Dkt. Tulia suala la bandari hata wazee huzeeka na upumbavu wao

Kama hilo darasa la sheria na hizo tafiti alisoma na kufanya mwenyewe kati ya watu wote naweza kumuelewa.
Ila asitutishie usomi wake ambao tija yake katika taifa na hata taasisi anayoiongoza mekua ni ndogo sana.
 
Mimi nimesoma Rungwe Alliance Secondary School mwaka 1965-1968. Ni mzee ambaye bila shaka Tulia ataniita "mpumbavu". Nina marafiki wengi sana wa Mkoa wa Mbeya wa zamani. Mimi sitoki mkoa huo. Nilikutana Kisungu, Mwakaleli,Kambasegela na wazee ambao hawana PHD lakini wakizungumza walikuwa na hekima kuliko Tulia. PHD ni njia moja tu ya kuelimika kama hukuwa kasuku au bado hujasahau ulichosoma. Kuna njia nyingi nyingine za mtu kuelimika. Alama ya PHD haikupi elimu, ni cheti cha ufaulu tu wa jambo moja finyu sana. Kwa kifupi kabisa Waingereza huita ugonjwa wa Tulia wa kutotofautisha kiwango cha ufaulu kwenye cheti cha shahada na kiwango cha kuelimika, "the case of a person's schooling interfering with his/her education". Poleni.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tangu tulia ajikabidhi kwa Samia aliposema bunge litafuata ushauri wa serikali, badala ya serikali kufuata maagizo ya bunge, hapo ndipo nikajua bunge linaongozwa na kikaragosi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu wiki hii upo maeneo gani?
Maana[emoji1787]
 
Huyo unayemuita ajuza ni daktari wa sheria aliyekuwa mwanasheria mkuu msaidizi wa JMT. Sio saizi yangu na yako.



Ajuza sio tusi.

Halafu Kwani kufikia vyeo hivyo Ndiyo nini? Si inategemea na kujulikana au kuwa na connection kwa mteuzi?
Maana nafasi hazitangazwi.

Halafu historia ni irrelevant,

Mtu atakuhumiwa kwa maamuzi anayofanya sasa na sio hizo hadithi zako za sijui aliwahi kuwa nani na nani !

It has nothing to do with current situation.

Aamue fairly and correctly Kwa niaba ya wananchi na kwa manufaa ya Umma.

Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi .

Tutanatajia wawe wanafanya maamuzi kana kwamba ingeamuliwa na wananchi wengi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Anaowaongoza wanamuelewa na kukubali namna anavyotumia nguvu ya hoja kwenye kila utatuzi wa masuala ya kikazi.

Humu jukwaani hakuna spika anayeonekana kufanya kazi vizuri, saa nyingine watanzania tunasumbuliwa na uwezo mdogo wa kuelewa mada husika na tunatanguliza matusi na kejeli kama kinga zetu.
 
Ingekuwa nchi nyingine mbawala angeshajiuzuru mwenyewe Kwa vuguvugu la mwitikio hadi wa huo Mkataba no matter what.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…