DKT. Slaa: Rais kumuelekeza Mwanasiasa lugha ya kutumia siyo sawa, tunaingia kwenye mgogoro mkubwa

DKT. Slaa: Rais kumuelekeza Mwanasiasa lugha ya kutumia siyo sawa, tunaingia kwenye mgogoro mkubwa

Yes, ni sawa na kuwafundisha waseme kile unachopenda tu, kuwa kiongozi wa siasa, tena kwenye mfumo wa vyama vingi lazima mwanasiasa uwe na ngozi ngumu, uvumilie madongo yakizidi nawe yajibu, lakini kuwataka wapinzani waseme kile unachopenda ili wakufurahishe huo ni sawa na udikteta.

Naona amejitahidi kuwapanga anavyotaka wale wa ndani ya chama chake, toa huyu hapa weka pale, toa yule kule leta hapa, muhimu aishie huko huko kwasababu ndio mamlaka yake kama mwenyekiti wao yalipoishia, lakini asijaribu kutoka nje ya hapo kufanya kwa wengine wasio wa chama chake, huo utakuwa ni ubabe.
 
Slaa; Nini tafsiri ya kuongea Kwa staha?

Nani akae btn Mwanasiasa na polisi kama mediator au msuluhishi Ili kutafsiri huyu katukana na yupi hajatukana mkutano ukiendelea?

Slaa; Unawezaje kuwambia watu waache dhambi bila kumsema vibaya shetani?

Slaa; Polisi wetu hawana weledi juu ya Katiba hivyo watazuia mikutano mingi wakisikia tu Jina la AMIRI Jeshi mkuu likitajwa!!!

Slaa; Rais arudi kurekebisha kauli yake, asiwapangie watu nini Cha kuongea sababu mawazo na maoni ya watu ni tofauti kulingana na Utashi.

Hoja muhimu sana, zijadiliwe Kwa makini.
 

Dr. Slaa yupo sawa kabisa lakini ni kwanini hapa katikati wakiti akilamba asali haya hakuyaona?
Umeisha sema alikuwa akilamba asali. Hivi lini mtatambua kuwa wanasiasa huwa hawapigi kelele wakiwa na asali mdomoni. Lini mtakubali kuwa wanasiasa ni wanafiki?
 
Back
Top Bottom