Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa IPU kwa kishindo, apata kura 172 kati ya 303

Hongera zake! Ila nawaza tu, "Rais wa umoja wa mabunge duniani( IPU)", sidhani kama hiki cheo kina mashiko yoyote duniani, kwanini wagombea wawe ni kutoka Afrika tu? Mbona Ulaya, Asia na kwingineko duniani hawakuonesha Nia ya kugombea hiyo nafasi?
 
Kuna wanaume wanamtizama kisha udenda unawatokaaa

Hongera Honorable
 
Kamenimalizia bundle.. ila kako good..
Shida ni Chama chake tu... MASHETANI
Yeah shida ni chama tu Na ubishi wake ila tukienda kitaaluma Kwa maspika wenzie na wabunge wenzie wanaogombea Mwenye sifa nadhani ni yeye.
 
Hongera zake! Ila nawaza tu, "Rais wa umoja wa mabunge duniani( IPU)", sidhani kama hiki cheo kina mashiko yoyote duniani,kwanini wagombea wawe ni kutoka Afrika tu? Mbona Ulaya, Asia na kwingineko duniani hawakuonesha Nia ya kugombea hiyo nafasi?
Ila waliwahi kuchukua nafasi hizo pia kwa muda mrefu
 
Namba ya simu ya nini tena komredi? 😳
 
Hapa ni vema kumpongeza dada kama yeye. Yani kwa umri wake ameendelea kuupiga mwingi. Ni jambo jema kama mwanasiasa wa umri wa kati anaepambana kubadili maisha yake. Bravo!

Lakini, kuhusu taifa,sioni lolote la maana. Kwa mfano, sidhani kama kuwa kwake raisi wa IPU kutasaidia bunge letu kupigania au kuwaadhibu wanaochezea miradi kama wa SGR. Kila kukicha danadana.
 
Somalia


View: https://youtu.be/tLgyVfDlP5o?si=of3U-aBwEmvdK8uB
 
========


Ndugu zangu Watanzania,

Mungu ni mwema, asanteeee sana kwa maombi yenu watanzania wenzangu kwa dada yetu na speaker wetu Dkt. Tulia Ackson.

Habari njema ni kuwa tayari ameibuka kidedea kwa kishindoo kikuu kilichoitetemesha Dunia kwa kupata kura 172 huku anayemfuatia kwa mbali kama kama kichuguu na mlima akiambulia kura 61.huu ni ushindi kwetu sote watanzania tunapaswa kuendelea kuishangilia kwa furaha zote na kujivunia dada yetu aliyetuheshimisha kama Taifa.

Ameonyesha uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kujenga hoja zenye ushawishi na mvuto kwa wapiga kura.kwa hakika Mungu wa Dr Tulia ni mkubwa sana na Anaendelea kuonyesha maajabu na kumtendea makubwa sana Dr Tulia.Mungu anamakusudi maalumu ya kumuumba Dr Tulia,ndio maana mnaona namna ambavyo Anaendelea kupata kibali cha kukubalika,kupendwa,kuungwa mkono na kuchaguliwa kila jina lake linapotua na kuwekwa mezani.

Binafsi nilimuombea sana dada yangu Dr Tulia,usiku na mchana nilifanya kazi ya kumuomba Mungu amsaidie.niliwaomba watanzania wenzangu tuunganishe maombi yetu kwa ajili ya kumuombea speaker wetu ,maana nilijuwa ushindi wa Dr Tulia ni ushindi wetu sote watanzania. Kwa imani nilijuwa ni lazima Dr Tulia Ashinde kwa kishindo na niliandika hata humu jukwaani kuwa Dr Tulia ndiye Rais ajaye wa IPU. Nilisema kwa uwezo wake mkubwa alio nao,Elimu yake,uwezo wa kujenga hoja na kupangua hoja kwa hoja ni vitu na mambo yanayombeba sana Dr Tulia.

Ndugu zangu Watanzania kwa namna Dr Tulia alivyogusa maisha ya wana Mbeya na nyanda za juu kusini nilikuwa naona kabisa ni lazima Mungu awe na Dr Tulia. maandiko kutoka katika biblia yanasema kuwa agusaye na kuwasaida maskini amemkopesha Mungu na kwamba atamlipa kwa mema na mazuri. Dr Tulia amesaidia watu wengi sana waliokuwa katika hali ya umaskini,amesaidia vijana,yatima,wazee ,wajane na watu wegi wenye uhitaji kwa kuwapa misaada ya kila aina na hatimaye kuwafanya kupata matumaini kutoka katika hali ya kukata Tamaa,imeinua matumaini ya wengi na kugusa mioyo ya wengi iliyokuwa imekata Tamaa.
 


Mimi sikutaka ashinde kwasababu ya wizi wa kura na ubunge wake fake. Lakini ameshinda na ingependeza kama wangemchukuwa kabisa astaafu ubunge aende huko kutuwakilisha.Hongera zake ingawa washindani wake hawaeleweki vizuri


View: https://youtu.be/tLgyVfDlP5o?si=of3U-aBwEmvdK8uB
 
Hongera Kwake

Hata Mbowe ni Makamu wa Rais wa Dunia huko Siasani

Kawaida sana 😂😂🔥🌟
Acha kumfananisha Dr Tulia na wababaishaji. Dr Tulia ni namba nyingine ile.ni mwamba kwelikweli.leo nadhani umeona namna alivyoitetemesha Dunia.umeona namna kila mtu akitamani kupiga picha ya kumbukumbu katika maisha yake .Dr Tulia ni mpango wa Mungu mwenyewe.
 
Kalinichefua tu kwenye IGA otherwise kalikuwa kanajitutumua
 
Kalinichefua tu kwenye IGA otherwise kalikuwa kanajitutu
 
Kama kuna mtu hakuona ushindi wa Tulia beforehand huyo mtu ni zwazwa 🤣 Tulia ni best speaker ever kutoka kwenye hii nchi.
 
Hongera Kwake

Hata Mbowe ni Makamu wa Rais wa Dunia huko Siasani

Kawaida sana 😂😂🔥🌟
Dr Tulia ni moto wa kuotea mbali,ni mpango wa Mungu mwenyewe,ni mtu aliye na kibali cha Mwenyezi Mungu mkononi mwake ndio maana unaona namna ambavyo amekuwa akipata ushindi kila jina lake liwekwapo mezani.
 
Kama kuna mtu hakuona ushindi wa Tulia beforehand huyo mtu ni zwazwa 🤣 Tulia ni best speaker ever kutoka kwenye hii nchi.
Niwaambia sana humu jukwaani kuwa Dr Tulia ndiye Rais ajaye wa IPU,niliwambia kuwa Dr Tulia anaungwa mkono kutoka katika kila kona ya Dunia.uwezo wa Dr Tulia ni mkubwa sana na wa maajabu.ni nyota Ing'aayo na kuangaza kila mahali.
 
Msomali


View: https://youtu.be/tLgyVfDlP5o?si=of3U-aBwEmvdK8uB


Tulia


View: https://youtu.be/IbmFSyFUi6g?si=PlrAf6Q7n2nJmBn8
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…