Dodoma: Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango ashiriki ibada Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska

Dodoma: Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango ashiriki ibada Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska

Yaani nyie mmzushie wee, halafu eti yeye any ama ever tu. Mbona nyie hamkunyamaza. Yamewashuka kabisa, mnakuja na makadiriko. Evil people, shame on you.
Unaongea kama Mwajuma ndala ndefu kwa mipasho.
Uliona wapi namzushie?
 
Mnatupanga asee yaani Mzee aonekane halafu asitoe salamu za pole kwa yaliyotokea Hannang 😁😁😁,Tiss yetu ni bora mm kuliko wao
 
Yule kigogo kabakiza kuolewa tu, ila ubingwa lazima washamvua wazee wazima. Mtu anapenda umbea kama mwanamke kikojozi bhn.
 
Mmesali nae Mzee leo?
Vipi kuhusu maafa ya Hannang amezungumzia au hajui 😁😁😁
Kweli limewashuka. Aibu yao kabisa. Tumesali naye leo parokia ya K- ndege Dodoma misa ya pili. Nimefurahi sana kumuona. MUNGU endelea kumlinda, ili wanaomtakia mabaya waendelee kuaibika.
 
Mmoj

Mmojawapo ni wewe. Ushahidi gani wakati picha unaziona. Tuliosali naye leo misa ya pili, parokia ya K-ndege dodoma ni ushahidi tosha. Yamewashuka kabisa. Na mkome. MUNGU endelea kumlinda . Mliomzushia msipotubu mtatangulia nyie. Sura zimewasinyaa.
Teremsha hasira, utajiambukiza pressure.
 
Mlokua mnamzushia kifo mna hali gani?Mlokua mnatangaza na kujiapiza kwamba akionekana mtafuta page zenu mshafuta?Mlokua mnapiga ngoma ya nchimbi na kuanza kumpost mpo wapi?Huwezi kushindana na Mungu hata kidogo!! Kwa mara nyingine wahuni na genge lenu mmefail again!!

Kama mnadhani mtafanikiwa kama mlivyofanikiwa kipindi kile basi safari hii mmechemka Mungu wetu hawezi kuruhusu hilo liwe labda atake yeye

Hii tabia ya kuzushia watu vifo siyo nzuri hata kidogo!! Na ingekua ni busara hawa wahuni washughulikiwe humo humo ndani ya chama na mtandao wao!!Lakini inakua ni vigumu maana wana mizizi kila mahali.

=======

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Mapadre mara baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili ktk Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma leo tarehe 10 Desemba 2023.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili leo Desemba 10, 2023. Ibada hiyo imeongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Dk Mpango amewaasa Watanzania kutumia vema mitandao ya kijamii.

Amesema matumizi yasiofaa ya mitandao ya kijamii yamekuwa yakiumiza watu wengi hivyo yampasa kila mmoja kutumia vema pamoja na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Makamu wa Rais amewashukuru waumini hao kwa kuendelea kumuombea ili aweze kutekeleza vema majukumu yake.
View attachment 2838329
View attachment 2838453

Muambieni aache kiki. Anajificha ili watu waanze kuuliza ndio anaibukia. Ni ushauri tu.
 
Asante Mungu!, maana...!.

Ila pia sisi Matomaso tupo!, kwa vile tulielezwa kuwa yupo nje ya nchi kikazi, tulitegemea picha ya kwanza ni picha ya akirejea nchini.

Picha ya pili ni VP akiwa popote kufanya lolote ni kumwakilisha rais, hivyo tulitegemea siku akirudi, apokelewe, aonekane akitoa mrejesho wa safari kwa aliyemtuma!.

Kama hii picha ni kweli ni ya leo, inamaana jana VP alikuwa Dodoma!, hivyo alitarajiwa kuonekana pale uwanjani kwenye maadhimisho ya uhuru!.

Anyway, kitu muhimu ni tumemuona yuko bukheri wa afya, tena amenyonga tai, hivyo kumaanisha hata ile taarifa kuwa ana hali fulani ni uzushi!, ingekuwa kweli, asingenyonga tai leo!. Hata hivyo asante kwa hii picha roho zetu zimetulia, ngoja nipitie meta data za hii picha kuithibisha ni ya leo!. Nimethibitisha
View: https://youtu.be/wytTpiQr4HA

Asante tena.

P

Kaka code ime eleweka, Kumbuka hata jemedari aliye tutoka.
👉Nae Ali enda kanisani kuaga🤒
 
Asante Mungu!, maana...!.

Ila pia sisi Matomaso tupo!, kwa vile tulielezwa kuwa yupo nje ya nchi kikazi, tulitegemea picha ya kwanza ni picha ya akirejea nchini.

Picha ya pili ni VP akiwa popote kufanya lolote ni kumwakilisha rais, hivyo tulitegemea siku akirudi, apokelewe, aonekane akitoa mrejesho wa safari kwa aliyemtuma!.

Kama hii picha ni kweli ni ya leo, inamaana jana VP alikuwa Dodoma!, hivyo alitarajiwa kuonekana pale uwanjani kwenye maadhimisho ya uhuru!.

Anyway, kitu muhimu ni tumemuona yuko bukheri wa afya, tena amenyonga tai, hivyo kumaanisha hata ile taarifa kuwa ana hali fulani ni uzushi!, ingekuwa kweli, asingenyonga tai leo!. Hata hivyo asante kwa hii picha roho zetu zimetulia, ngoja nipitie meta data za hii picha kuithibisha ni ya leo!. Nimethibitisha
View: https://youtu.be/wytTpiQr4HA

Asante tena.

P

Kuwa kana Tomaso sio sifa njema; usifikiri kuwa Yesu alifurahishwa na Tomaso kutoamini ufufuko wake. Tomaso kutoamini kuwa Yesu alikufa, inaonyesha, hata mafundisho yake (Yesu), alikuwa hayaamini, maana habari za kufa na kufufuka kwa Yesu zilienezwa hata kabla Yesu hajakufa. Hivyo, tusidhani kuwa Yesu alifurahi alopomwambia Timaso aje kutia vidole vyake kwenye kovu za vidole vyake ili kuhakikisha kuwa ndiye Yesu aliyekufa. Heri yao walioamini pasipo kuona!

Sio kila arejeapo makamu wa Rais kutoka safari za nje lazima kuwe na ujumbe wa kumpokea na kisha atoe salamu za huko alikotoka. Kukiwa na umuhimu wa
 
Kwa nini Watu hupenda kuombea wengine Mabaya hata kama hawajawahi kuwakosea
Hii ni tatizo la subconscious mind

Zamani nilikuwa nawaza Sana kwanini watu ufurahia habari Mbaya za MTU sasa nilivyosoma subconscious mind nikaelewa kuwa hilo tatizo limeanzia mbali.
 
Kuna Wakati waseminari hutumia Lugha mahsusi ili Ujumbe uwafikie wenye Macho ya kuona na Masikio ya kusikia

Dr Mpango amesema alikuwa Kwenye majukumu maalumu, na Hii ilishaelezwa na Waziri mkuu

Dr Mpango anasema ni vema Mitandao ya Kijamii ikatumika Vizuri, ukiangalia uzushi na kuchafuana ndio kumetamalaki Kwenye mitandao na ni juzi tu Katibu mkuu wa CCM alijiuzulu

Hata Yesu aliposema " Naona Kiu" hawakumuelewa

Aliposema " Eloi Eloi ramasbaktani" hawakumuelewa

Na hata aliposema " Imekwisha" hawakumuelewa

Watanzania tujifunze kutumia vizuri tena kwa maadili mitandao ya Kijamii

Unaweza kuuliza fulani yuko Wapi Bila Kumzushia Ugonjwa au Kifo

Ahsanteni sana

Heri Wenye Moyo Safi maana hao Watamuona Mungu!
 
Naona unalemba mwandiko

Kwani kufoka unadhani kuandika kwa herufi kubwa au kuongea kwa sauti?

Unaweza ukawa unanongoneza sikioni lakini ukawa unafoka
 
Makamu wa Rais yuko pigo moja tu la moyo kutoka kuwa Rais kwa hiyo afya yake ni jambo linalotuhusu watanzania wote. Makamu wa Rais hapaswi kupotea kwa muda mrefu vile bila maelezo yanayoeleweka kwa raia wa nchi yake.
Aidha, watanzania wanakumbuka walivyofichwa kuhusu afya ya Rais wa awamu ya tano mpaka umauti ulipomkuta. Sidhani kama serikali imewaomba msamaha raia wake kwa hadaa ile. Watanzania pia wanakumbuka pia kuwa Makamu wa Rais aliwahi kuugua sana hivyo si ajabu kuugua tena.
Uongozi wetu unatakiwa kuwachukulia raia zake kama watu wazima na kuwapa maelezo yanayoeleweka wanapohoji uwepo wa viongozi wetu wakuu. Huku kuficha ficha ndio kunakotufikisha hapa. Tuwaige wenzetu ambao wanatoa taarifa kamilifu kwa raia wao pale tu ambapo kiongozi anapokuwa haonekani hadharani.

Amandla...
 
Gentmycine
anasema aliwekwa bond mpaka deni lilipwe
Kigogo
anasema alikata moto
Sexless
Anasema aliambiwa na anko wale ambaye ni TISS kuwa maini yalikuwa yameoza
Mange
Alisema alifanyiwa upasuaji
kasimu
alisema yupo nje ya nchi kazi maalumu
isdori mwenyewe
alisema alikuwa nje ya nchi kimajukumu.

ila neno nipo mzima aa afya kama unavyo niona alilitamka mara nyingi mbele ya raisi kumhakikishia KANAKWAMBA RAISI NAYE ALIKUWA NA MASHAKA NA AFYA YA MAKAMU
 
Kuna Wakati waseminari hutumia Lugha mahsusi ili Ujumbe uwafikie wenye Macho ya kuona na Masikio ya kusikia

Dr Mpango amesema alikuwa Kwenye majukumu maalumu, na Hii ilishaelezwa na Waziri mkuu

Dr Mpango anasema ni vema Mitandao ya Kijamii ikatumika Vizuri, ukiangalia uzushi na kuchafuana ndio kumetamalaki Kwenye mitandao na ni juzi tu Katibu mkuu wa CCM alijiuzulu

Hata Yesu aliposema " Naona Kiu" hawakumuelewa

Aliposema " Eloi Eloi ramasbaktani" hawakumuelewa

Na hata aliposema " Imekwisha" hawakumuelewa

Watanzania tujifunze kutumia vizuri tena kwa maadili mitandao ya Kijamii

Unaweza kuuliza fulani yuko Wapi Bila Kumzushia Ugonjwa au Kifo

Ahsanteni sana

Heri Wenye Moyo Safi maana hao Watamuona Mungu!
Nimependa sana hiyo paragraph ya mwisho
 
Wale wote ambao walimzushia kifo wakiwemo wanasiasa walaaniwe wote.
Kuzusha kifo ni dhambi kubwa Sana
 
Back
Top Bottom