Dodoma: Makamu wa Rais, Mpango amtembelea Festo Dugange Hospitali ya Benjamin Mkapa

Dodoma: Makamu wa Rais, Mpango amtembelea Festo Dugange Hospitali ya Benjamin Mkapa

Kama ni kweli, inakuwaje tuwe na viongozi wazinzi?!!! Uadilifu unatokea wapi hapo wakati kiongozi ni mzinzi?!!!!

Ndio maana kila mwaka ripoti ya CAG inaonyesha ubadhirifu wa fedha za umma kwasababu walio wengi sio waadilifu.....hili ni Janga, inatupasa kama Taifa kutengeneza viongozi waadilifu na wenye hofu ya Mungu.
 
Uliza kwanza yafuatayo:
1. Alipokewaje hosptslini bila Pf3
2. Polisi yupi amepima hiyo ajali
3. Majeruhi wako wapi?
4. Kama majeruhi wapo ni akina nani, kama wamekufa wanazikwa wapi na lini
5. Kauli ya serikali/ jeshi la polisi imetolewa na nabi kuhusisna na hiyo ajali
6. Aliyefumaniwa anatiwa nini na wapi
7. Gari la walipa kodi liko wapi na lina hali gani?
8. Nafasi ya uwaziri iko wazi au bado ataendelea nayo.
9. Kesi ya kuharibu mali ya umma na kusababisha ajali uchunguzi umegikia wapi na atapelekwa lini mahakamani?
10. Namba ya hiyo gari iliyopata ajali ni namba gani?
11. Kama gari alilokuwa anaendesha ni lake binafsi alitokea wapi kwenda wapi ?

Kwa mtu ambaye ni waziri tena Tz maswali yako yote hayana jibu maana hakuna mtu ambaye anajipenda wawe polisi au nani atagusa!
 
Amuonye kama yanayosemwa ni kweli,kuchepuka na mke wa mtu,siyo vema.
... na wala sio kosa kisheria kwa mujibu wa sheria za Tanzania kuchepuka na mke wa mtu as long as mmekubaliana. Tena mumewe akiwakuta kuna taratibu za kufuata na sio kuleta fujo au kuumiza watu!
 
M
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amemtembelea na kumjulia hali Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Dk Festo Dugange ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari.

Habari toka vyanzo mbalimbali zinaeleza Dk Dugange alipata ajali hiyo usiku wa kuamkia Aprili 26, 2023. Hata hivyo, mpaka sasa si Jeshi la Polisi wala viongozi wa wizara yake waliokuwa tayari kuthibitisha kuhusua ajali ya kiongozi huyo.

Kwa mujibu wa picha ya inayomuonesha Makamu wa Rais akiwa hospitalini, Naibu Waziri huyo amevunjika mkono wa kulia.
View attachment 2603789
Mchepuko noma
 
JK alipotaka kuhamishia serikali yake kanda ya kati, wazee wakamuita na kumwambia. Tunawajua wasaidizi wako, ni watu ambao bado damu inachemka, kwa vyeo na posho posho hizi wanazopata, wanakuwa wamechangamka kweli! Wakifanya mambo yao hapa Bongo, ni jiji kubwa, hayataonekana. Ila ukiwapeleka kanda ya kati ka mji (kwa wakati ule) ambako hata mtu akipanda bajaji anakamaliza ndani ya nusu saaa, wataumbuka...
Mzee akasita kuhamishia shughuli kanda ya kati...
nitakuwa wa mwisho kuamini uadilifu wa hawa viongozi wakuu si makamu wa rais, si waziri mkuu. Waziri mkuu ndiyo amenikatisha tamaa kupitiliza. Hawa wote ni waovu na wanafiki wakubwa. Hivi wananchi wanapoona mambo km haya watawezaje kuwaamini ktk kusimamia maadili? Bila hata haya wanamtembelea badala hata wangekaa kimya. Hizi ni dharau kubwa sana kwa wananchi.
 
Kama ni kweli, inakuwaje tuwe na viongozi wazinzi?!!! Uadilifu unatokea wapi hapo wakati kiongozi ni mzinzi?!!!!

Ndio maana kila mwaka ripoti ya CAG inaonyesha ubadhirifu wa fedha za umma kwasababu walio wengi sio waadilifu.....hili ni Janga, inatupasa kama Taifa kutengeneza viongozi waadilifu na wenye hofu ya Mungu.
Je ni vipi kuhusu gari yetu, au kwa kuwa wamezoea kuchezea pesa zetu?
 
JK alipotaka kuhamishia serikali yake kanda ya kati, wazee wakamuita na kumwambia. Tunawajua wasaidizi wako, ni watu ambao bado damu inachemka, kwa vyeo na posho posho hizi wanazopata, wanakuwa wamechangamka kweli! Wakifanya mambo yao hapa Bongo, ni jiji kubwa, hayataonekana. Ila ukiwapeleka kanda ya kati ka mji (kwa wakati ule) ambako hata mtu akipanda bajaji anakamaliza ndani ya nusu saaa, wataumbuka...
Mzee akasita kuhamishia shughuli kanda ya kati...
Tabia za watu wachache zikachelewesha mradi wa kimkakati duh
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amemtembelea na kumjulia hali Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Dk Festo Dugange ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari.

Habari toka vyanzo mbalimbali zinaeleza Dk Dugange alipata ajali hiyo usiku wa kuamkia Aprili 26, 2023. Hata hivyo, mpaka sasa si Jeshi la Polisi wala viongozi wa wizara yake waliokuwa tayari kuthibitisha kuhusua ajali ya kiongozi huyo.

Kwa mujibu wa picha ya inayomuonesha Makamu wa Rais akiwa hospitalini, Naibu Waziri huyo amevunjika mkono wa kulia.
View attachment 2603789
Maelezo ya picha,Pole,punguza speed mzee,siunaona sasa mambo yenyewe yalivokaa vibaya...
 
Hili tukio limenifanya niwaze mbali sana, pia kunikumbusha kauli za marehemu mzee wangu, alikuwa akiniambia (jina) usiache kumhofia Mungu kwa vile huna uhakika kama yupo au hayupo, wewe mhofie ili usitende mambo ya hovyo kwa vile kutenda mambo ya hovyo kuna hasara siku zote, ni bora utende mema ili kama Mungu yupo uwe mahali salama, lakini pia kama hayupo utaepuka hizo hasara za kutenda mambo ya hovyo.....Nafikiria hasara/aibu/fedheha na dhambi alizopata huyu N/Waziri, na si ajabu akapoteza na kazi kama maadili yakifuatwa, Mkewe/Watoto/Familia wanamuonaje wakienda hapo Hospital......RIP Mdingi wangu, ushauri wako umeniweka mahali salama siku zote katika maisha yangu.
Niece. Maadili ni Bora kuliko ovyo na ovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom