Dkt. Tulia Ackson alamba kura zote asilimia 100, aapishwa kuwa Spika wa Bunge

Dkt. Tulia Ackson alamba kura zote asilimia 100, aapishwa kuwa Spika wa Bunge

Hongera nyingi sana kwa Dr. Tulia.
Hakika anafaaa sanaaaaa.
yaani...anatoshaaaa hadi chenji inabaki.
 
Hongera sana Dr. Tulia,
Tunakuamini utatuongoza vema
[emoji1241][emoji1241][emoji1241]
 
Hata hivyo vyama vya upinzani hawakuwa serious kwa kuteua watu makini kwa Uspika.
 
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, ameshinda uchaguzi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 376 kati ya 376 zilizopigwa sawa na asilimia 100.

Hii inamaanisha na wabunge 19 wa chama cha CHADEMA waliohudhuria leo kura zao zimo kwenye jumla hiyo.

Spika Tulia Akckson ameapishwa kuwa Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimrithi mtangulizi wake aliyeng'atuka, Job Ndugai.
Duh! hiyo 100 uwa inapatikana tz tu hasa kizazi hiki, nakumbuka hata mwl Nyerere hakuwahi kupata hiyo 100 na haiwezekani watu 376 wakawa na mawazo sawa labda kama wote wameangalizia😂😂😂
 
Kwahiyo kati ya watu 376 waliopo kwenye Bunge letu katika hili la kumchagua speaker wote akili zao zimefanana? Hakuna hata mmojaa mwenye maono ya tofauti? Inafikirisha
 
Unajipiga panga mguuni halafu unashangaa maumivu..

Hili lilikuwa linafahamika toka awali,,, kujifanya tunashangaa haya ya leo wengi ni unafiki tu..

Hongera kwa Tulia,,, naamini sasa familia yake na yeye itaendelea kufaidi mema ya hii nchi yenye maziwa na Asali....

Namsisitiza tu Tulia Akson afuate sana sheria za Meza "Asiongee sana wakati wa kula"
 
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, ameshinda uchaguzi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 376 kati ya 376 zilizopigwa sawa na asilimia 100.

Hii inamaanisha na wabunge 19 wa chama cha CHADEMA waliohudhuria leo kura zao zimo kwenye jumla hiyo.

Spika Tulia Akckson ameapishwa kuwa Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimrithi mtangulizi wake aliyeng'atuka, Job Yustino Ndugai.
Pia hao wabunge wa upinzania waliogombea uspika hawakujipigia wao wenyewe 🤷‍♂️
 
Zaidi ya 50% ya hao wabunge ni bao la mkono na hata hao 19 wanaoitwa wa upinzani ni dhuluma za yule mtu wa ovyo Ndugai, wabunge wa kweli wapo mtaani, miaka yote CCM wanaiba kura ila 2020 CCM ilifanya wizi mkubwa ambao haujawahi kutokea tangu tupate uhuru
 
Jobu maskini hakutegemea kilichotokea mpaka kuukosa uspika wake ambao ulikuwa ushaota mizizi tena kuukosa kwa kiwango hiki, Rais wa nchi inabidi tu aheshimiwe hakuna namna nyengine, mama akiwa nyumban lakini kazini ni mkuu wa majeshi yote.
Dah sijui wanaume wa Tanzania hatima yetu ni nini,tunaongozwa na wanawake?Ni obvious Shetani ameikamata Tanzania.Anataka aimalize Tanzania kama alivyoumaliza humanity Eden.Inaogofya sana.
 
Dah sijui wanaume wa Tanzania hatima yetu ni nini,tunaongozwa na wanawake?Ni obvious Shetani ameikamata Tanzania.Anataka aimalize Tanzania kama alivyoumaliza humanity Eden.Inaogofya sana.
Kwa mujibu wa dini yetu kiongozi mwanake ni shida., lakini ukweli ni kwamba mama ameipoza nchi, watu wamerudi kuwa na amani, wakati ule watu waliishi kwa khofu sana, mateso, vipigo havina sababu, kutekwa, kes za kubambika, wizi hivi hivi, lakini watu hawakuwa huru na mazao yao kama wale wakulima wa korosho., upinzani ulisiginwa mpaka ukutani ata hivi kuandika hapa ilikuwa una hofu sana nk
 
Kwahiyo kati ya watu 376 waliopo kwenye Bunge letu katika hili la kumchagua speaker wote akili zao zimefanana? Hakuna hata mmojaa mwenye maono ya tofauti? Inafikirisha
Hata ndugai alikiluwepo
 
Jobu maskini hakutegemea kilichotokea mpaka kuukosa uspika wake ambao ulikuwa ushaota mizizi tena kuukosa kwa kiwango hiki, Rais wa nchi inabidi tu aheshimiwe hakuna namna nyengine, mama akiwa nyumban lakini kazini ni mkuu wa majeshi yote.
Kosa alifanya ndugai kukaaa kimya karibu wiki nzima badala ya kutoka hadharani kurekebisha kauli yake ikaonekana amedhamilia,,, sasa sijui alikua anapima kina cha maji.... Hiyo ndo imemcost uspika wake,,, atajilaumu hadi siku ya mwisho
 
Jamaa liongo hili. Wagombea kutoka vyama vya TLP, NRA, CCK, ADA-TADEA, SAU ni wambunge?
Hukua na haja ya kunitusi,
Nilikua sifahamu kanuni zao ila nimefahamishwa nikaelewa,
Nikafuta kauli yangu
Sasa unaniita muongo kwani nimeongopea nini?
Nikikwambia muongo mama yako utafurahi?
 
Kwa mujibu wa dini yetu kiongozi mwanake ni shida., lakini ukweli ni kwamba mama ameipoza nchi, watu wamerudi kuwa na amani, wakati ule watu waliishi kwa khofu sana, mateso, vipigo havina sababu, kutekwa, kes za kubambika, wizi hivi hivi, lakini watu hawakuwa huru na mazao yao kama wale wakulima wa korosho., upinzani ulisiginwa mpaka ukutani ata hivi kuandika hapa ilikuwa una hofu sana nk
Mimi kwa Magufuli sikuishi kwa hofu kwa kuwa nilijua mabeberu hawatatuchezea na pia sikuwa na makando kando.Waliokuwa na makando kando ndio walio kuwa na hofu.Sasa nina hofu kwa kuwa najua mabeberu wameikamata nchi na Shetani is in control.Ni baada ya muda tu atadhihirisha makucha yake halisi kwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom