Dkt. Slaa: Tunapinga uwekezaji wa DP World sababu Mkataba wake una sura ya wizi na ufisadi

Wakuu, naona Watanganyika wameamka.
Nimeogopa kiongozi wa dini ameomba maombi magumu sana.

Amemtaja Samia kama Kiongozi MKAIDI🤣🤣🤣
 
Wanaelewa Kila kitu wanachokifanya. Hii kitu Iko well organized! Na ilikuwa inatekelezwa kwa Siri wananchi wasielewe chochote. Mungu ni mwema kwa taifa lake aliloliumba,akautoa mkataba sirini na kuuweka palipo wazi.
Amen
 
Wakuu, naona Watanganyika wameamka.
Nimeogopa kiongozi wa dini ameomba maombi magumu sana.

Amemtaja Samia kama Kiongozi MKAIDI[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
wachilia mbali mbinguni!. Maombi yale hayanyanyuki japo mita moja kwenda juu

Mwenyezi Mungu hasikilizi dua za wajinga
 
Kuwapiga mkwara wanaotoa maoni yao sio poa.
Kuwapiga mkwara ni ujinga binadamu yoyote ukiwa na tatizo uwezo wako wa kufikiri unaongezeka unapowapiga mkwara watu ndipo wanaamusha ubongo kwakufikiri zaidi. Binadamu ana akili sana lakini binadamu huyohuyo ni mivu wa kufikiri
 
Safi sana,mmeonyesha njia,kazi kwetu wananchi kulinda rasilimali zetu au kuziacha ziende kwenye mikono ya waaarabu
 
Rais wa Akudo sound pengine?
 
Nyinyi endeleeni kuwasikiliza tu wenzenu wanalipwa na makampuni yanayowatuma yanayoelekea kupoteza ulaji bandarini nyinyi mmebaki kukesha mitandaoni kuwasikiliza badala ya kwenda mashambani na kwenye shughuli zitazokuingizieni kipato na familia zenu.
Na wewe endelea kuwasikiliza akina Kitenge na Steve Nyerere. Wenzio washalambishwa..... Nenda shamba I endelea na shughuli zako.
 
hakika wameitendea haki jumatano ya leo, vizazi vitawakumbuka kama sio watu wajinga.

Kwasasa Taifa linahitaki raia wakali na wakorofi ili watawala watimize wajibu wao.
 
Hivi Slaa hakuona Ufirauni aliokuwa anafanya Magufuli na hakusema lolote kama yeye ni mtu wa kusimamia haki kwa nini alinyamaza kimya wakati wa Magufuli na ushenzi wote uliokuwa unafanyika sasa ndio ameamka kutoka usingizini na kuona serikali inafanya ushenzi?? Akinijibu nikielewa na sio kejeli nitamheshimu huyo mzee . Sitaki unafiki
 
Sure.
 
Kuna mambo sio ya kudharau. Mdharau mwiba, mguu huota tende
 
Tunapinga wizi wa mikataba ya aina hiyo kama huo wa bandari na DP world
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…