DKT. Slaa: Rais kumuelekeza Mwanasiasa lugha ya kutumia siyo sawa, tunaingia kwenye mgogoro mkubwa

1. Kosoa kwa staha.
2. Chawa wangu watakuvaa.
3.mikutano ya vyama vya siasa ichochee maendeleo.

Hizi kauli tatu zote zilikuwa ni soft threat kwa wapinzani.

Mtu anakwambia hii ni haki yako lakini ifurahie ninavyotaka mimi.
 
Mpinzani ambaye huwa namuelewa ni huyu mzee kiukweli anajua kujenga hoja na kupangua hoja nadhani aliwapika vijana wengi sana wa chadema na tangu aondoke yeye sijaona vijana wapya wenye hoja wakiibuka chadema.
Wameibuka watu kama mdude nyagali
 
Dr. Slaa alikuwa wapi kuyasema hayo wakati ule wa Magufuli alipokuwa akilazimisha kila mwanasiasa amsifie yeye na serikali yake?

Dr Slaa alikuwa wapi wakati ule Ben Saanane akipotezwa kwa sababu ya kuhoji tu PhD ya kimchongo ta Magufuli?

Dr. Slaa alikuwa wapi wakati ule Tundu Lissu akimiminiwa risasi kisa tu kupingana na Magufuli kuhusu Makinikia?

Binafsi namuona Dr. Slaa kama mwanasiasa mnafiki, mjinga na mpumbavu.
 
Dr. Slaa alishachoka na kuchokwa kisiasa. Hana tena platform ya kufanya siasa akaeleweka. Wapinzani hawana tena muda naye, CCM wameshamchoka baada ya kumtumia kama kondom ya kisiasa na wanaharakati wanamuona kama mjinga fulani.


Binafsi nasema bora hata Mrema kuliko Dr. Slaa, japokuwa wote ni wale wale.
 

Nothing wrong with his opinion, nothing wrong with your views regarding my views on his comments as well.
 
Achana na Slaa...kama ni mpumbavu ni mzigo wake.

Tuje kwenye hoja yake, vipi ina mashiko!?
 
Bado tupo mbali sana tena sana kutoka kwenye kitu inaitwa demokrasia!!
 
1. Kosoa kwa staha.
2. Chawa wangu watakuvaa.
3.mikutano ya vyama vya siasa ichochee maendeleo.

Hizi kauli tatu zote zilikuwa ni soft threat kwa wapinzani.

Mtu anakwambia hii ni haki yako lakini ifurahie ninavyotaka mimi.
Mwongozo wa kufanya wanasiasa wote nchi nzima kuwa mbilikimo! Marehemu Mkapa, pamoja na uwezo wake mkubwa, uzoefu mpana na kipaji cha kuongea alipenda sana kusoma hotuba zake kwenye ghafla muhimu. Alijitambua udhaifu wake wa kujiamini sana na hivyo kuweza kutamka kauli zisizopendeza mbele ya umma na kwa hadhi yake kama kiongozi mkuu. Kusema kweli mwanzoni katika urais wake alikuwa akisoma takriban hotuba zake zote. Haipendezi hata kidogo, hasa wakati huu tuapojipambanua kuwa tunataka kurejesha umoja na maelewano kitaifa, kila kauli ya kiongozi kuzua gumzo. Inaelekea wasaidizi wa Rais hawatekelezi wajibu wao ipasavyo.
 
Wapo, lakini usimwamini mwanasiasa yeyote.
Ni kweli na ndio maana huwa inaaminika kwamba kwenye siasa hakuna Adui wa kudumu wala Rafiki wa kudumu !! They dance according to the music !! Na wengi wao japo sio wote wanaamini siasa ni uongo uongo tu !!
 
Hakuongea kitu kabisa. Isitoshe, alitumika sana, tena mara nyingi tu kutoa kauli tata kuhalalisha ukandamizaji na uonevu wa kipindi kile. Alidiriki hata kubeza kupigwa risasi kwa Tundu Lissu kuwaaminisha watu ulikuwa uhalifu wa kawaida tu ambao hutokea kwa kila mtu. Kwa kufahamu uwezo wake mkubwa wa kuona mambo mabaya yasiyofaa kufanyika katika nchi hii yenye historia nzuri kisiasa na kiuongozi, na baada ya kukaa kimya na kufumbia macho ukatili wote uliotendeka kipindi cha nyuma, angalau katika hatua hizi za awali busara ingemuelekeza Dkt. Slaa kupongeza kwanza haya yaliyotokea juzi badala ya kukosoa! Nafasi ya kukosoa na hata kurekebisha bado ipo tu.
 
Slaa ni mlafi na muuaji
 
Kipindi cha magu ulimuona akiongea??
Tujadili HOJA, Tusimpangie muda wa kuongea,

By the way kipindi Cha Magu Wala RUSHWA walitishwa, Alijitahidi kutunza na kusimama raslimali za Nchi, hatukusikia TEMBO wetu wakiuwawa na majangili au wanyama kisafirishwa nje ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…