Dkt. Yahaya Nawanda apandishwa Kizimbani kwa Tuhuma za Ulawiti, aachiwa kwa dhamana

Dkt. Yahaya Nawanda apandishwa Kizimbani kwa Tuhuma za Ulawiti, aachiwa kwa dhamana

Ameburuzwa kwenye Mahakama ya Mkoa wa Mwanza akikabiliwa na kosa moja la Ulawiti

Amepandishwa leo July 9 baada ya makelele mengi ya wadau kutaka haki itendeke

Bado haijajulikana kama ataswekwa Rumande au atapata dhamana.

====

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Yahaya Nawanda, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza na kusomewa shitaka moja la kumwingilia kinyume na maumbile Tumsiime Ngemela (21) katika eneo la Rock City Mall jijini Mwanza.

Mshtakiwa huyo amefikishwa katika mahakama hiyo mapema leo Julai 9, 2024 na kusomewa shitaka hilo ambalo anadaiwa kulitenda Juni 2, 2024 katika eneo hilo kinyume na kifungu cha sheria cha 154 kifungu kidogo (a) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Erick Maley, Waendesha mashtaka wa kesi hiyo ambao ni Wakili wa serikali Magreth Mwaseba na Martha Mtiti waliitaja kesi hiyo kuwa ni kesi namba 1883 ya mwaka 2024.

Hatahivyo mshtakiwa alikana shtaka hilo na yuko nje ya dhamana baada ya kukamilisha masharti aliyokuwa amewekewa ambayo ni kuwa mtumishi wa serikali pamoja na bondi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh 5 milioni.

Baada ya kukamilisha masharti hayo, Mshtakiwa yupo nje ya dhamana hadi Julai 16, 2024 ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa hoja za awali huku upande wa mlalamikaji ukitakiwa kwenda na mashahidi.

Pia soma
Hapo hakuna kesi, CCM inanmtengenezea mazingira ya kukutwa hana hatia maana wafiraji na wasagaji wamejazana huko CCM
 
Kama ingekuwa nchi kama Marekani ambako kuna makampuni ya uchunguzi yaliyosajiliwa kampuni mojawapo ingepewa kazi na wakili wa mtuhumiwa kuchunguza credibility ya huyo binti yaani matendo yake ya nyuma , kama aliwahi kudanganya kwa masuala ya kisheria, ikithibitika aliwahi kuongopa basi kesi ingetupwa. Rejea kesi ya Rais wa zamani wa banki ya Dunia ilikuwa kama hii. Kuna binti mfanyakazi wa hoteli alimpakazia kuwa amembaka, Huyo binti anatoka Africa Magharibi, basi hiyo kampuni ikafanya uchunguzi ikaonekana huko nyuma huyo binti wakati anaomba visa kuingia Marekani aliwahi kudanganya hivyo sio credible; kwa,msingi huo kesi ya ubakaji dhidi ya Rais huyo wa zamani wa benki ya dunia ikatupwa.

..ukikosekana ushahidi wa kitabibu ndipo kesi inakwenda ktk hatua ya kuangalia credibility ya mtoa madai ya tukio la ubakaji.

..Kama kuna ushahidi wa kitabibu kwamba huyo binti aliingiliwa kesi itakuwa ngumu kwa mheshimiwa RC.

..Katika mazingira hayo sina uhakika kama madai kwamba huyo binti hana tabia njema, au aliwahi kumshitaki mtu mwingine kama anavyofanya kwa RC, yatapewa uzito mkubwa.
 
Nyota ipi huyo kil.aza alikua nayo? Yaani waache kumpa kesi Mpina wampe huyo zero brain? We usubiri issue kuwa kwenye uke au njia ya haja kubwa kwamba wakemia hawajui tofauti au ndio unaleta ujuaji tu?

Nyie mkae kwa kutulia subirini ushahidi na vielelezo I believe hata kuna message alimtumia kumuomba radhi kumuingilia so yote yatawekwa wazi tu.
Wilaya zipo nyingi kuliko mikoa.Ni mara chache watu kupanda kutoka Mkuu wa Wilaya mpaka kuwa Mkuu wa Mkoa.Wengi huishia hapo hapo na kupotea.
Kwa yeye kupanda Cheo haraka,ninamchukulia kama mtu mwenye Bidii Fulani na Bahati.Ndio maana nilisema Nyota yake iling'aa.
Ingekuwa ni Zerobrain kabisa kama unavyosema asingekuwepo hapo alipo.
Kuhusu Mkemia kujua tofauti kati ya Uke na njia ya haja kubwa kwa kutumia karatasi zilizotumika kufuta uchafu baada tendo hilo siwezi kujua.
Kama akiiona tofauti hiyo na ikatumika kumtia hatiani mtuhumiwa nataishangaa Mahakama kwa uamuzi huo.
Kweli unaamini Kuwa mtu anaweza kuandika ujumbe wa kumuomba radhi mwanamke kwa kumuingilia kinyume na maumbile kwenye simu?
Kama aliandika kweli basi ndio vizuri,kesi inaisha mapema.
Tunachotaka Haki itendeke,pande zote mbili.
Kuhusu Kwa nini hawajamharibia Mpina,inategemea na dhima ya wanaotaka kukuharibia.Pia weak points zako,Umegusa nini au maslahi ya nani!
Mimi nimezungumzia ninachokiona tu,sio lazima kiwe sahihi.
 
Nyota ipi huyo kil.aza alikua nayo? Yaani waache kumpa kesi Mpina wampe huyo zero brain? We usubiri issue kuwa kwenye uke au njia ya haja kubwa kwamba wakemia hawajui tofauti au ndio unaleta ujuaji tu?

Nyie mkae kwa kutulia subirini ushahidi na vielelezo I believe hata kuna message alimtumia kumuomba radhi kumuingilia so yote yatawekwa wazi tu.
Hapo sasa!
 
Wacha haki itendeke. Swali langu, Je, ikithibitika ni kweli Nawanda alimlawiti yule binti, zile pesa milioni 10 alizopewa binti atazirudisha au zitakuwa zake au??

Wanasheria mtusaidie hapa. Maana binti aliulizwa ulipewa kiasi gani na Nawanda. Akajibu, alipewa milioni 10 cash. Anazo na hajazitumia hata shilingi.
Mtuhumiwa akizidai tu hizo pesa atakuwa amemulika kwenye uthibitisho kwamba katika siku tajwa, saa na mahali alikutana na huyo msichana na akamtendea kitendo kilichozidi mahusiano ya kimapenzi ambayo mwenzie yalimsababishia madhara ya kimwili na kisaikolojia bila ridhaa hivyo alivunja sheria.

Sexual offences special provisions section 154 (1), (a)
1720539140795.png
 
Ameburuzwa kwenye Mahakama ya Mkoa wa Mwanza akikabiliwa na kosa moja la Ulawiti

Amepandishwa leo July 9 baada ya makelele mengi ya wadau kutaka haki itendeke

Bado haijajulikana kama ataswekwa Rumande au atapata dhamana.

====

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Yahaya Nawanda, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza na kusomewa shitaka moja la kumwingilia kinyume na maumbile Tumsiime Ngemela (21) katika eneo la Rock City Mall jijini Mwanza.

Mshtakiwa huyo amefikishwa katika mahakama hiyo mapema leo Julai 9, 2024 na kusomewa shitaka hilo ambalo anadaiwa kulitenda Juni 2, 2024 katika eneo hilo kinyume na kifungu cha sheria cha 154 kifungu kidogo (a) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Erick Maley, Waendesha mashtaka wa kesi hiyo ambao ni Wakili wa serikali Magreth Mwaseba na Martha Mtiti waliitaja kesi hiyo kuwa ni kesi namba 1883 ya mwaka 2024.

Hatahivyo mshtakiwa alikana shtaka hilo na yuko nje ya dhamana baada ya kukamilisha masharti aliyokuwa amewekewa ambayo ni kuwa mtumishi wa serikali pamoja na bondi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh 5 milioni.

Baada ya kukamilisha masharti hayo, Mshtakiwa yupo nje ya dhamana hadi Julai 16, 2024 ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa hoja za awali huku upande wa mlalamikaji ukitakiwa kwenda na mashahidi.

Pia soma
Kosa la kubaka na kulawiti sina hakika kama lina dhamana.
 
Yesu anasemaje kuhusu kulawiti?
1 WAKORINTHO 6:9 INASEMA
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi Ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti.

ENGLISH: "Know ye not that the unjust shall not inherit the kingdom of God? Do not err: neither fornicators nor idolaters nor adulterers nor effeminate nor homosexuals.

TAFSIRI NYINGINE: 9 Or do you not know that wrongdoers will not inherit the kingdom of God? Do not be deceived: Neither the sexually immoral nor idolaters nor adulterers nor men who have sex with men[a] 10 nor thieves nor the greedy nor drunkards nor slanderers nor swindlers will inherit the kingdom of God.
 
Back
Top Bottom