johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Huyo Saidi ndio mshenzi pekee aliyenyongwa utawala wa Nyerere!Swala sio uchaga.. swala sio uchadema.. swala Zima ni kwamba, kleruu alikuwa mdwanzi Sasa akayakanyaga kwa mhehe asiefagilia unyonge akamnyoosha mchana kweupee... R.i.p mwamwindi
Mchonga alitia saini kwa kuwa kleruu alikuwa mshkaji Wake. Ila kiukweli kleruu alikuwa mdwanzi na kwa taarifa yako tu mwamwindi anaehesabika Kama shujaa iringa kwa kitendo chake Cha kukataa unyonge na dharau dhidi ya kleruuHuyo Saidi ndio mshenzi pekee aliyenyongwa utawala wa Nyerere!
Mwamwindi au Kleruu?Hilo jina kwa Mara ya kwanza nililiona nilpofka chuo cha mifugo na kilimo ironga kilosa morogoro kuna bweni pale linaitwa jina hilo
Kleruu
Mnooo....tena alitoka kunywa pombe kijiji cha Chang'olo,ndio akaja na pombe zake hadi shambaniKwa maelezo mbalimbali hapo juu inaonekana Mkuu wa mkoa alikuwa mchokozi
Nadhani katika kusaini hukumu ile Mwl Nyerere alikuwa katika capacities mbili: Ya kwanza kama Rais wa nchi ambaye sheria inasema ndiye atakayeridhia utekelezwaji wa hukumu ya kifo inapotamkwa na mahakama, lakini ya pili ni capacity ya kibinadamu ya kutaka kumlipia rafikiye kisasi, ambayo hii inaelekea ilimzidi. Imagine katika miaka 23 ya uongozi wake, ni watu wengi sana walihukumiwa adhabu za kifo, lakini aliridhia 3 tu, mojawapo ikiwa hii ya Mwamwindi. Labda zingeletwa na hizo hukumu nyingine alizosamehe tukaona hazikumgusa binafsi naweza kufuta maneno yangu, lakini nahisi kutekelezwa kwa hukumu hii haraka haraka kulichangiwa pia na ukweli kwamba kosa lililotendwa lilimuumiza Nyerere binafsi. Hivi kwa mfano ukipigana na mtu mtaani ukamuumiza halafu ukakamatwa ukashitakiwa mahakamani, na huko ukakuta hakimu ni baba mzazi wa mlalamikaji, unatarajia nini? Sisemi ilikuwa sawa Nyerere kuendeshwa na hisia binafsi, lakini tunapaswa kuangalia pia namna ya kudhibiti hali kama hii. Katika mahakama zetu kuna utaratibu (sijui kama umeandikwa au la) kuwa hakimu akiona kesi husika ana maslahi nayo, huwa anajitoa na kuomba ipangiwe hakimu mwingine. Kwa rais wa nchi hali ikoje? Hivi mtu akihukumiwa kunyongwa kutokana na kutenda jambo ambalo liligusa maslahi binafsi ya rais (rafiki yake, familia yake nk), rais anaweza kusema kuwa 'anajitoa' katika suala la kuridhia utekelezwaji wa hukumu hiyo?
Mzee Said Mwamwindi katika miaka ya mwanzo ya 1970 alimuua Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Kleruu ambaye alikuwa akitumia madaraka ya ofisi yake kunyanyasa wananchi.
Kwa wakati ule alishtakiwa kwa mauaji na kuhukumiwa kunyongwa kama muuaji.
Lakini ni kama Solomon Mahlangu aliyehukumiwa na mahakama ya makaburu kwa hatia ya ugaidi na uhaini anavyo onekana Leo shujaa na mpigania uhuru, kwanini na sisi tusimtangaze Mzee Said Mwamwindi kama shujaa na mpigania haki dhidi ya watumia ofisi vibaya dhidi ya Wananchi?
Maana baada ya tukio lile tabia za ma RC na ma DC zilibadilika na kuheshimu sheria na katiba hadi kilipo ingia madarakani kizazi hiki kisicho soma historia.
SAID MWAMWINDI NI SHUJAA
Sent using Jamii Forums mobile app
Pascal Mayalla tusaidie kujibu swali hilo kwani mwenzetu umesoma sheria pale mlimani.Ikitokea mtu akashikwa na hasira baada ya kutukanwa hadharani na kiongozi kwa uonevu, kwa nyakati hizi nini kitatokea?
Du ! Post hii ni ya long time sana, lakini nimeona nichangie ! Mkuu hukumjua Dr. Kleruu kweli ? But after numerous responses you came to understand who he was and what he did ! Happy new year 2020 🙂Alikuwa daktari wa nini huyu Kleruu? Alikuwa kabila gani?
Pia kuna issue ya kuwa Nyerere wakati mwingine alikuwa anatibiwa mambo ya akili, je inawezekana alikuwa "incapacitated" wakati wa kuweka saini hapa? inawezekana personal loss za huyo Dr. Kleruu iliweza kumfanya mzee wa watu akawa katika hali ya kutoweza kutoa maaamuzi akiwa timamu. Naweza nisi-substantiate hizi habari za Nyerere kutibiwa mambo ya akili ila kuna daktari mmoja wa muhimbili kipindi cha nyuma aliwahi kunigusia kuwa alikuwa na tatizo hili na familia yake wana tatizo la akili vile vile.