Dkt. Tulia Ackson ateuliwa na CCM kugombea Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Akiongea na wanahabari, msemaji wa Chama cha Mapinduzi, Shaka Hamdu Shaka amesema chama kimeptisha Tulia Acksoni kuwa mgombea wa kiti cha uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia soma: Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

PERSONAL DETAILS
Surnname:
Mwansasu
Middle Name: Ackson
First Name: Tulia
Salutation: Hon. Dr
Marital Status: Married
Date of Birth: 23 Dec. 1976
Place of Birth: Tukuyu Mbeya.
Sex: F
Email: tuliaj@gmail.com
Postal Address: 35093 Dar es Salaam

EDUCATION BACKGROUND
1984 - 1990 Mabonde Primary School Primary Education
1991 - 1994 Lolera Secondary School CSE
1995 - 1997 Zanaki Secondary School ACSE
1998 - 2001 University of Dar es Salaam LLB
2001 - 2003 University of Dar es Salaam LLM
2005 - 2007 University of Cape Town Ph. D

EMPLOYMENT EXPERIENCE
2011 - 2015 University of Dar es Salaam Senior Lecturer
2009 - 2015 University of Dar es Salaam Associate Dean
2001 - 2001 Attorney General's Office Trainee

HOBBIES
Reading Books
Physical Exercises

View attachment 2089489
Kitinda Mimba Tulia Ackson, amezaliwa 23 Novema 1976 Katika Kijiji cha Bulyaga, Kata ya Tukuyu, wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwenye familia ya Akson Mwansasu akiwa ni mtoto wa 11

Alianza safari yake ya Masomo katika Shule ya Msingi Mabonde, Tukuyu, Rungwe mkoani Mbeya.

Elimu ya sekondari alisoma katika Shule ya Wasichana ya Loleza iliyoko jijini Mbeya, barabara ya kwenda Mtaa wa Ghana alikohitimu kidato cha nne.

Alijiunga na Shule ya Wasichana ya Zanaki ambako alimalizia masomo yake ya kidato cha sita mwaka 1997.

Mwaka 1998 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kitivo cha sheria na kufanikiwa kuhitimu chuoni hapo. Alitunukiwa shahada ya sheria mwaka 2001.

Mwaka huohuo wa 2001, Chuo hicho Kikuu cha Dar es Salaam kilimtaka kubaki chuoni hapo kwa ajili ya kufundisha sheria, hivyo alifundisha huku akiendelea kusaka shahada ya uzamili.

Akiwa bado anafundisha chuoni hapo, mwaka 2003 alimaliza masomo kabla ya kufanya mtihani wa uwakili wa kujitegemea mwaka 2004. Mwaka 2005 alijiunga na Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini kufanya shahada ya uzamivu na kufanikiwa baada ya miaka miwili.

Mwaka 2008 alikwenda chuo cha Max Planck Institute for International and Social Law cha Munich, nchini Ujerumani alikokuwa akifanya ‘post doctoral research’.

Mwaka 2009 alirudi nchini katika ajira yake ya awali ya ualimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na aliteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Shule Kuu ya Sheria, nafasi ambayo alikuwa nayo mpaka mwaka 2014.

Kutoka wajumbe wa elimu ya juu, Dk. Tulia alikuwa miongoni mwa wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete wa Awamu ya Nne katika Bunge la Katiba lililofanyika kwa awamu mbili.

Awamu ya kwanza lilifanyika kuanzia Februari 18, 2014 hadi Aprili 25, 2014. Kwa siku 21 za kwanza alikuwa miongoni mwa wajumbe waliotunga kanuni za Bunge hilo lililoongozwa na Mwenyekiti Samwel Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan.

Mwaka huohuo wa 2014 aliteuliwa na Chuo Kikuu cha Bayreuth cha nchini Ujerumani ili kufanya utafiti kuhusu hifadhi za jamii, utafiti uliojulikana kama Awarded the Alexander Von Humboldt Research Fellowship.

Hata hivyo, utafiti huo aliufanya kwa kipindi cha miezi sita tu, kwani akiwa katika mapumziko, ndipo alipoteuliwa tena na Kikwete kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Septemba 9, 2014

Amekuwa naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kipindi cha miezi miwili tu kutokana na Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli, kutengua uteuzi huo na kumteua kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, akiwa ni mbunge wa kwanza kati ya nafasi 10 za wabunge aliopewa Rais kwa mujibu wa sheria.

Kati ya kazi nzito alizofanya akiwa Mwanasheria Mkuu ni kuongoza jopo la mawakili wa Serikali katika kesi maarufu kwa jina la mita 200, kwani kulitokea mvutano baina ya vyama vya upinzani na Serikali katika kutafsiri sheria ya umbali wa wananchi kukaa mara baada ya kupiga kura.

Mahakama Kuu ilitafsiri sheria hiyo kwa kuagiza wapiga kura kukaa mbali kwa zaidi ya mita hizo baada ya kuridhishwa na hoja za upande wa Serikali ambako Dk. Tulia alikuwa kinara kwa kutaka korti iamue hivyo.

Alhamisi Novemba 19, 2015 wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipiga kura ya kumchagua Tulia kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo. Uchaguzi huo ulifanyika mapema asubuhi ndani ya Ukumbi wa Bunge. Katika uchaguzi huo, Dk. Tulia (CCM) alipata kura 250 kati ya 351 za wabunge wote, huku mpinzani wake, Magdalena Sakaya (CUF) akipata kura 101.

Dk. Tulia ambaye ameolewa na James Andilile na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume

2020 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini
Ccm ilishakufa kimebaki kikundi fulani cha watu wanalinda maslai yao tu # tunataka katiba mpya #
 
Soon jaji mkuu atakua mwanamke...
Natoka mkoa ambao mwanaume ana mamlaka, najisikia vibaya sana...
Jpm alichemka sana kuteia hawa wanawake

Usiogope
Hakuna anayeweza chukua nafasi ya mwanaume

Kama huamini kamuulize mume wa Tulia
 
Dr. Msomi Tulia Ackson ameteuliwa na CCM kugombea Uspika wa Bunge.

Kinachosubiriwa na kupigiwa kura tu na wabunge wa CCM.

Ukubali ama ukatae Tulia ndie spika mpya wa JMT.

Kazi Iendelee.

This country is doomed to fail.
Upuuzi
 
2001 - 2003 University of Dar es Salaam LLM
2005 - 2007 University of Cape Town Ph. D
Asante mleta mada kwa taarifa hii muhimu. Pia nauliza toka 2003 Mpaka 2005 , Mheshimiwa Dr Tulia alikuwa anajishughulisha na nini?

Na Je. Ni kweli PhD aliisoma miaka 2 ama 3 ?
 
Mkuu, huko CCM huwa mnatumia vigezo gani kumtambua kada kama “mwizi” na “fisadi” au “mtu safi”? Sijawahi kusikia maamuzi rasmi ya kumng’oa fisadi toka kwenye chama. Au ni siri za ndani?
Huwa tunamalizana nao kimya kimya kama tulivyomalizana na Lowasa chadema mkamchukua tukamalizana naye sanduku la kura na Chenge mchukueni awe mgombea wenu uraisi si anazo pesa za kuwahonga kununua chadema kama Lowasa alivyokinunua ? Mchukueni
 
Nashangaa watu wanaumia Tulia kuteuliwa. Hata angeteuliwa nani haitasiadia chochote kwa sababu wote ni CCM. CCM ni ukoo mmoja hata aje nani hakuna la maana atakalobadilisha.

Labda angekuja mtu ambae yuko nje ya mfumo, na tatizo atapenya kupitia mlango gani na wakati bungeni majority ni CCM. Lazima wapitishe mtu wao.

CCM hawana cha kupoteza zaidi ya maslahi yao. Hivyo she nani hawana shida.
 
Asante mleta mada kwa taarifa hii muhimu. Pia nauliza toka 2003 Mpaka 2005 , Mheshimiwa Dr Tulia alikuwa anajishughulisha na nini?

Na Je. Ni kweli PhD aliisoma miaka 2 ama 3 ?

Mbona imeandikwa alipomaliza 2003 alibaki chuon kama Mkufunzi(nadhan mkufunzi msaididiz)
 
Akiongea na wanahabari, msemaji wa Chama cha Mapinduzi, Shaka Hamdu Shaka amesema chama kimeptisha Tulia Acksoni kuwa mgombea wa kiti cha uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia soma: Spika Job Ndugai, amejiuzulu Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

PERSONAL DETAILS
Surnname:
Mwansasu
Middle Name: Ackson
First Name: Tulia
Salutation: Hon. Dr
Marital Status: Married
Date of Birth: 23 Dec. 1976
Place of Birth: Tukuyu Mbeya.
Sex: F
Email: tuliaj@gmail.com
Postal Address: 35093 Dar es Salaam

EDUCATION BACKGROUND
1984 - 1990 Mabonde Primary School Primary Education
1991 - 1994 Lolera Secondary School CSE
1995 - 1997 Zanaki Secondary School ACSE
1998 - 2001 University of Dar es Salaam LLB
2001 - 2003 University of Dar es Salaam LLM
2005 - 2007 University of Cape Town Ph. D

EMPLOYMENT EXPERIENCE
2011 - 2015 University of Dar es Salaam Senior Lecturer
2009 - 2015 University of Dar es Salaam Associate Dean
2001 - 2001 Attorney General's Office Trainee

HOBBIES
Reading Books
Physical Exercises

View attachment 2089489
Kitinda Mimba Tulia Ackson, amezaliwa 23 Novema 1976 Katika Kijiji cha Bulyaga, Kata ya Tukuyu, wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwenye familia ya Akson Mwansasu akiwa ni mtoto wa 11

Alianza safari yake ya Masomo katika Shule ya Msingi Mabonde, Tukuyu, Rungwe mkoani Mbeya.

Elimu ya sekondari alisoma katika Shule ya Wasichana ya Loleza iliyoko jijini Mbeya, barabara ya kwenda Mtaa wa Ghana alikohitimu kidato cha nne.

Alijiunga na Shule ya Wasichana ya Zanaki ambako alimalizia masomo yake ya kidato cha sita mwaka 1997.

Mwaka 1998 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kitivo cha sheria na kufanikiwa kuhitimu chuoni hapo. Alitunukiwa shahada ya sheria mwaka 2001.

Mwaka huohuo wa 2001, Chuo hicho Kikuu cha Dar es Salaam kilimtaka kubaki chuoni hapo kwa ajili ya kufundisha sheria, hivyo alifundisha huku akiendelea kusaka shahada ya uzamili.

Akiwa bado anafundisha chuoni hapo, mwaka 2003 alimaliza masomo kabla ya kufanya mtihani wa uwakili wa kujitegemea mwaka 2004. Mwaka 2005 alijiunga na Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini kufanya shahada ya uzamivu na kufanikiwa baada ya miaka miwili.

Mwaka 2008 alikwenda chuo cha Max Planck Institute for International and Social Law cha Munich, nchini Ujerumani alikokuwa akifanya ‘post doctoral research’.

Mwaka 2009 alirudi nchini katika ajira yake ya awali ya ualimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na aliteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Shule Kuu ya Sheria, nafasi ambayo alikuwa nayo mpaka mwaka 2014.

Kutoka wajumbe wa elimu ya juu, Dk. Tulia alikuwa miongoni mwa wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete wa Awamu ya Nne katika Bunge la Katiba lililofanyika kwa awamu mbili.

Awamu ya kwanza lilifanyika kuanzia Februari 18, 2014 hadi Aprili 25, 2014. Kwa siku 21 za kwanza alikuwa miongoni mwa wajumbe waliotunga kanuni za Bunge hilo lililoongozwa na Mwenyekiti Samwel Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan.

Mwaka huohuo wa 2014 aliteuliwa na Chuo Kikuu cha Bayreuth cha nchini Ujerumani ili kufanya utafiti kuhusu hifadhi za jamii, utafiti uliojulikana kama Awarded the Alexander Von Humboldt Research Fellowship.

Hata hivyo, utafiti huo aliufanya kwa kipindi cha miezi sita tu, kwani akiwa katika mapumziko, ndipo alipoteuliwa tena na Kikwete kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Septemba 9, 2014

Amekuwa naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kipindi cha miezi miwili tu kutokana na Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli, kutengua uteuzi huo na kumteua kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, akiwa ni mbunge wa kwanza kati ya nafasi 10 za wabunge aliopewa Rais kwa mujibu wa sheria.

Kati ya kazi nzito alizofanya akiwa Mwanasheria Mkuu ni kuongoza jopo la mawakili wa Serikali katika kesi maarufu kwa jina la mita 200, kwani kulitokea mvutano baina ya vyama vya upinzani na Serikali katika kutafsiri sheria ya umbali wa wananchi kukaa mara baada ya kupiga kura.

Mahakama Kuu ilitafsiri sheria hiyo kwa kuagiza wapiga kura kukaa mbali kwa zaidi ya mita hizo baada ya kuridhishwa na hoja za upande wa Serikali ambako Dk. Tulia alikuwa kinara kwa kutaka korti iamue hivyo.

Alhamisi Novemba 19, 2015 wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipiga kura ya kumchagua Tulia kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo. Uchaguzi huo ulifanyika mapema asubuhi ndani ya Ukumbi wa Bunge. Katika uchaguzi huo, Dk. Tulia (CCM) alipata kura 250 kati ya 351 za wabunge wote, huku mpinzani wake, Magdalena Sakaya (CUF) akipata kura 101.

Dk. Tulia ambaye ameolewa na James Andilile na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume

2020 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini
Safi Sana , huwezi pitisha fisadi kama Chenge na wale wengine wasio na uzoefu.

Naibu awe Zungu au Masele
 
Ilikuwa suala la muda tu.imetuchukua muda mrefu Sana Wana Mbeya kutoa kiongozi mkuu miongoni mwa mihimili mikuu mitatu.niliongea humu kwamba ni zamu yetu Wana Mbeya
 
CCM niileile kazi inaendelea ya awamu ya 5 katika muhimili wa Bunge
 
CCM hoyeeee asante kulipiga chini fisadi na jizi Andrew Chenge
Kuna watu ni mapumbavu kweli,hivi kwa akili ya kawaida hivi unaweza kumfanya Chenge awe Spika? Ungekuwa ni utani na matusi kwa wananchi.

Mama alivyopata ngekewa ya Urais ndivyo Tulia kapata ngekewa ya USpika.

Ana uzoefu kama Naibu na Makinda alikuwa Naibu akawa Spika.
 
Ilikuwa suala la muda tu.imetuchukua muda mrefu Sana Wana Mbeya kutoa kiongozi mkuu miongoni mwa mihimili mikuu mitatu.niliongea humu kwamba ni zamu yetu Wana Mbeya
Afadhari hata maana wametutenga Sana mkuu.

Na spika lazima apite bilakupingwa kwenye Jimbo lake,Akina Sugu tutawaachia Jimbo jipya 😅😅
 
Back
Top Bottom