mara nyingi. kila baada ya wiki mbili nakuwa dom au napita dom kwenda mikoa mingine kwa shughuli zangu. Kukiwa vikao vya ccm tu, hoteli zote na vigesti vyote hata vya uchochoroni vinajaa. Pia hoteli nyingi za dodoma ni chafu, breakfast zao ni mbovu hata huwa sili unaweza ukatapika kama unabisha asubuhi nenda area c pale simba hotel, lion lodge, faru lodge, safari na vihotel na vilodge vyote vilivyoko maeneo yale na dodoma yote ni aibu, isipokuwa sehemu chache kama Kemy Lodge
Ninaijua dodoma tangu kikiwa kimji kidogo sana miaka ya 1980's nikiwa nasoma mazengo secondary na baadaye baada ya chuo nikafanya kazi dom, ninaijua dodoma ndani nje mpaka imekuwa hivyo ilivyo, hakuna kitu cha maana cha kuringishia, bado sana.
kuisifia dodoma na kuiponda miji/majiji ya zamani ni kutimiza dhana/mithali ya mwamba ngoma huvutia kwake lakini dodoma hakuna lolote.
Ndiyo sababu hata rais ye yote wa nchi hata akiwa peke yake akifanya ziara tz haletwi dodoma-makao makuu maana ni aibu. Uncle magu alikurupuka bila kupaandaa.