Dkt. Slaa: Niliudhika kwa maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema siyo gaidi? Ataka wananchi wanyamaze Mahakama ifanye kazi yake

Dkt. Slaa: Niliudhika kwa maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema siyo gaidi? Ataka wananchi wanyamaze Mahakama ifanye kazi yake

Ila mzee Slaa amekuja haribu sana huku mbele mbele ... yaani kwa ufupi mzee amezeeka vibaya sana, ee Mungu nisaidie nimalize mwendo salama
Mjadala wetu mzuri wa kujadili vipengele vya mkataba wa Bandari sasa umekuwa mjadala wa kutafuta Mabush lawyers kwenda kumchomoa Mzee.
 
Nne ni Kampuni hiyo kuahidi ujenzi wa msikiti mkubwa mbeya kabla ya KAZI kuanza!!

Bado tu hujasikia harufu ya RUSHWA? Au hujui RUSHWA ni upendeleo, kupata usichostahili, kutokula Kwa JASHO?

Niendelee?!!
Mkuu acha udini kabisa kwani mojawapo ya madharti wanayopewa Ni kusaidia Jamii je kujenga misikiti,kuchimba visima,shule, hospital Ni dhambi? Mbona haya Mambo yapo tangu na tangu hao wamechimba Sana visima vya maji katika Taasisi za Elimu maeneo tofauti tofauti Tanzania sikuwahi kusikia malalamiko,Slaa arejee hii kauli yake kwa Mbowe.
 
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Balozi Dkt. Wilbrod Slaa amekiri kuudhika na maneno kuwa 'Mbowe si gaidi' ambayo hutolewa na baadhi ya wananchi kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Amesema wananchi wanatakiwa kuiachia mahakama ambayo ndio chombo cha haki.

“Katika masuala yaliyoko mahakamani ninaona kwanza kuna sura inatumika, kwenda kule Mahakamani kama sehemu ya siasa kitu ambacho mimi sikubaliani nacho.

“Hivyo sijaenda kwa kuwa ni kitu ambacho sikubaliani nacho, sikubaliani na principal ambayo inatumika, mnaenda kule kisha mnaanza kujipiga picha na mpo kwenye mitandao, hiyo ni siasa, mimi sichezi hizo siasa.

“Mimi nikiamua kumtembelea Mbowe nitaenda nyumbani kwake, sitaki kufanya kitendo cha Mbowe kuwa gerezani kuwa siasa, kama ni kumuombea nitauombea kwa nafsi yangu.

“Niliudhika tangu siku ya kwanza na yale maneno ‘Mbowe si gaidi’, nyie ni nani mpaka kusema Mbowe siyo gaidi?

“Wanatakiwa kuachia chombo cha haki kitoe maamuzi siyo wananchi.

“Lakini sina chuki na Mbowe wala sina uadui, nimeshakutana na Mbowe mara kadhaa airport, tukakumbatiana, tukabadilishana namba japo hakuna aliyempigia mwenzake,” anasema DK SLAA.

Source: MwanaHalisi

Na mimi sitaki kusikia kuwa Slaa siyo mhaini wacha Mahakama ifanye kazi yake
 
Mkuu acha udini kabisa kwani mojawapo ya madharti wanayopewa Ni kusaidia Jamii je kujenga misikiti,kuchimba visima,shule, hospital Ni dhambi? Mbona haya Mambo yapo tangu na tangu hao wamechimba Sana visima vya maji katika Taasisi za Elimu maeneo tofauti tofauti Tanzania sikuwahi kusikia malalamiko,Slaa arejee hii kauli yake kwa Mbowe.
Huyo Jamaa na hoja zake za udini ana chuki tu na Bibie Tausi
 
Back
Top Bottom