Dodoma: 12 wafariki na 63 kujeruhiwa kwenye ajali ya Basi la Frester kogongana na Lori

Dah!! Ajali imetupunguzia tena wanaume!
Walah tutaowana wanawake kwa wanawake tunapoelekea
 
Kwamba nikichukua bunduki saa 7 usiku nikavamia sehem nikaiba polisi hapaswi kulaumiwa?
Ile ni Huduma sio uhalifu. Na wamepewa utaratibu wa kutoa huduma. Wamesomea namna ya kuendesha hayo mabasi. Hakuna Dereva anayeendesha basi kubwa ambaye hajasomea udereva. Na hakuna Tajiri anamwajiri Dereva wa basi asiyesomea udereva na kuwa na uzoefu wa kuendesha basi. Basi ni Mali ya mtu yenye thamani kubwa lakini pia Kuna abiria ambao ni roho za watu.
Mara nyingine Polisi anauliza kama Dereva alikua anaendesha gari vizuri abiria wote wanamtetea Dereva. Hapo utawalaumu Vipi Polisi. Mbona Ndege au Meli zinafuata utaratibu kulingana na njia zake na Hali ya hewa . Na hawasemi mpaka wasimamiwe na Polisi muda wote Huko baharini au angani.

Mara nyingi ukiwa kwenye basi Polisi akisimamisha basi na kuingia ndani kutoa hata salamu na kujua changamoto abiria wanakua wakwanza kunungunika na kuona kuwa anawachelewesha .

Hao TRAFIKI walioko wenyewe TU wanaonekana kama Kero na wengi Barabarani Sasa unataka wapange mstari kuanzia Kagera Mpaka DSM kuzuia madereva wasiojali maisha yao na ya watu wengine.
 
Dah!! Ajali imetupunguzia tena wanaume!
Walah tutaowana wanawake kwa wanawake tunapoelekea
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hatari sana . Waombeeni úzima Toka Kwa Mungu. Mungu awakinge wanaume na madhili Yote katika Maisha.
 
Hi kweli mdau,mi Baada ya kuzipanda hizo Frester km mara nne kutokea pale cbe dom na kuonekana mi ndo mshamba wa mwendokasi nimehamia kwenye Saratoga au advanture za kutoka Kigoma.Hao Frester wanakimbia mno
We km Mimi brooo...sipandi,majinjah Osaka Wala frester pale CBE Dom,hizo gari hapana,napanda Adventure na Saratoga Dar Kumi naingia asubuhi au alfajir habari sipati na nafika vzr Tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwamba gari ilikua na abiria 75?

Na inabeba abiria 53
Kuna vindoo mule kwenye mabasi vinakaliwa na abiria,nshakalia ndoo kuanzia CBE kwenye gari Zifuatazo,majinjah,simiyu yetu, adventure,Saratoga na pia wanasimamisha wengine then gari za kutoka Huko masafa Zina watoto wengi mnoo wanapakatwa na wazazi wao kukuta abiria 80 kawaida tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Na list iliyotoka ya majeruhi na waliopona mbona ina watu less than 40

Hata kama ni excess hapa kuna walakini ndio mabasi yatabeba excess lakini ndo 20+? Duh
 
We km Mimi brooo...sipandi,majinjah Osaka Wala frester pale CBE Dom,hizo gari hapana,napanda Adventure na Saratoga Dar Kumi naingia asubuhi au alfajir habari sipati na nafika vzr Tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hizo za kigoma ndo nimehamia kila ninapokuwa natoka hapa Cbe.......hayo mengine wanatumia ule uchovu walionao abiria kuwa ndo kigezo kwa wao kumwaga mambio,maana abiria wengi wanakuwa wamelala na mwendo hawauoni
 
Na list iliyotoka ya majeruhi na waliopona mbona ina watu less than 40

Hata kama ni excess hapa kuna walakini ndio mabasi yatabeba excess lakini ndo 20+? Duh
Watoto wanaopakatwa huwa ni wengi sana.......aghlabu sana kukosa watoto kumi na kuendelea kwenye basi moja na ukizingatia njia hizo hawasisitizi kila abiria kwa kiti kimoja km ilivyo njia za kaskazini
 
Na list iliyotoka ya majeruhi na waliopona mbona ina watu less than 40

Hata kama ni excess hapa kuna walakini ndio mabasi yatabeba excess lakini ndo 20+? Duh
Sabini kawaida Broo..pale kwa dereva Wanakaa watu 3,vindoo sita ,halafu Kuna wanaosimama kama 7 hivi pale kati broo wanakalish si chini ya watu 15 to 20!!!ukijumlisha na wale abiria 53 na watoto wadogo waliowabeba mbona 75 mpk 80 inafika
Jaribu kuexperience siku moja

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hizo za kigoma ndo nimehamia kila ninapokuwa natoka hapa Cbe.......hayo mengine wanatumia ule uchovu walionao abiria kuwa ndo kigezo kwa wao kumwaga mambio,maana abiria wengi wanakuwa wamelala na mwendo hawauoni
Kabisa za kigoma ni salama mdogo mdogo mnafika

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hili basi lilibeba watu wangapi?
12 dead + 62 majeruhi + wazima.wasiojulikana idadi yao. Kuna basi linawezabeba abiria wote hao hapa Tanzania?
 
Hebu define huyo shetani na hao vibaraka wake. Uzembe wa binadamu mwenyewe kwa kusinzia, kutokuwa makini au uchovu halafu kiurahisi tu tunamsingizia shetani.
Yaan unamtetea shetani kweli? Ehh hayo mauzembe,kusinzia n.k ni kazi ya shetan hyo ili analeta ili uharibu,Mungu hawezi kuletea usingiz wakat unaendesha,endelea umtetea tu
 
Hii ya malori kuungana kama treni kiukweli kabisa ni kero kubwa sana. Si kwamba nasifia speed ila haya malori yanakuaga kama yanafanya kusudi vile. Fikiria hapo yapo 10 yameungana alafu sasa speed yao 5kph.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…