Wewe hukuona polisi walivyo andamana kwa niaba yao, au ulikuwa umejificha pangoni?Hivi yale maandamano waliyosema akina Mdude na Mwabakusi kuwa yatafanyika piga ua garagaza hata kwa mtalimbo wa Polisi yaliishia wapi? Na akina Mdudu hao wamepotelea wapi? Tulikuwa tunasubiri akina Mdudu na wake zao waandamane ili sisi tuwe tunapiga vigelegele kila wanamopita wanaandamana lakini cha ajabu hawakuonekana maana walisema piga ua garagaza lazima waandamane na kuwa polisi wasingekuwa na ubavu wa kuwazuia.