Dkt. Stephano Reuben Moshi: Askofu Mkuu wa Kwanza KKKT Tanzania

luambo makiadi

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2017
Posts
10,602
Reaction score
8,798
Wakuu nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama mada isemavyo,baba Askofu Dr Moshi ni Mkuu wa Kwanza wa KKKT Tanzania ambapo aliongoza taasisi hiyo ya pili kwa ukubwa(ya Kwanza ni Roman Catholic) kati ya mwaka 1963-1976

Askofu Dr Moshi alifanya Mambo mengi na makubwa kiroho na kijamii ambapo aliheshimika ndani na nje ya nchi

Askofu Dr Stephano Moshi ndiye muanzilishi/muasisi wa hospital ya Kanda ya rufaa ya Kanda ya kaskazini ya KCMC, pia chuo kikuu Cha kumbukumbu ya Stephano Moshi (STEMUCO) Cha mjini Moshi kilipewa jina lake ili kumuenzi

Askofu Dr Moshi alizaliwa mnamo mwaka 1906 katika Kijiji Cha Mamba Kotela kata ya Marangu magharibi na kufariki mwaka 1976.

Nawasilisha.

 
Kumbe ndo huyu Dr!!!??!!!!! Nafurahi kumjua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…