Uchaguzi 2020 Dkt. Tulia Ackson achukua fomu ya Ubunge Mbeya Mjini kupitia CCM. Asindikizwa na mumewe

Uchaguzi 2020 Dkt. Tulia Ackson achukua fomu ya Ubunge Mbeya Mjini kupitia CCM. Asindikizwa na mumewe

Naibu Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson amechukua fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM. Akiwa amesindikizwa na mume wake James Andilile Mwainyekule, Dkt. Tulia amefika Ofisi za CCM Wilaya ya Mbeya leo Julai 14 2020 na kuchukua fomu hiyo.

Mbeya mjini Sugu anza kufungasha, hilo jimbo sio lako tena.
Aliyekuwa naibu spika,au bunge hamjalivunja nyie ccm mbunda milia?
 
Sugu ana album alikuwa anaipika ina mistari ya jela alikokaa na bungeni imeshiba na wakati wa kuipakua umewadia anarudi tena kwenye gemu ubunge hatoupata tena mwenyewe kafika! huyu Tulia huwezi kumlinganisha na Sugu na atapata sapoti ya serikali Mbeya mpya itaonekana na kupendeza!!

Sugu ni mhuni, mvuta bangi , msela na mropokaji tu hana hadhi ya kuwa mbunge!!anafaa kuwa kiongozi wa umoja wa bodaboda, huyu goli la mkono ni halali kabisa kwake!!!

hebu msikie anavyojinasibu kuvuta bangi hapa chini!

Lumumba pigeni kelele zenu zote, ila mkumbuke Sugu ndie mbunge alieongoza kwa kupata kura nyingi 2015, huyo dada yenu kama anategemea miujiza mwambieni aende kwa Mwamposa.
 
Naibu Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson amechukua fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM. Akiwa amesindikizwa na mume wake James Andilile Mwainyekule, Dkt. Tulia amefika Ofisi za CCM Wilaya ya Mbeya leo Julai 14 2020 na kuchukua fomu hiyo.

Mbeya mjini Sugu anza kufungasha, hilo jimbo sio lako tena.
Kumbe kana mme hako ka mama ,ok ila kitendo cha yeye kuwania ubunge ni hatari Sana kwa ndugai nasikia jiwe anataka kawe ka spika,sijui ndugai mzee wa bakora atakubali zengwe Kama alilopigwa mh Sitta
 
Usilolijua ni kama usiku wa kiza. Ungemjua huyo jamaa wala usingesema hayo maneno. Ndoa yao iko vizuri sana na wote ni vigogo katika Serikali hii tukufu na pia wote wana mpunga mrefu ni familia ambayo mume na mke wote wako vizuri kiuchumi na kimadaraka

Sasa huko kwenye Ubunge wanaenda kutafuta nini?
 
Mnajitahidi sana kupotosha lakini nikuhakikishie mimi kama mwenyeji na mkazi wa Mbeya Sugu anashinda mchana kweupe, CCM haina wapiga kura huku labda angalau pale Sinde na Ilolo.

Halafu we jamaa una jina zuri ila mambo yako ya kiboya sana, badili ID kwa ajili ya kulinda heshima ya jina
 
Back
Top Bottom