Dodoma: 12 wafariki na 63 kujeruhiwa kwenye ajali ya Basi la Frester kogongana na Lori

Dodoma: 12 wafariki na 63 kujeruhiwa kwenye ajali ya Basi la Frester kogongana na Lori

Usiku ndio kutamu kwa kukimbia sababu lami imepoa. Usiku hata ukiwa na tyre za mchongo unafika uendako bila kwere taa na macho yawe vizuri tu.
We kimbia tu,sisi tutakuja kula ubwabwa

Ova
 
Screenshot_20230209_163612_Chrome.jpg
 
Dereva wa kibongo hata umuweke miundo mbinu gani bado ajali zitatokea

Discipline Discipline tena madereva wa sasa hawa waliyoanza kuendesha magari miaka 2000 ni shida

Ova
Miundo mbinu ni mwarobaini Mkuu.

Kumbuka miaka ya 1990 mpaka 2005 jinsi ajali zilivyokuwa nyingi Barabara ya Kuanzia Kibaha mpaka Morogoro. Ukifika Chalinze kuelekea Morogoro ilikua ni janga kubwa sana. Baada ya kufanyia ukarabati mkubwa na kuweka njia za kuchepuka ajali imekua ni nadra sana kutokea kwenye Barabara hiyo.

Hata uwekaji wa matuta unawekwa kimakosa.
TANROAD katika kubana matumizi wanaweka vituta vidigo Maarufu Kwa Jina la Rasta badala ya matuta makubwa . Matokeo yake magari makubwa kama mabasi hayapubguzi Mwendo na mara nyingi yanaharibik1
 
Unakariri fresta niza kahama tu, zipo znatoka morogoro-bukoba, yapo Barbara ya moro-dar yanazurula tu.

Hua mnajua yatokaga kahama tu kwenda mwnza na dar tu. Safiri kaka acha kukaa barabarn kushangaa magar

Sio nakariri ni vile mtoa post alivyotoa post yenyewe ,.
Kabla ya kuleta update aliandika ajali imetoka asubuhi, basi ikitokea kahama.
Wewe utakuwa umekuja kusoma baada ya kuedit post .
Soma post#20, na #83 wote wanashanga basi itoke Kahama halafu ipate ajali kibaigwa saa 1 asubuhi.
Nasafiri sana na nafahamu ratiba na rout za mabasi mengi.
Acha kukurupuka
 
Ni ajali mbaya sana imetokea hapa Kibaigwa Silwa, bado mchakato wa kubaini athari unaendelea.
Nita-updates soon ngoja tuokee watu kwanza.

Kama una ndugu yako alipanda basi hilo kutokea njia ya bukoba kwenda Dar

USSR

===
Ajali imetokea Kijiji cha Silwa, Kata ya Pandambili,Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, baada ya Basi la Frester lenye namba za Usaji T 415 DPP kugongana na lori lililokuwa linatokea Morogoro kwenda Dodoma saa saba Usiku wa kuamkia leo tarehe 9/02/2023.

Ajali hiyo imesababisha Vifo ni 12 ambapo waliofariki ni Wanawake 4 na Wanaume 8. Majeruhi ni 63.

View attachment 2511188View attachment 2511189View attachment 2511190
View attachment 2511398View attachment 2511399View attachment 2511400
siku wakilipotiwa watu wanao kufa na kuwa walemavu sababu ya boda boda na noha nchi nzima kwa siku kila mtu atashika mdomo!!!chanjo kikuu cha hajari nchi hiii polisi barabalani watu wamelalamika mpaka wameamua kunyamaza kumia ndani kwa ndani mamlaka sijui zinawaogopa hawa watu
 
Kuzidi Kwa abilia kunaweza sababisha ajali? Dadavua
ndugu yangu unapopata ajali ya gari, makosa yote huainishwa hata bima tu itachunguzwa lakini kwa namna yoyote ile haisababishi ajali, bora hata kuzidisha abiria inaweza kusemwa gari lilizidi uzito likapoteza mwelekeo.
 
Majeruhi 63
Marehemu 12
Jumla 75
Uwezo wa Basi 52+dereva na konda.
Polisi wapo, barrier zipo, katazo la kutembea usiku lipo. Sheria ya kila abiria akalie kiti ipo.
Nini mbaya katika hii sekta.?

Hii tabia ya kuzidisha abiria kwa tamaa ya posho iko Sana mabasi ya Moro na tanga. Lkn who cares.
Surprise Basi la Moro au tanga lazima ukute Kuna abiria wamekaa kwenye engine. Matrafik wengi aidha Ni vipofu hawalioni au wanagawiwa posho.

Nakumbuka Kuna siku tunatoka Mwanza abiria mashabiki wa mwendo kasi wanamwambia dereva. Mimi nitakulipia faini mbili, mwingine mbili, inamaana dereva akitoa rushwa kwa polisi abiria ndio wanaingia mfukoni.
Hizi sheria huwa madereva hawazingatii kabisa, ila hata abiria na sisi sijui huwa nini kinatufanya kujazana kwenye gari,ifike hatua sasa na abiria akijaa kwenye gari na yeye pamoja na dereva na kondakta wote wapigwe faini, sheria nazo ziwape mamlaka abiria wakamate gari linalovunja sheria,abiria wakamate gari na walipelekea polisi na kama ni faini ilipwe ndani ya gari,ifike wakati iwe ni kosa kisheria kwa kondakta kuongea na trafiki nje ya gari,yani liwe ni kosa la moja kwa moja kwa trafiki na kondakta,hapa pakiwekwa mitego michache kabisa, adabu itarudi.
 
Yote kwa yote, yule RPC wa sasa wa Mwanza, former mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, alikuwa anafanya kazi nzuri. Huyu wa sasa yawezekana ana compliance kiaina.
Kwani yeye alikua anaendesha hayo magari Barabarani.?

Magari yanagongana Uso Kwa uso hapo tatizo linamhusu Vipi mkuu wa kikosi.
Tatizo ni miundo mbinu na uzembe wa madereva wenyewe.
Hapo hakuna wa kulaumiwa zaidi madereva wenyewe na miundo mbinu isoyoendana na wakati huu wenye magari Mengi na shughuli nyingi za kiuchumi zinazowafanya watu kukimbizana na maisha.

Lakini pia Kuna suala la maslahi Duni ya madereva na wasimamizi wa SHERIA Barabarani.
TRAFIKI wanafanya kazi ngumu Kwa mishahara Duni inayowafanya kuishi Kwa kutegemea zaidi rushwa zinazotokana na kiwababaisha madereva na kuwatishia kuwaandikia faini nyingi Barabarani matokeo yake madereva wanalazimika kutoa rushwa.
Dereva amepewa mzigo wa ndizi kutoka Rombo , na Elfu 50 kama posho. Anakutana na askari Barabarani wasiopungua 50 mpaka akifika DSM ,matokeo yake posho yote inaishia kwenye mikono ya askari njiani na mara nyingine anaandikiwa faini mana Hana Tena pesa za kugonga. Kosa lenyewe ni mpasuko mdogo kwenye kiyoo.
Matokeo yake madereva wanakua na maisha Duni na stress kubwa . Huku wakiwa wanaendesha magari kama watumwa wasioijua kesho yao.
Hali kadhali Polisi nao hivyo hivyo wanasimamia SHERIA Kwa Lengo la kupata chochote badala ya kuzuia makosa na kutoa Elimu.
Ingekua kwenye Beria wanawasimamisha madereva na kuwapima kilevi au kuwaambia wapaki magari wapumzike nusu saa kupunguza usingizi lakini Hilo ni kinyume chake kabisa wanatumia nafasi hiyo kuomba pesa ili kupunguza ugumu wa MAISHA kutokana na mishahara Duni isiyotosha Kununua chakula Kwa Mwezi mmoja achilia mbali mahitaji mengine na familia .
 
Back
Top Bottom