Dodoma: Maadhimisho ya Mei Mosi, Waliofukuzwa kwa vyeti feki kulipwa, ahadi ya Nyongeza ya Mishahara yatolewa, Unyanyasaji kazini wakemewa

Dodoma: Maadhimisho ya Mei Mosi, Waliofukuzwa kwa vyeti feki kulipwa, ahadi ya Nyongeza ya Mishahara yatolewa, Unyanyasaji kazini wakemewa

Dawa ya kupata mshahara mkubwa ni kuacha kazi na kwenda kufanya kazi nyingine, namaanisha usiache kazi kwenda kutafuta kazi nyingine bali tafuta kazi nyingine ukipata kazi andika 30 days notice kisha nenda kafanye kazi mpya, shida watumishi wengi wa serikali wanataka wakae serikalini mpaka wastaafu...ifike mahala unafanya kazi miaka 5 unatimka sehemu nyingine kutumia uzoefu wako sio unakomaa tu serikalini unasubiri huruma ya Rais ya Mei Mosi na akiingia mjuaji hakuna kupandisha mshahara hata miaka 5 kama kwa Rais aliyepita. Na akicheza vizuri na akili za wananchi anawashinda maana watumishi wa serikali hawazidi million 1 kati ya Watz 55million.
Mkuu wewe subiri siku ya Saba Saba(siku ya wakulima) ukalilie ongezeko la Bei ya mazao, sisi tuache tulilie nyongeza ya mshahara, unadhani Kila mtu akiacha kazi kisa kuogopa kudai masrahi mazuri nani atalitumikia taifa letu?
 
Watumishi kila hotuba ya mei mosi wanadai nyongeza ya mshahara tu.

Ila je madai yao yanaendana na kiwango tunachokizalisha kama Taifa.

Maana isijekuwa kila tunachopata kinamwenda kwenye kilipana posho na mishahara tu.

Maendeleo hakuna.

Tugawane keki ndogo tunayoioata kwa kutumia busara.

Inawezekana kweli huyaoni kutegemea na jicho unalotumia - lakini wao wakitimiza wajibu wao, na siasa iwashinde nguvu- wao wafanyeje!!! Tafakari
 
Hakuna kikubwa na cha ajabu atakachofanya kwa wafanyakazi wa Tanganyika huyo mkoloni kutoka Zanzibar

Kama hela nyingi anapeleka sehemu ndogo kama Zanzibar je hiyo ya kuwaongezea watanganyika mishahara kwa rate za maana ikowapi?
Kuwa na heshima huyo si mkoloni ni MTANZANIA mwenzako
 
Inatakiwa Mei Mosi iwe inatangulia kabla Jenister Mhagama kuongea au kusoma bajeti yake pale Dodoma!!!


Nadhani mnanielewa na mnafahamu alichokisema Bungeni
 
Back
Top Bottom