Aliyekuwa Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam , Musa Salum , ametua Dodoma ambako amepata mapokezi Makubwa vikiwemo ving'ora vya Polisi huku akisindikizwa na msafara wa Magari na lundo la Pikipiki .
Haifahamiki ameenda Dodoma kufanya nini .
Bali Malalamiko ya Waislam waliomlima barua Mufti ya kutaka afafanue sababu hasa ya Musa Salum kupokelewa na msafara mzito , yanasema hivi , KWANINI MTU MAAMUMA ASIYE NA CHEO CHOCHOTE KUPOKELEWA KIHESHIMA NAMNA ILE UTADHANI NI KIONGOZI WA DARJA LA JUU ? Je hii si dharau kwa Baraza la Ulamaa na Mufti Mwenyewe ?