Nabii Sulemani wa kwenye Qurani alitumia majini kumsaidia kazi zake na ipo kwenye Qurani.
Ushahidi ndio huo ndani ya Qurani na Aya ipo.
Ushanifahamu hapo ?
Kama Mwislamu Sulemani aliyatumia basi ni ruksa kwa Mwislamu mwingine kuyatumia pia.
Au hadi nikuwekee Aya ndio uridhike ?,,🤣?
Mpaka umeleta point hii hapa means haujasoma post zangu za nyuma kuna mtu alitumia dalili hiyo hiyo kwamba sulaiman (alayhi salaam) aliyatumia hivyo na sisi tuyatumie 🤨 really?
Nadhani inanibidi nikuelimishe na kuelimisha wengine kadiri nitakavyojaaliwa na Allah (subhana huwataala) ok tuanzie hapa . Kwanza jua kila nabii ana umma wake na zama zake kuna vitu ambavyo umma fulani ulihalalishiwa na kisha umma nyengine ukakatazwa na anayehalalisha na kuharamisha ni Allah(subhana huwataala) pekee kukupa mfano .
Bani israil kipindi cha nabii musa (alayhi salaam) waliharamishiwa wanyama ambao kwato zao hazijapasuka , mafuta ya kondoo na ng'ombe ispokuwa ya kwenye migongo na matumbo, ndege ambao miguu yao haijapasuka mfano bata pia waliharamishiwa vyakula ambavyo mwanzo vilikuwa halali kabisa na vitamu n.k ushahidi ni aya hizi mbili hapa
Al-An'am 6:146
وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ حَرَّمْنَا كُلَّ ذِى ظُفُرٍۖ وَمِنَ ٱلْبَقَرِ وَٱلْغَنَمِ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ شُحُومَهُمَآ إِلَّا مَا حَمَلَتْ ظُهُورُهُمَآ أَوِ ٱلْحَوَايَآ أَوْ مَا ٱخْتَلَطَ بِعَظْمٍۚ ذَٰلِكَ جَزَيْنَٰهُم بِبَغْيِهِمْۖ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Na wale walio fuata dini ya Kiyahudi tumewaharimishia kila mwenye kucha. Na katika ng'ombe na kondoo na mbuzi tumewaharimishia shahamu yao, isipo kuwa ile iliyo beba migongo yao au matumbo yao, au iliyo gandamana na mifupa. Tuliwalipa hivyo kwa sababu ya uasi wao. Na bila ya shaka Sisi ndio wasema kweli.
Na pia waliharamishiwa baadhi ya vyakula vizuri walivyokuwa wanavipenda ushahidi ni aya hii hapa.
An-Nisa' 4:160
فَبِظُلْمٍ مِّنَ ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ طَيِّبَٰتٍ أُحِلَّتْ لَهُمْ وَبِصَدِّهِمْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ كَثِيرًا
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Basi kwa dhulma yao Mayahudi tuliwaharimishia vitu vizuri walivyo halalishiwa. Na kwa sababu ya kuwazuilia kwao watu wengi na Njia ya Mwenyezi Mungu,
lakini kwa mtume muhammad (swalalah alayhi wasalam) Allah (
Subhana huwataala) ametuhalalishia wanyama wote ispokuwa nguruwe , nyamafu , na wanaowinda kwa meno
Na kwenye mazao na matunda hatujaharamishiwa chochote katika hayo na tunakula nyama ya kondoo na mafuta yake tunatumia na tunakula bata, na mbuni na ngamia e.t.c hii ni ne'ema kutoka kwa Allah (subhana huwataala).
Kipindi cha nabii sulayman(alayhi salaam) masanamu yaliruhusiwa kama mapambo na sulaiman(alayhi salaam ) alikuwa mtume lakini kasri lake lilipambwa na masanamu pia ushahidi ni aya hii hapa.
Saba' 34:13
يَعْمَلُونَ لَهُۥ مَا يَشَآءُ مِن مَّحَٰرِيبَ وَتَمَٰثِيلَ وَجِفَانٍ كَٱلْجَوَابِ وَقُدُورٍ رَّاسِيَٰتٍۚ ٱعْمَلُوٓا۟ ءَالَ دَاوُۥدَ شُكْرًاۚ وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِىَ ٱلشَّكُورُ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na masanamu, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yasiyo ondolewa mahala pake. Enyi watu wa Daudi! Fanyeni kazi kwa kushukuru. Ni wachache katika waja wangu wanao shukuru.
Lakini katika umati muhammad (swalalah alayhi wa salaam) masanamu ni kharamu na haifai kuyatengeneza .
Tukirudi kwenye point yako , ni kwamba waislamu huwa hatufuati mawazo yetu kwenye maswala ambayo yana hukmu tayari na kufanya hivyo kutakupelekea kwenye upotevu mfano wewe ulivyo sema hivi
"........Kama Mwislamu Sulemani aliyatumia basi ni ruksa kwa Mwislamu mwingine kuyatumia pia?......"
Hapo umetumia akili yako bila ya kufuata hukumu na inaweza kupelekea kuwapoteza wengi maana waislamu sisi tunamtegema Allah( subhana huwataala ) kwa kila jambo rejea surat fatiha aya ya tano nanukuu.
Al-Fatihah 1:5
إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.
Hiyo aya hapo juu ni dalili tosha kwamba tunatakiwa kumuomba Allah (subhanna huwataala ) pekee na si viumbe alivyoviumba .
Kingine jua kwamba sulaiman (alayhi salaam) alikuwa mtume na alimuomba Allah (subhanna huwataala) aweze kumpatia ufalme ambao hatopata kumpatia yeyote baada yake na Allah( subhanna huwataala) akamjibia dua yake kwa kumpatia ufalme wa dunia na akamfanya khalifa wa binadamu, majini na wanyama na hao wote walimtii yeye KWA RUKHSA YA ALLAH ( the almighty) ushahidi ni aya surat sad aya ya 35-37
Sad 38:35
قَالَ رَبِّ ٱغْفِرْ لِى وَهَبْ لِى مُلْكًا لَّا يَنۢبَغِى لِأَحَدٍ مِّنۢ بَعْدِىٓۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji.
Sad 38:36
فَسَخَّرْنَا لَهُ ٱلرِّيحَ تَجْرِى بِأَمْرِهِۦ رُخَآءً حَيْثُ أَصَابَ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika.
Sad 38:37
وَٱلشَّيَٰطِينَ كُلَّ بَنَّآءٍ وَغَوَّاصٍ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Na tukayafanya mashet'ani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi.
Mwisho wa kunukuu.
Na aya ya 37 inaweka wazi kabisa kwamba yote hayo yaliwezekana kwa amri ya Allah(subhanna huwataala)
Sisi umma huu mtume wetu ni muhammad (swalalah alayi wasaalam) amepewa hukmu tofauti na nyuma zilizopita hivyo basi tunafuatata hukmu za mtume wa mwisho.
Hope nimeondoa sintofahamu na Allah(subhanna huwataaala) ni mjuzi zaidi