Dodoma hapakaliki, Watu wa Jiji wanafunga biashara za Watu kisa Service Levy

Naona wameamua kudhibiti wafanya biashara wachache tu wawepo
Kama mnavyoambiwa msizaane na wazungu
Hapo kuna watu wakubwa nyuma ya biashara hizo
Wanataka muwaachie mji labda mkalime
 
Mshika Kibubu Mkuu alishasema " kama hatuendani na wanavyotaka tuhamie Burundi"

Ni wakati sasa wakufunga biashara na kutimkia Burundi.
 
Hakuna tatizo, maana nchi hii kila kitu anafanya mama wa shoka, iron lady, simba wa yuda, yule ambaye hajawahi tokea dunia nzima, chief wa machief, Dr Samia, jabali kuu.

Kazi iendelee
Cc Lucas mwanshambwa
 
Labda ni kwaajili ya kunenepesha wabunge maana tunaambiwa wanapandishiwa posho toka 13 kwenda 18
 
Serikali ya Tanzania inaongozwa na wasomi waliowekwa madarakani na wachawi, waganga pori na wasoma viganja ambao karibia wote ni TABULARASA.... Ukiona msomi anashiriki SHIRKI ujue alienda shule kama stages za ukuaji na siyo kuelimika

Kimsingi tunaishi kama mazombi ndani ya nchi huru inayopeperusha bendera yake kwa furaha huku wananchi WAKIHAHA
 
Poleni.Hao wanaofunga wamepewa mamlaka na nani?
 
Leo nimesikiaa wapo ihumwa tra na jiji Kaz yao Ni kufunga maduka bila maelezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…