Mimi.
JF-Expert Member
- Sep 7, 2011
- 2,120
- 3,059
Masele alikuwa anafaa sana hii nafasi
Masele Hajui fitina wala kuroga ndio kilichomcost ,🤣🤣🤣
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Masele alikuwa anafaa sana hii nafasi
serikali haiendeshwi kwa kugeukana hayo mambo yapo chadema ndiyo maana hawasongi mbele wao kila siku dili tu mara wauze chama kwa lowassa makengeza ni mtu wa dili nakuwageuka wenziesana siyo ka ccm
Kabebwa na gender Mwenyekiti asingemtupa,Ila ni bora kuliko Chenge.
Ni vyema ungeangalia nchi nzima kuwa imepata badala ya kuzungumzia Chadema maana huyu sasa ni kiongozi wa kitaifa.Safi sanaaaa anafaa chadema watakomaaa
tunawatumikia wananchi hao chadema tuwakomoe ni kinanai kwanza wanashida gani?
Wanawake mwaka wao huu wakishindwa tena basi.Soon kaji mkuu atakua mwanamke...
Natoka mkoa ambao mwanaume ana mamlaka, najisikia vibaya sana...
Kwenye mafanikio na usawa! Jpm alikosea sana kuteiq hawa wanawake. Ndio udhaifu aliotuachiaSafari ya kwenda wapi?
Je CCM iliwahi kufanya chaguo lisilo sahihi kwako?Maamuzi mazuri sana yamefanywa na CCM.
Dr. Tulia ni Chaguo sahihi kabisa.
We haya weeeKwenye mafanikio na usawa! Jpm alikosea sana kuteiq hawa wanawake. Ndio udhaifu aliotuachia
That’s real dumbSafi sanaaaa anafaa chadema watakomaaa
mimi ni mkuryaWanawake mwaka wao huu wakishindwa tena basi.
KILA kitabu na zama zao awamu iliyopita kama wewe ni wa kanda na kabila pendwa au ni chawa kama ulikosa teuzi sahau bahati haiji mara mbili.
Mama anatuvusha.
Akiongea na wanahabari, msemaji wa Chama cha Mapinduzi, Shaka Hamdu Shaka amesema chama kimeptisha Tulia Acksoni kuwa mgombea wa kiti cha uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia soma: Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
PERSONAL DETAILS
Surnname: Mwansasu
Middle Name: Ackson
First Name: Tulia
Salutation: Hon. Dr
Marital Status: Married
Date of Birth: 23 Dec. 1976
Place of Birth: Tukuyu Mbeya.
Sex: F
Email: tuliaj@gmail.com
Postal Address: 35093 Dar es Salaam
EDUCATION BACKGROUND
1984 - 1990 Mabonde Primary School Primary Education
1991 - 1994 Lolera Secondary School CSE
1995 - 1997 Zanaki Secondary School ACSE
1998 - 2001 University of Dar es Salaam LLB
2001 - 2003 University of Dar es Salaam LLM
2005 - 2007 University of Cape Town Ph. D
EMPLOYMENT EXPERIENCE
2011 - 2015 University of Dar es Salaam Senior Lecturer
2009 - 2015 University of Dar es Salaam Associate Dean
2001 - 2001 Attorney General's Office Trainee
HOBBIES
Reading Books
Physical Exercises
View attachment 2089489
Kitinda Mimba Tulia Ackson, amezaliwa 23 Novema 1976 Katika Kijiji cha Bulyaga, Kata ya Tukuyu, wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwenye familia ya Akson Mwansasu akiwa ni mtoto wa 11
Alianza safari yake ya Masomo katika Shule ya Msingi Mabonde, Tukuyu, Rungwe mkoani Mbeya.
Elimu ya sekondari alisoma katika Shule ya Wasichana ya Loleza iliyoko jijini Mbeya, barabara ya kwenda Mtaa wa Ghana alikohitimu kidato cha nne.
Alijiunga na Shule ya Wasichana ya Zanaki ambako alimalizia masomo yake ya kidato cha sita mwaka 1997.
Mwaka 1998 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kitivo cha sheria na kufanikiwa kuhitimu chuoni hapo. Alitunukiwa shahada ya sheria mwaka 2001.
Mwaka huohuo wa 2001, Chuo hicho Kikuu cha Dar es Salaam kilimtaka kubaki chuoni hapo kwa ajili ya kufundisha sheria, hivyo alifundisha huku akiendelea kusaka shahada ya uzamili.
Akiwa bado anafundisha chuoni hapo, mwaka 2003 alimaliza masomo kabla ya kufanya mtihani wa uwakili wa kujitegemea mwaka 2004. Mwaka 2005 alijiunga na Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini kufanya shahada ya uzamivu na kufanikiwa baada ya miaka miwili.
Mwaka 2008 alikwenda chuo cha Max Planck Institute for International and Social Law cha Munich, nchini Ujerumani alikokuwa akifanya ‘post doctoral research’.
Mwaka 2009 alirudi nchini katika ajira yake ya awali ya ualimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na aliteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Shule Kuu ya Sheria, nafasi ambayo alikuwa nayo mpaka mwaka 2014.
Kutoka wajumbe wa elimu ya juu, Dk. Tulia alikuwa miongoni mwa wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete wa Awamu ya Nne katika Bunge la Katiba lililofanyika kwa awamu mbili.
Awamu ya kwanza lilifanyika kuanzia Februari 18, 2014 hadi Aprili 25, 2014. Kwa siku 21 za kwanza alikuwa miongoni mwa wajumbe waliotunga kanuni za Bunge hilo lililoongozwa na Mwenyekiti Samwel Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan.
Mwaka huohuo wa 2014 aliteuliwa na Chuo Kikuu cha Bayreuth cha nchini Ujerumani ili kufanya utafiti kuhusu hifadhi za jamii, utafiti uliojulikana kama Awarded the Alexander Von Humboldt Research Fellowship.
Hata hivyo, utafiti huo aliufanya kwa kipindi cha miezi sita tu, kwani akiwa katika mapumziko, ndipo alipoteuliwa tena na Kikwete kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Septemba 9, 2014
Amekuwa naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kipindi cha miezi miwili tu kutokana na Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli, kutengua uteuzi huo na kumteua kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, akiwa ni mbunge wa kwanza kati ya nafasi 10 za wabunge aliopewa Rais kwa mujibu wa sheria.
Kati ya kazi nzito alizofanya akiwa Mwanasheria Mkuu ni kuongoza jopo la mawakili wa Serikali katika kesi maarufu kwa jina la mita 200, kwani kulitokea mvutano baina ya vyama vya upinzani na Serikali katika kutafsiri sheria ya umbali wa wananchi kukaa mara baada ya kupiga kura.
Mahakama Kuu ilitafsiri sheria hiyo kwa kuagiza wapiga kura kukaa mbali kwa zaidi ya mita hizo baada ya kuridhishwa na hoja za upande wa Serikali ambako Dk. Tulia alikuwa kinara kwa kutaka korti iamue hivyo.
Alhamisi Novemba 19, 2015 wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipiga kura ya kumchagua Tulia kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo. Uchaguzi huo ulifanyika mapema asubuhi ndani ya Ukumbi wa Bunge. Katika uchaguzi huo, Dk. Tulia (CCM) alipata kura 250 kati ya 351 za wabunge wote, huku mpinzani wake, Magdalena Sakaya (CUF) akipata kura 101.
Dk. Tulia ambaye ameolewa na James Andilile na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume
2020 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini
Haikuwa Rahisi kwake kupita japo sina huwakika kama mafuta na maji huchangamana ila Mungu atabaki kuwa Mungu. Na anayo safari ngumu wala sio rahisi mwenye akili na maono atanielewa.

Ulichelewa wapi sasaMi
mimi ni mkurya
Ameiba nini Msukusu huyu?CCM hoyeeee asante kulipiga chini fisadi na jizi Andrew Chenge