungumzia uchaguzi. Juzi kuna taasisi moja imezungumzia tume huru, watu wanakufa wewe unazungumzia Tume ya Uchaguzi?
Kinachotokea katika nchi yetu ni kichekesho, katiba ya 1977 iliandikwa kama appendix ya CCM, kitu fulani kinachoning'ingia, kitu kisicho na umuhimu. Wananchi hawajawahi kupewa nafasi, hawajawahi kutengeneza katiba yao.
Bunge la CCM lilijigeuza wakawa Bunge maalumu kutengeneza Katiba, tafuta mwaka 1977 CCM walikuwa wangapi? Ni lini mwajiriwa anaandaa mkataba wake mwenyewe? Serikali tunaiajiri sisi, Rais tunamwajiri sisi. Kinachofanyika ni kama Rais anatengeneza mkataba wenye masharti anayotaka yeye.
Katiba hii ya sasa ilijadiliwa kwa saa 2 tu, kama sikosei wabunge walioongewa walikuwa 8 au 9. Tumeona mchezo wa 1977 unataka kujirudia tena kwa hali mbaya zaidi.
Katiba haianzishwi kwa mdomo tu wa Rais, huanzishwa kwa muswada. nchi yetu inaongozwa kishamba. Sasa nawauliza, hivi tunaakili au tumegeuzwa kuwa nyani (kufundishwa umuhimu wa katiba kwa miaka 3). Mimi kwa akili yangu ya kawaida watanata kutupiga.
Bunge limegeuka kuwa sehemu ya Serikali badala ya kusimama upande wa wananchi na tutasimama na vyama vinayotetea wananchi. Katiba inatoa tafsiri ya mali za taifa na zinalindwa vipi.
Sisi tumesema pamoja na IGA, katiba ni ajenda yetu ya pili na tunamuambia Rais ndani ya siku 30 tulizotoa tuone mwelekeo wa katiba mpya ya wananchi, katiba ni mali ya wananchi.
Unapomsikia Rais anasema anamuweka Waziri kwenye wizara fulani halafu anamwambia wewe unakifua na kumuandaa kwa mambo yanayokuja (uchaguzi) unakuwa huoni nia njema. Halafu unamsikia Rais anasema atatoa bilioni 125 kwa polisi kwa ajili ya jukumu hiko, kwani Kazi ya polisi kwenye uchaguzi ni nini?
Nahodha wa Mtumbwi wa Vibwengo!
Shekhe Mselem: Nyuma ya DP world kuna BeberuSijapata kuona watu waongo kama hawa, eti mkataba umeingiwa kati ya nchi na kampuni. Khaa.
Namsikiliza mdudu anavyoongea na kutukana hovyo.
hata ikiwa hivyo, kwani kuna sheria ipi inayoikataza nchi kuingia mkataba na kampuni?
Hivi wana akili sawa hawa?
😂😂😂Nahodha wa Mtumbwi wa Vibwengo!
Mahakimu wa Kenya au Rwanda?Mdudu achukuliwe akajibu wapi mahakama imesema "huu mkataba ni mbovu", hapa sasa kachokoza mahakimu.
Hatari snMagufuli aliitwa mshamba.
Sasa serikali nzima imeitwa ni ya kishamba.
Refa endelea kuchochea Kuni.
Mtaje wewe!Mbona kuna askofu hujamtaja ni nani?