Dkt. Tulia suala la bandari hata wazee huzeeka na upumbavu wao

Dkt. Tulia suala la bandari hata wazee huzeeka na upumbavu wao

Mwanzo wa mkataba ni lini,mwisho ni lini,maslahi ya Taifa ni yapi,ya mwekezaji ni yapi?lini tutafanya mapitio kuona hali ya wakati huo kama tunahitaji kubadili baadhi ya mambo?

Wewe na Prof. Shivji, Jaji Warioba nani anafahamu sheria kuliko mwingine na kuwa na uzoefu wa kuzitumia unaompa muda mrefu wa kutafsiri?

Kwanini bandari za Zanzibar hazipo ndani ya huo mkataba wakati bandari ni suala la Muungano?
 
Dr. Tulia Kama umo humu nisome na ujitafakari Sana na pia uuchunge ulimi wako usijizime data! Yaani Prof. Shivji mwalimu wako tangu mwaka wako wa kwanza Hadi uprofesa awe mpumbavu kweli?

Hebu kuwa serious dada yetu. Wazee wetu hata waweje bado hawastahili kuitwa wapumbavu! Na hapa umetutusi wote ambao ni uzao wa hao wazee wetu kuwa nasi ni wapumbavu!

Hapana kwa kweli, jishushe na uwaombe watanzania radhi kwa kauli yako hii kwani uwepo wa werefu hunasibishwa na uwepo wa wapumbavu na hakuna werefu bila uwepo wa wapumbavu!

Nikuulize, umetumia instrument gani kuwapima hao wazee na kupata jawabu Hilo? Utapoteza hiyo nafasi unayoiringia mapema Sana 2025 na wakishupaza shingo hao wazee huenda wakakung'oa kwenye kiti hicho kabla ya muda wako kuisha!
 
SPIKA wa Bunge, Tulia Akson amewajia juu watanzania waosema bandari imeuzwa na kubainisha kuwa Mtu mpumbavu anazeeka na upumbavu wake...
Wanafunzi anaotamba kuwafundisha chuo kikuu ndo kina Mwijaku?
 
SPIKA wa Bunge, Tulia Akson amewajia juu watanzania waosema bandari imeuzwa na kubainisha kuwa Mtu mpumbavu anazeeka na upumbavu wake...
Mh Spika hapa ametumia maneno makali kidogo. Neno upumbavu huwa ni neno kali mno, japo hata sisi wengine huwa tunalitumia.

Aende nao taratibu mwishowe watamwelewa tu.
 
Mwanzo wa mkataba ni lini,mwisho ni lini,maslahi ya Taifa ni yapi,ya mwekezaji ni yapi?lini tutafanya mapitio kuona hali ya wakati huo kama tunahitaji kubadili baadhi ya mambo?Wewe na Prof.Shivji,...
Bandari za Zanzibar hazimo kwa sababu tayari wamepewa makaburu
 
SPIKA wa Bunge, Tulia Akson amewajia juu watanzania waosema bandari imeuzwa na kubainisha kuwa Mtu mpumbavu anazeeka na upumbavu wake...
Nchi inaweza kuwa ipo katika hali salama kwa kuwa hata na wajinga milioni 1 kuliko kuwa na watu wanafiki, waongo na waabudu matumbo yao 10 w asa kiwango cha mtu kama Tulia.
 
Mh. Tulia ni kama amekerwa na namna wakili mwabukusi alivyo ongea na wazee wa Mbeya Siku mbili zilizopita, akiwa Mbeya na kile kinacho one kana kukerwa na uchambuzi wa wakili mwabukusi, alihujikuta akiongelea mkataba wa Bandari huku akiwaponda aliowaita wapotoshaji wa mkataba huo kuwa ni wapumbavu na hawawezi elimika, ingawa hakujibu hoja hata moja Bali walionyesha majigambo ya Elimu yake na uzoefu alionao ktk sharia.

Nawashauri tu wasomi wetu, na vijana wanaosoma kuwa wasisome ili kupata sifa na kuheshimiwa... Bali wa some ili elimu yao isaidie kutatua changamoto za maisha. Kusoma na kujigamba wakati huna uwezo wa kutumia elimu yako kuzuia au kutatua changamoto ni upumbavu kama upumbavu mwingine tu.

 
Back
Top Bottom