Ukweli ni kua Mh.Rais na timu yake ya uongozi chini ya CCM,wamefanya maamuzi safi wakati sahihi. Zilipigwa sana kelele kuhusu wawekezaji,mizigo kuchelewa bandarini na rushwa kuwepo bandarini.Kwa kiasi kikubwa naona sasa serikali ya awamu ya sita imefanya maamuzi sahihi ili kutatua matatizo tuliokua tumezoea.
Mwisho,wanasiasa wengi waliomba nchi yetu pamoja na serikali kufanya paradigm shift ya kutoka kwenye diplomasia ya kiasa (political diplomacy)kwenda kwenye diplomasia ya uchumi(economic diplomacy). Sasa Mama Samia Suluhu na serikali yake wamejua faida yake na kuanza kutekereza ilo lakini wanatokea watu wanaanza kupotosha. Sote tukiungana kwa pamoja na kushirikiana na serikali yetu uhakika kwa kupiga hatua kubwa hupo kwenye uchumi wa bandari yetu na uchumi wa blue.
MUNGU IBARIKI TANZANIA