Dodoma: 12 wafariki na 63 kujeruhiwa kwenye ajali ya Basi la Frester kogongana na Lori

Dodoma: 12 wafariki na 63 kujeruhiwa kwenye ajali ya Basi la Frester kogongana na Lori

Mbona RC hajawasimamisha kazi madaktari kwa kutokufika eneo la ajali kwa wakati?
Nani kasema hawakufika kwa wakati sahihi ,tena bila wao wangekufa wengi manesi na madaktari walifika haraka sana tena sana ,acha ukilaza binti unaonekana una matatizo ya akili

USSR
 
Tulounga mkono madereva kupunguziwa adhabu barabarani, trafiki kupunguzwa barabarani, tochi kulegezewa mwendo wake wa kumulika watu, madereva kuonewa huruma, sasa tujipongeze kwa kazi nzito ya kuruhusu ajali za barabarani.
Tungekuwa tunawapa adhabu kali madereva , faini zingekuwa kubwa, trafiki wangeendelea kula vichwa vya madera wazembe haya yasingetokea
Tuendeleeni kuomboleza.
Matrafiki kujazana kula rushwa ni kero kwa madereva wengine ambao wastaarabu. Waweke lane separators magari yasikaribiane kama ilivyo sasa
 
Mkuu mimi ni dereva na naongea kwa experience usiku ni hatari mara 1000 kuliko mchana, watu wengi wamechoka usiku wanatembelea reserved energy, wengi wamevurugwa na macho yao hayawezi kuhimili mwanga wa taa, wengi hukimbia sana bila kuchukua tahadhari, wembamba wa barabara na mashimo, malori yanayopaki bila kuweka alama yeyote, uzoefu mdogo wa madereva wengine, haya yote husababisha ajali sana usiku.
Usiku ndio kutamu kwa kukimbia sababu lami imepoa. Usiku hata ukiwa na tyre za mchongo unafika uendako bila kwere taa na macho yawe vizuri tu.
 
Duh.... Mwezi mmoja uliopita familia yangu ilikuwa kwenye hili basi. Mungu awarehemu
 
Ni ajali mbaya sana imetokea hapa Kibaigwa Silwa, bado mchakato wa kubaini athari unaendelea.
Nita-updates soon ngoja tuokee watu kwanza.

Kama una ndugu yako alipanda basi hilo kutokea njia ya bukoba kwenda Dar

USSR

===
Ajali imetokea Kijiji cha Silwa, Kata ya Pandambili,Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, baada ya Basi la Frester lenye namba za Usaji T 415 DPP kugongana na lori lililokuwa linatokea Morogoro kwenda Dodoma saa saba Usiku wa kuamkia leo tarehe 9/02/2023.

Ajali hiyo imesababisha Vifo ni 12 ambapo waliofariki ni Wanawake 4 na Wanaume 8. Majeruhi ni 63.

View attachment 2511188View attachment 2511189View attachment 2511190
View attachment 2511398View attachment 2511399View attachment 2511400


Roho ya mauti imeinuka kwa kasi
Tumuombe sana Mungu
 
Ukiwasikiliza watu wanaoahabikia usiku watakupa sababu wabakwepa usumbufu wa polisi na tochi zao, hapa utajua ni watu wa kukimbia hovyo bila kujali alama za barabarani
Hatari Sana Hasa Usiku Mwingi
 
Mkuu wa Usalama barabarani ajiuzulu, kama sivyo basi IGP ajiuzulu. Wameshindwa kutuhakikishia usalama.
 
Taifa gani ambalo watu wanaangamia lakini wale wanaolipwa kwa kodi zetu kutuhakikishia usalama, hawawajibiki. Na Rais na cabinet wake wanakaa kimyaaa!!!
 
Sahihi Usemacho Lakini Mamlaka Ya Kudhibiti Nauli Nayo Ipo Shida
Dar Es Salaam ~Kagera Nauli 80000/= Moja Kwa Moja Sasa Ukishuka Njiani Usafiri Mpya Shida Tena
... usalama kwanza mkuu fedha nini? Safari kama ya Bukoba - Dar more than 1200km sio mchezo; sio abiria, dereva, wahudumu na hata chombo chenyewe kinachoka mbaya ukizingatia na kesho yake over and over again wanageuza!

Ukiwa Dodoma pale, saa 11 jioni ndio gari za Mwanza/Bukoba/Kigoma/Musoma - Dar/Mbeya/Songea ndio zinakuwa zinaingia. Unajiuliza huko zinakoenda bado masaa 8 mbele ndio zifike! Utaratibu ungelazimisha Dodoma iwe ndio hub pa abiria kubadili magari; unless zinazovuka hapo total distance haitazidi 800km.
 
Kama kawaida masuluhisho zimamoto kazini.

Hata hivyo tatizo kubwa kwenye ajali hizi ni ujinga yaani elimu duni ya madereva.

Kiwango cha chini cha elimu kuendesha vyombo kama hivi vingekuwa reviewed.

Mfano, kama graduates wanaosaka ajira wangepewa hizi kazi wakalipwa vizuri matatizo haya yangegeuka historia.
... binadamu hujifunza kutokana na makosa; taratibu hubadilika baada ya makosa au changamoto kutokea. Mimi nashauri tu humu mitandaoni; sina nafasi ya maamuzi. Tunapiga tu soga za hapa na pale that simple don't take it serious.
 
... usalama kwanza mkuu fedha nini? Safari kama ya Bukoba - Dar more than 1200km sio mchezo; sio abiria, dereva, wahudumu na hata chombo chenyewe kinachoka mbaya ukizingatia na kesho yake over and over again wanageuza!

Ukiwa Dodoma pale, saa 11 jioni ndio gari za Mwanza/Bukoba/Kigoma/Musoma - Dar/Mbeya/Songea ndio zinakuwa zinaingia. Unajiuliza huko zinakoenda bado masaa 8 mbele ndio zifike! Utaratibu ungelazimisha Dodoma iwe ndio hub pa abiria kubadili magari; unless zinazovuka hapo total distance haitazidi 800km.
Ite iwe hub kuna magari yamekwenda congo, Uganda,Kenya Zambia na n.k cha msingi ni kubadilisha dereva tu niliwahi kutoka Kampala ukifika kahama mtu anamle mwenzake

USSR
 
Au gari za abiria zisisafiri zaidi ya masaa 12 kwa siku.
... ni sawa lakini tatizo dereva bado anakuwa ni yule yule gari lile lile. Abiria wanatakiwa wapate completely new environment kwa maana ya gari na dereva. Unless uniambie makampuni wawe na magari mawili linaloleta abiria lifaulishe kwenye gari jingine at the hub.

Hapo sawa; naul inaweza kukatwa ya moja kwa moja ila at some point watabadilishiwa gari na dereva ili kutoa nafasi kwa dereva wa awali kupumzika vya kutosha na gari kufanyiwa service. That I would agree. Kuburuza 1200km sio mchezo.
 
Uko sahihi, nilikuwa naangalia shuhuda moja kwenye channel moja ya kidini ya nje, kijana mdogo anasema alichukuliwa msukule, kwahiyo moja ya kazi walizokuwa wanafanya ni kwenda baadhi ya maeneo na kusababisha ajali, then wanachukua damu na kuwapelekea wahusika ambao wanaishi chini ya bahari.Hii dunia ni zaidi ya unavyoijuwa...
...Umeamini Ushuhuda wa Kijana....??
 
Majeruhi 63
Marehemu 12
Jumla 75
Uwezo wa Basi 52+dereva na konda.
Polisi wapo, barrier zipo, katazo la kutembea usiku lipo. Sheria ya kila abiria akalie kiti ipo.
Nini mbaya katika hii sekta.?

Hii tabia ya kuzidisha abiria kwa tamaa ya posho iko Sana mabasi ya Moro na tanga. Lkn who cares.
Surprise Basi la Moro au tanga lazima ukute Kuna abiria wamekaa kwenye engine. Matrafik wengi aidha Ni vipofu hawalioni au wanagawiwa posho.

Nakumbuka Kuna siku tunatoka Mwanza abiria mashabiki wa mwendo kasi wanamwambia dereva. Mimi nitakulipia faini mbili, mwingine mbili, inamaana dereva akitoa rushwa kwa polisi abiria ndio wanaingia mfukoni.
 
Back
Top Bottom