Dodoma: Basi lililobeba Wabunge wa Tanzania lagonga Lori na kuwajeruhi Wabunge 23

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Moja ya basi lililokuwa limewabeba Waheshimiwa Wabunge wanaoelekea kwenye Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki limepata ajali ya kugongana na lori la mizigo maeneo ya Mbande Kongwa asubuhi hii.

Majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa Hospitali ya Uhuru na Hospitali ya Benjamini Mkapa za Mkoani Dodoma.

========

Baadhi ya wabunge waliokuwa wanasafiri kuelekea Mombasa Kenya kushiriki mashindano ya 14 ya Mabunge ya Afrika Mashariki, wamepata ajali katika eneo la Mbande mkoani Dodoma baada ya Basi waliokuwa wakisafiria kugongana na Lori.


 
Natumaini kuna wengi watakuwa wamekufa.
Dah aseee kweli mmewachoka hawa vibaka.

Hapo utakuta basi lilikuwa mwendo wa ngiri na kufanya vurugu barabarani kisa tu limebeba wakujiita "waheshimiwa".

Maana hii nchi watunga sheria na walinda sheria ndio wanaongoza kuvunja sheria.
 
Kwa muonekano wa hii ajali (bus imekula mbele kwa dereva na lorry nyuma upande wa dereva pia) hapo nashindwa kuimagine scenario ilikuwaje.

Yani imagination inaniambia dereva wa bus alitaka kuanza ku overtake gari iliyokuwa mbele yake huku lorry likitokea upande wa tofauti na bus lake ila akakosea makadirio akajikuta ameshatoa chuma sekunde kadhaa kabla hajapishana kabisa na lorry ndio maana ameligonga kwa sehemu ya nyuma upande wa kulia (angalia mpact inaonekana lorry limepigwa kuelekea nyuma ndio maana hata mlango umejikunywa kurudi nyuma) na yeye dereva bus lake likapata majeraha upande wake wa kulia. Sioni explanation ya tofauti hapo na mwendo kasi lazima ndio chanzo.

Wataalamu wa barabarani hebu nirekebisheni.
 
Kuna jambo Mungu anajaribu kutufunulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…