Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu JF ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua Lissu risasi. Nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.

Note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
Km wameshindwa marekani na EU wamesema wako tayari kusaidia mbona hawataki kupokea hilo pia?
 
Amesema “ni jambo ambalo ni tukio la kawaida”

Kutaka kuuwawa kwa mwanasiasa wa upinzani mchana kweupe na bila uchunguzi, siyo tukio la kawaida!
Tukio lolote linabaki kuwa la kawaida mpk uchunguzi u prove vinginevyo.
 
Hakuna aliewahi kuacha upadre alioapa madhabahuni akawa salama;
aliacha upadre,
akaacha mke,
akaiacha CDM
laana ile inasonga mbele hadi kiyama chake.
 
Balozi Mteule na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa amesema tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida na ameitaka jamii kuliacha Jeshi la Polisi kukamilisha upelelezi na kutoa majibu.

Dkt. Slaa ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Clouds juu ya hali ya kisiasa ya Tanzania na mustakabali wa maisha yake baada ya kuondoka CHADEMA, amesema hafurahishwi na baadhi ya watu kuwataja hadharani watuhumiwa wa tukio hilo kwasababu linaharibu uchunguzi wa polisi.

“Mimi kinachoniudhi ni hii watu kusema hadharani kwamba kuna hiki na hiki tunasuspect (tunahisi) waliofanya ni fulani. Sheria inasema ukihisi nenda polisi katoe taarifa sio unaenda kwenye vyombo vya habari”, amesema Dkt. Slaa.

Amesema hawezi kuzungumzia kwa undani suala la Lissu kupigwa risasi, ikizingatiwa kuwa watu wengi wamepigwa risasi nchini na kazi ya kuwabaini wahalifu waliomshambulia ni ya polisi sio viongozi wa siasa au wananchi.

“Lakini kama binadamu hakuna anayependa binadamu yeyote aumizwe lakini matukio haya ya kuumizwa yametokea nchi hii kwa watu wengi sana. Na mimi sio chombo cha dola kujua kwamba unanyoosha kidole kwa kitu ambacho hatukiamini; mimi ni msomi”, amesema Dkt. Slaa na kuongeza kuwa,

“Ukitoa taarifa za upelelezi unaharibu upelelezi. Mimi niko Canada mauaji yapo kila siku na watu wanapotea, wanapigwa risasi wakiulizwa polisi wanakwambia suala hilo liko kwenye upelelezi tukifikia hatua nzuri tutatoa taarifa”.
Nimerudia kusoma mara kadhaa hii post lakini nashindwa kuona mahali ambapo "Dr. Slaa amemtolea uvivu Tundu Lissu".
Dr. Slaa katoa maoni yake lakini hakuna mahali popote ambapo amefanya kilichoandikwa kwenye kichwa cha hii mada.
 
Baada ya kamanda Barlow aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kuuwawa usiku wa manane.
Asubuhi ya siku iliyofuata walikamatwa watuhumiwa katika maeneo mbali mbali ya TANGANYIKA
ni nani alienda kushtaki polisi?
 
Yeye ile list of shame alikwenda kutoa taarifa Polisi au TAKUKURU? Au anavyokomaa kuwa Lowasa ni fisadi kuna taarifa yoyote aliyoipeleka TAKUKURU?
Consigliere, si list of shame Mh.Tindu A. Lissu alisemema ndiye mhusika mkuu
 
Ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu JF ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua Lissu risasi. Nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.

Note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
Mbona unakua na akili kama za mtoto mdogo, Ulishawai kujiuliza zile CCTV Camera ziliondolewa kwa sababu zipi?
 
Huu uzi bavicha wanatiririka utadhani wana mirembe, dr slaa kasema wazi si lisu tu kapigwa risasi bali na wengne wengi wamepigwa risasi na kuuawa kiaina...so wote hao liachiwe jeshi la polisi (kwa mujibu wa sheria) lifanyie uchunguzi, na ikiwa kuna mtu anao ushahidi zaidi unaoweza kusaidia apeleke dawati la polisi.
 
Yeye mwenyewe alipokuwa katibu wa Chama cha upinzani mke wake alipigwa mapanga na alikaa India kwa kipindi kirefu akitibiwa Polisi walimpa hitimisho la uchunguzi?

Tundu Lissu amepigwa risasi mchana katika makazi ya watumishi waandamizi wa serikali anasema ni tukio la kawaida.

Ukitaka kuwa rafiki wa mbwa koko, anza kwa kumpa makombo....
 
Yeye ile list of shame alikwenda kutoa taarifa Polisi au TAKUKURU? Au anavyokomaa kuwa Lowasa ni fisadi kuna taarifa yoyote aliyoipeleka TAKUKURU?
List of shame iliandaliwa na Tundu Lissu na ikasomwa na Dr. Slaa hadharani baada ya aliyeiandaa (Lissu) kugwaya kuisoma kwa kuogopa kupelekwa kotini.
 
List of shame iliandaliwa na Tundu Lissu na ikasomwa na Dr. Slaa hadharani baada ya aliyeiandaa (Lissu) kugwaya kuisoma kwa kuogopa kupelekwa kotini.
Kwanini Dr. Slaa aliisoma hadharani kwenye vyombo vya habari badala ya kuipeleka Polisi?
Kuna wakati aliyekua Spika wa bunge wa wakati ule Samweli Sitta aliwahi kumshauri Dr. Slaa kuzipeleka Polisi tuhuma fulani alizokuwa nazo badala ya kuzipeleka bungeni, kwanini Dr. Slaa aliukataa ushauri ule wa Spika?
 
Huyu ni msaliti wa Ukatoliki, haaminiki hata kidogo. Achana naye. CCM damu sasa, what else do you expect na ameahidiwa ubalozi, hawezi kulikoroga. Kutoka kuosha vyombo hotelini, leo ni diplomat, hawezi kuuona ubaya wa Lisu kupigwa risasi na huyo anayetuhumiwa.

Dr Slaa ni kati ya wasomi wa kiwango cha juu sana Tanzania Eastern Africa na Africa. PhD - zaidi ya shahada nne! inatambulika duniani. Wewe sijui una shahada ngapi and you dare talk ill of him?.
 
Back
Top Bottom