Dkt. Tulia: Viongozi walioapa akiwemo Mkurugenzi wa Uchaguzi wasome na kuelewa Ilani ya CCM ili kumuunga mkono Rais

Huyu tulia anajitahidi kufanya mambo mengi mazuri huko mbeya. Nashangaa kwa nini hupenda kutoa matamshi matata hivi wakati kazi zake zinajipambanua zenyewe.
 
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi akasome ilani ya CCM, WTF...spika wa bunge ndio anamshauri mwenzake hivyo?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwaapisha viongozi wateule Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 27 Februari, 2023

Dr. Tulia Ackson
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson amewaasa viongozi wote walioapa leo akiwemo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kusoma na kuielewa vyema Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri kama sehemu ya kumuunga mkono Rais Samia na Serikali yake. Amesema kwa kuwa Rais amewaaamini, wanapaswa pia kurudisha imani hiyo kwa wananchi.

Pia, amewataka kutunza ahadi ya kiapo pamoja na Kumshauri Rais kwa hekima. Kiapo hakijasema kitaisha lini hivyo wanapaswa kuendelea kutunza siri Maisha yao yote.

Samia Suluhu Hassan
Rais Samia amesema alidhani atamaliza Mhula wake na Baraza lilelile la Mawaziri lakini haijakuwa hivyo, ndio maana amemteua Mhe. Ulega kuchukua nafasi.

Amewapongeza wote walioapa, amesema kuwa siyo kwamba waliochanguliwa/kubaki hawana makosa, bali yeye kama mama anawalea.

Mabadiliko haya pia yameingiza watu waliokuwa nje ya Serikali ili kuwafanya walete ujuzi wao. Amesema kila anayeonekana ana akili zaidi atanyofolewa aliko ili aingie Serikalini kuongeza uzoefu.

Ameeleza mpango wake wa kuanzisha wizara mpya ambayo itatangazwa pindi mambo ya kisheria yatakapokaa sawa.

Akitaja sababu za kufanya mabadiliko haya, amesema kuwa Kutokuelewana kati ya watendaji ni miongoni mwa sababu zilizomfanya abadili Watendaji wa Wizara. Amesema hapendi tabia hii na ikiwa itatokea tena, wahusika wote wa mgogoro huo atawaondoa.
Asante Spika.
Ila kuwa ukijua Huyu Kailima ni mzigo na bomu muda utaongeza.
Kwani hamtoshi hapo mahali.
Tume hii inatakiwa vichwa vya kuchaguliwa pande na Kona zote na hata ukiwa wa upande wa pili kuwemo ndani na isitoshe tumemianzie kwenye Halmashauri kuja juu.
 
Hii nafasi haiteuliwi na mwenyekiti wa CCM bali inateuliwa na Raisi kama Majaji, mwanasheria mkuu na mabalozi. Sasa kama nilivyosema mwanasheria mkuu naye anafuata ilani ya chama au katiba
Rais wa JMT ni lazima awe Mwenyekiti wa CCM
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwaapisha viongozi wateule Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 27 Februari, 2023

Dr. Tulia Ackson
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson amewaasa viongozi wote walioapa leo akiwemo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kusoma na kuielewa vyema Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri kama sehemu ya kumuunga mkono Rais Samia na Serikali yake. Amesema kwa kuwa Rais amewaaamini, wanapaswa pia kurudisha imani hiyo kwa wananchi.

Pia, amewataka kutunza ahadi ya kiapo pamoja na Kumshauri Rais kwa hekima. Kiapo hakijasema kitaisha lini hivyo wanapaswa kuendelea kutunza siri Maisha yao yote.

Samia Suluhu Hassan
Rais Samia amesema alidhani atamaliza Mhula wake na Baraza lilelile la Mawaziri lakini haijakuwa hivyo, ndio maana amemteua Mhe. Ulega kuchukua nafasi.

Amewapongeza wote walioapa, amesema kuwa siyo kwamba waliochanguliwa/kubaki hawana makosa, bali yeye kama mama anawalea.

Mabadiliko haya pia yameingiza watu waliokuwa nje ya Serikali ili kuwafanya walete ujuzi wao. Amesema kila anayeonekana ana akili zaidi atanyofolewa aliko ili aingie Serikalini kuongeza uzoefu.

Ameeleza mpango wake wa kuanzisha wizara mpya ambazo zitatangazwa pindi mambo ya kisheria yatakapokaa sawa.

Akitaja sababu za kufanya mabadiliko haya, amesema kuwa Kutokuelewana kati ya watendaji ni miongoni mwa sababu zilizomfanya abadili Watendaji wa Wizara. Amesema hapendi tabia hii na ikiwa itatokea tena, wahusika wote wa mgogoro huo atawaondoa.
Huyu Mnyarwanda Mnyakyusa ana kauli tata sana!
 
Itachukua muda sana Waafrika kuwa na akili...

Sisi ni mateka wa ujinga wetu wenyewe, ni watumwa watiifu wa ujinga wetu wenyewe...
 
Rais wa JMT ni lazima awe Mwenyekiti wa CCM

Sio lazima na hata huyu Raisi alipata Uraisi kabla hajawa mwenyekiti. Lakini ukiwa Raisi haina maana kuwa teuzi unazofanya zote ni za kichama mfano mwana sheria mkuu sio nafasi ya kisiasa, majaji sio nafasi za kisiasa. Nchi zote za kidemokrasia ndiyo mfumo Raisi anateua lakini haina maana kila nafasi ni ya kisiasa. Nafasi ya mkurugenzi wa uchaguzi sio nafasi ya kisiasa. Sasa kwenye ilani kuna lini kuhusu mkurugenzi wa uchaguzi? Kuiba uchaguzi au?
 
Wasomi dizaini ya Dr. Tulia ndiyo wanasababisha vilaza kama baby taley wanunue PhD za mchongo.
 
Sio lazima na hata huyu Raisi alipata Uraisi kabla hajawa mwenyekiti. Lakini ukiwa Raisi haina maana kuwa teuzi unazofanya zote ni za kichama mfano mwana sheria mkuu sio nafasi ya kisiasa, majaji sio nafasi za kisiasa. Nchi zote za kidemokrasia ndiyo mfumo Raisi anateua lakini haina maana kila nafasi ni ya kisiasa. Nafasi ya mkurugenzi wa uchaguzi sio nafasi ya kisiasa. Sasa kwenye ilani kuna lini kuhusu mkurugenzi wa uchaguzi? Kuiba uchaguzi au?
Ndio sababu nimekuambia muundo wa Katiba ya JMT ni wa Chama kimoja

Rais wa JMT lazima awe Mwenyekiti wa CCM!
 
Sasa muundo wa katiba ya nchi una uhusiano gani na muundo wa katiba ya chama. Mwenyekiti ni muundo wa katiba ya chama sio nchi. Wakati CUF ikigombea Malim Seif hakuwa mwenyekiti wa chama! Katiba ya nchi ni tofauti na katiba ya chama naona huelewi hili. Pata elimu kwanza inaelekea mambo mengi bado hujaelewi
 
Yaani Mkurugenzi wa uchaguzi ni wa chama au serikali? Anatakiwa kufuata sheria na katiba. Haja apa kwa kulinda sera za chama kwasababu ni nafasi ya kiserikali sio ya kichama. Ni sawa na mwanasheria mkuu aseme atasoma sera za CCM badala ya kuahidi kufuata sheria
Tulia ana ukuda na unazi wa KICCM Kupindukia. Mpaka anasahau majukumu ya kisheria ya baadhi ya Wateule kama Mkurugenzi wa Uchaguzi
 
Akemee na dhana hasi ya ‘kuula’…..

But I doubt it.

That would be asking too much from her.

Don’t think she’s capable of even thinking about it….
Roho mbaya inakusokoya bure. Be nice to your president Nigga.
 
Sasa muundo wa katiba ya nchi una uhusiano gani na muundo wa katiba ya chama. Mwenyekiti ni muundo wa katiba ya chama sio nchi. Wakati CUF ikigombea Malim Seif hakuwa mwenyekiti wa chama! Katiba ya nchi ni tofauti na katiba ya chama naona huelewi hili. Pata elimu kwanza inaelekea mambo mengi bado hujaelewi
Endelea kukariri!

Katiba ya JMT ni ya 1977

Katiba ya CCM ni ya 1977

Hivyo vyama vyenu Katiba zake zinaanzia 1992

Freeman Mbowe na Hamad Rashid ndio watanielewa Siyo Wewe!
 
Nionyeshe sehemu kwenye katiba inayoonyesha kwamba majukumu ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ni ya kichama na sio ya kisheria. Mwenyekiti wa trume kazi yake ni kusimamia uchaguzi sio sera. Unatafuta kiki sasa
 
Kwani sheria za Tanzania zinasimamiwa na nani?

Kama hujui muulize Mbowe au Halima James Mdee!
 
Sheria za Tanzania zinaaimamiwa na mwana sheria mkuu sio Raisi! Umesoma siasa za wapi? Hata kwenye nchi za kubwa Raisi anachagua mwana sheria mkuu lakini haina maana anapeleleza wapinzani pekee ni msimamizi wa sheria zote kwa mtu yeyote. Nenda kaangalie sheria inasema kazi za mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ni nini?
 
Wewe unazungumzia sheria za Kwenye makaratasi!

Hiyo AG si ndio yuko Bungeni na akina Halima Mdee au umesahau

Unaishi kwa kukariri!
 
Back
Top Bottom