Uchaguzi 2020 Dkt. Tulia Ackson achukua fomu ya Ubunge Mbeya Mjini kupitia CCM. Asindikizwa na mumewe

Uchaguzi 2020 Dkt. Tulia Ackson achukua fomu ya Ubunge Mbeya Mjini kupitia CCM. Asindikizwa na mumewe

Comment za watu wa Sugu wanahasira aisee.minaona uchaguzi huu kama ni vita huwenda ikaanzia Mbeya mjini.
Sijui hawa viumbe kama watalala sikuhiyo japo Dr.Tulia atashinda.
 
Hao waliosoma wamekusaidia nn ww zumbukuku
Sugu hapiti na wala hatumtaki, tumechoka kuongozwa na watu wasio soma, kazi kupigana bungeni. Mbeya maendeleo yamesimama hakuna sababu ya siasa za wana harakati. Mbeya mkitaka maendeleo chagueni CCM, wapinzani mtabaki hivyo hivyo miaka yote miradi yote mtakua mnaisikia na kuona kwenye TV
 
sugu awe makini sana, sifa za mpinzani wake naona zipo wazi wazi
1. Ni MWANAMKE anayejiamini
2. Ni mwanamke MSOMI WA SHERIA
3. Ana UCHUMI wake imara
4. Ni MTOAJI na MCHANGIAJI wa shughuri za maendeleo ukimuhitaji
5. Amewahi shika nafasi kubwa za juu nchini, kama vile kuwa NAIBU SPIKA wa Bunge


Sugu atambue hizi alafu atafute namna bora ya kumzidi kete mwana mama.
Mbeya mkoa wangu mm nipo mbali, yeyeto akija poa tu...nikija salimia wazazi nikute mambo safi huko. Kila laheri nawatakieni
 
Hatimaye Siku Tuliyoisubiri imewadia Mhe. Mbunge Wa Mbeya 2020-2025 Na Naibu Spika Dkt Tulia kachukua fomu ya kugombea Ubunge kilichobakia tunasubiri kuapishwa kwake mjengoni mwezi wa kumi na 11.



View attachment 1506787

HATIMAYE Aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mbunge wa kuteuliwa,Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson ameonesha dhamiri yake yak taka kumn’goa Mbunge aliyemaliza muda wake wa jimbo la Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi alimaarufu “SUGU”.

Alikuwa ni majira ya saa 1.55 alfajiri Mheshimiwa huyo aliposhuka katika gari nambari za usajili T.675 Land Cruiser Prado Tx akiwa ameambatana na Mume wake James Mwanyekule na kuingia katika Ofisi za CCM Wilaya ya Mbeya na kupokelewa na Katibu wa Chama hicho Wilaya,Gervas Ndaki.

Saa 2.08 asubuhi leo Julai,14,2020 amekabidhiwa fomu hiyo baada ya kupata maelekezo na taratibu za chama cha Mapinduzi ambapo kwa sehemu kubwa kwa mara ya kwanza Mume wake Mheshimiwa huyo alitumia fursa hiyo kumpigia chapuo kuwa anayo maono ya Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla hivyo wanambeya waitumie fursa hiyo ya kumtumia.

“Mimi siyo Mwanasiasa lakini siku zote za maisha yetu Mke wangu kipenzi amekuwa na ndoto na maono ya kuwatumikia wanambeya na watanzania wote kwa ujumla,name ninamuunga mkono na sote tumuunge mkono,amesema

Safari ya Tulia kuelekea kuwa Mbunge tena lakini kwa sasa kwa sura ya kupigiwa kura na wapiga kura wake imeanza leo rasmi(Julai,14,2020 majira ya saa 2.08 alfajiri)Mbeya wanahitaji Kiongozi bora na siyo bora Kiongozi.
Duuuh mume ndio anasura ya mke,halafu mke ndio anasura ya kiume[emoji16][emoji16]
 
sugu awe makini sana, sifa za mpinzani wake naona zipo wazi wazi
1. Ni MWANAMKE anayejiamini
2. Ni mwanamke MSOMI WA SHERIA
3. Ana UCHUMI wake imara
4. Ni MTOAJI na MCHANGIAJI wa shughuri za maendeleo ukimuhitaji
5. Amewahi shika nafasi kubwa za juu nchini, kama vile kuwa NAIBU SPIKA wa Bunge


Sugu atambue hizi alafu atafute namna bora ya kumzidi kete mwana mama.
Mbeya mkoa wangu mm nipo mbali, yeyeto akija poa tu...nikija salimia wazazi nikute mambo safi huko. Kila laheri nawatakieni
We ndiyo unaona makubwa hayo

Ova
 
We ndiyo unaona makubwa hayo

Ova
Something is better than nothing!. Jipangeni vizuri ili kumkabili, wekeni hoja vizuri ili wananchi wawaelewe wawapeni kura otherwise ubunge hapo mjini mtausikia tu msimu huu. Usipoteze kunijibu mm mtandaoni, wapiga kura wapo huko mbeya. MM napenda kusikia mbeya inaendelea, kama tulia anapiga kazi njema kuliko aliyekuwepo basi nitawashawishi wampe kura anayewasaidia ili awasaidie zaidi kwa imani (Hakuna mwenye hati miliki na jimbo hilo)
 
Usilolijua ni kama usiku wa kiza. Ungemjua huyo jamaa wala usingesema hayo maneno. Ndoa yao iko vizuri sana na wote ni vigogo katika Serikali hii tukufu na pia wote wana mpunga mrefu ni familia ambayo mume na mke wote wako vizuri kiuchumi na kimadaraka
Wewe ni house maid wao?? Maana unawajua mnooo
 
huyu Mumewe ajiandae na leso za kumfuta machozi mkewe.
Katika ulimwengu wa kiroho dada yangu Betina anapaswa kutambua pamoja na umaarufu alionao,kitendo cha post yake hii kukosa msisimko inadhihirisha namna alivyopwaya...Ili kulinda heshima yake kitaaluma anapaswa tu kuchutama maana huo ndio uungwana kuepusha dhahama ya kuvuliwa nguo
 
Usilolijua ni kama usiku wa kiza. Ungemjua huyo jamaa wala usingesema hayo maneno. Ndoa yao iko vizuri sana na wote ni vigogo katika Serikali hii tukufu na pia wote wana mpunga mrefu ni familia ambayo mume na mke wote wako vizuri kiuchumi na kimadaraka
Mkuu Funza, mumewe amesema yeye si mwanasiasa, kuna cheo gani kikubwa kinapatikana nje ya siasa kwa nchi hii?
 
Huyo amechukua tu fomu, lakini kuna mtu ameshaandaliwa anaitwa Mwakatobe, ndiye atakaye peperusha bendera ya ccm Mbeya Mjini.
Chezea Magu wee.
Shika hayo maneno yangu.
Sawa nimetunza screenshot kwa drive
 
MBEYA TUNAJITEKENYA NA KUCHEKA WENYEWE

Tuliaminishwa Dr Tulia, anastahili kuwa muwakilishi wetu. Tukaaminishwa kuja kwake Mbeya ni matakwa ya Rais.
Kwamba anamtaka Tulia, baadaye awe SPIKA wa bunge.
Tuliaminishwa, elimu na ushawishi wake atachukua jimbo kirahisi. Lugha imegeuka, tunaaminishwa sasa hata kwa nguvu atachukua Dr Tulia.
Kwa hiyo siyo kwa elimu na mvuto wake tena, bali nguvu zetu ndo zitampa Jimbo?
Tumeamua kuwadharau wana Mbeya kiasi hicho?
Kwamba tunawaletea Mbunge wa kuwa Spika?
Kwamba Uspika wake utaleta na kufufua viwanda Mbeya?
Utaleta flyover na maji ya kutosha Mbeya?
Uspika wake utaondoa urasimu kwenye biashara za watu?
Kwamba Uspika wa Ndugai umeleta maendeleo makubwa Kongwa?
Kwamba Kongwa kuna maendeleo kuliko Mbeya?
Kwamba wana Mbeya tutapaa kimaendeleo kama Njombe Kusini ya Anne Makinda?
Tulia atatuletea maendeleo Mengi kama Urambo kwa marehemu Sitta?
Tutapaa kimaendeleo kama jimbo la Ukerewe kwa Mzee Msekwa?
Hiyo ndo njia tuliyochagua kutumia kushawishi wana Mbeya?
Tuache kujitekenya na kucheka wenyewe.
Natazama akili ya watu wachache kwenye vijiwe vya siasa.
Wanaojilisha upepo kuwa Tulia atasaidia kuchukua jimbo.
Kuamini katika Tulia, tutapigwa kipigo cha mapema sana kuliko siku zote.

Ndimi Mwana CCM.
Edwin Mwakanyamale,
Forest Mbeya.
 


Yaani Wanyaki wamemuona Tulia Ackson hafai kuwa Mbunge wao, wakaamua kumchangia fedha za kuchukua fomu ili akagombee Jimbo la Mbeya Mjini. Ni DHARAU ya hali ya JUU kwa WASAFWA.
 
Huyu Mdada alikosa washauri wakati wa maamuzi ya kugombea hasa mikakati ya kampeni hasa zile foundations zake ambazo zilikaa kitakrimatakrima. Zile takrima angezitumia jimbo la Sauli au Kule Busokelo angefukuruka kirahisi sana.

Ila kwasabb kwny siasa kuna mbinu nyingi za ushindi hasa ikitumika mbinu ya Dollar basi hii mbeleko inaweza leta ushindi!! Lakini kwnnn utumie mbeleko wakati mwana mwepesi wa Rungwe magaribi na masharki wapo???

Angefikir sana kabla ya kuamua angenyanyua mzigo mzito kw ngv kidogo sasa.Tusubiri tuone!!!
 
Back
Top Bottom