Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Sema Ccm Imepitisha Mkataba Wake Kama Ilivyosema Mwanzo
 
Imekwisha, miaka watayokubaliana Asilimia 90 ya waliyopitisha hawatakuwepo duniani
Wacha kupotisha, yaliyojadiliwa leo siyo mkataba.

Hakuna kwenye makubaliano yoyote ya ushirikiano wa kimaendeleo wa nchi na nchi ambao unakuwa na kikomo, kunakuwa na mwanzo tu.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Gati namba 8-11 ndo ilikuwa TICTS. Hatuna hizi Gati tangu enzi za Mkapa.
CCM ni adui mkubwa wa hili Taifa.
Kama Taifa hapa tumeliwa.
 
Wacha kupotisha, yaliyojadiliwa leo siyo mkataba.

Hakuna kwenye makubaliano yoyote ya ushirikiano wa kimaendeleo wa nchi na nchi ambao unakuwa na kikomo, kunakuwa na mwanzo tu.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Sabato Njema
 
Hii ngoma iliisha kitambo san leo ilikua kuigiza tu kupitia bungeni kama sheria isemavyo!!
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema huko nyuma kwamba , nanukuu "ANAYEKULA NYAMA YA MTU HAACHI" Mwisho wa kunukuu , kwa tafsiri pana maana ya usemi huu wa Nyerere ni kama ile methali ya wahenga iliyosema MAZOEA HUJENGA TABIA

Kwamba ukizoea kufanya jambo fulani basi utaendelea tu kulifanya hata kama ni baya , ili mradi wewe binafsi au familia yako inafaidika .

Bandari zetu wamepewa Waarabu kibwege kabisa kwa vile tu wenye mamlaka wameamua kuigawa ili wao wafaidike , nakuhakikishieni kwamba hakuta kuwa na ufanisi wowote ule , NIPO HAPA JF NIMEKAA , Yaani tunauza mali zetu kwa ajili ya uvivu tu wa kazi na fikra , yaani tunaamini tu kwamba hatuwezi , ila wanaoweza ni waarabu ! Poor Tanzania !

Tumesahau ya NET GROUP , ATCL , TRL , TTCL na hata RICHMOND , tulitumia nguvu kubwa kushawishi na kudanganya umma kwamba kutakuwa na Tija , leo kiko wapi ?

Haya mmeuza Bandari kwa watu wenu ni Shirika lipi lingine mnafuatia kuliuza ili tujiandae ?

Nakulilia Tanzania .

 
Gati namba 8-11 ndo ilikuwa TICTS. Hatuna hizi Gati tangu enzi za Mkapa.
CCM ni adui mkubwa wa hili Taifa.
Kama Taifa hapa tumeliwa.
Kajichanganya, hizo gati zimejengwa kwa mkopo wa awamu ya 5 kutokea 2017
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…