Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Azimio la Bunge kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini leo Juni 10, 2023.



======

Leo Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania linatarajia kujadili mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya DPWorld unaodaiwa kutotaja ukomo kuhusu Ushirikiano katika Uendeshaji, Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari zote za Baharini na Maziwa zilizopo Tanzania Bara

Mkataba umeibua maswali ambayo hayajapatiwa ufafanuzi wa kina ikiwemo thamani na muda wa uendeshaji pamoja na sababu za Tanzania kuingia mkataba na kampuni inayotajwa katika kesi za ukwepaji kodi na migogoro katika utekelezaji mikataba huku baadhi ya Nchi zikiikataa kampuni hiyo.

Je, unaufahamu kiasi gani Ushirikiano wa DP-World na Bandari?

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anawasilisha Pendekezo la Kuridhiwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini, leo Juni 10, 2023

PROF. MAKAME MBARAWA
"Pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji Huduma za haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.”

“Hali ya sasa ya utendaji imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na Bandari shindani kikanda. Kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es salaam ni Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban.”

"Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar umetokana na changamoto ikiwemo kukosekana kwa Mifumo ya kisasa ya TEHAMA, maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena, Maegesho ya Meli, mitambo ya kutosha na ya kisasa ya kuhudumia shehena ambayo ina gharama kubwa ya Uwekezaji.”

“Meli kutumia muda mrefu kupakia na kupakua shehena gatini kwa wastani wa Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1 inayokubalika Kimataifa, pamoja na Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anasema "Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar umetokana na changamoto ikiwemo kukosekana kwa Mifumo ya kisasa ya TEHAMA, maeneo ya kutosha ndani na nje ya Bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena, Maegesho ya Meli, mitambo ya kutosha na ya kisasa ya kuhudumia shehena ambayo ina gharama kubwa ya Uwekezaji.”

Pia, “Meli kutumia muda mrefu kupakia na kupakua shehena gatini kwa wastani wa Siku 5 ikilinganishwa na Siku 1 inayokubalika Kimataifa, pamoja na Meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Mkataba wa DP World kuendesha Bandari utakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za Miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa Mikataba ya Nchi mwenyeji na Mikataba ya miradi

Amesema "Msingi wa Mkataba huu kuendana na Mikataba ya miradi ni kutokana na kwamba unaweka msingi unaowezesha kuingia na kutekelezwa kwa Mikataba 10 Nchini."


Huyu aliekua mwenyeki vijana taifa na naibu waziri hana akili
 
Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.


[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sawasawa..
 
Tanzania nchi yangu,nakupenda sana....
Watu wenye hoja kina mdee wanapigwa vita kwa personal attacks,
Badala ya kuchangia wasikilize ni taarifa kila Muda spika ana muharasi harasi,
 
Watanganyika waarabu wanachukua ukanda wote wa bahari ya Hindi kuanzia Tanga, Bagamoyo, Dar, Lindi hadi Mtwara.

Sasa basi ikifika 2025 tusipokuwa makini kwenye uchaguzi mkuu kumuondoa Saa100 imekula kwetu mazima.
2025 mtafanya nini boss, uchaguzi ni kupotezeana muda. Machafuko pekee ndio yatarejesha nguvu za wananchi kwenye maamuzi.
 
Duh. Nasikiliza wabunge wanavyolamba asali na kuongea upupu.., aibu naona mimi msikilizaji.

Hii ndo democracy kweli? Yaan tunachagua wawakilishi lakini wao wanapendekeza maslahi yao..
Yaan maoni ya waliowachagua hayama mantiki???
 
Nafuatilia Bunge hapa naona Mdee kakubali kumpa Maua yake Spika Msomi Tulia.
Mdee..... Mhe! Spika nakubali wewe ni Mbobezi lakini akaanza kujiuma uma.....
 
Mimi pia huwa nakerwa na watu wanaojipendekeza, eti mama, mama, hadi aibu! Unakuta janaume jitu Zima, mama,mama, come-on! Tunaweza ku-survive bila kujipendekeza kwa namna hiyo. Unaweza kukuta hata mama yake mzazi hamuiti kwa heshima, adabu na mara kwa mara hivyo. Frankly I hate such habits.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni Wapumbavu sana sana
 
Back
Top Bottom