25000q
JF-Expert Member
- Dec 27, 2022
- 4,805
- 3,762
ccm wanamteua kwanza kisha ndio uchaguziKumbe Mufti ni unachaguliwa? Sio kuteuliwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ccm wanamteua kwanza kisha ndio uchaguziKumbe Mufti ni unachaguliwa? Sio kuteuliwa
wanao pigiwa ving,ora nchii wana julikana alahadi kawa nani?nchi hii inavituko sanaHakuna Hoja Zaidi Majungu.
Utaratibu Wa Police Unajulikana Ni Huduma Unalipia Unapewa Escort Sasa Maulid. Analeta Uchochezi Kwenye Imani.
Mufti Atoke Hadharani Azungumzie Pikipiki Ama Hiyo Escort.
kwakweli huyu anaviashiria vya ubinafsi ya kutaka kujiona ye ni bora kuliko wengine.Hata mapokezi atakuwa ameyatengeneza hao si wanalipwa tu kumtisha sheikh mkuu ahisi maamuzi yake siyo.Barua ya Wazi
Assalaam Alaykum,
Sheikh Mkuu, Mufti wetu wa Tanzania, nimeguswa kukuandikia barua hii ya wazi ama kwa kuhoji na kutaka ufafanuzi, ama kwa kushangazwa na nilichokiona.
Kama nilivyoshangazwa, nimefuatilia kwa ndugu zetu wengi katika imani, ama kwa hakika, tukio ninalolileta kwako limejenga taharuki kubwa kwetu waumini.
Nimeona video mtandaoni ikimwonesha aliyekuwa Sheikh wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akipata mapokezi ya ving'ora vya polisi na msafara wenye magari na pikipiki, mkoani Dodoma. Na kulakiwa na waumini kama Sheikh mwenye darja.
Sheikh wetu, tukio hilo limetengeneza mshangao mkubwa. Hayajapita majuma mawili tangu ulipomwondoa Alhad Mussa kuwa Sheikh wa Dar es Salaam. Inastaajabisha anatokeza na mapokezi makubwa.
Waislam wana maswali matano. Alhad Mussa anafikisha ujumbe gani? Anataka kumaanisha yeye ni mkubwa kuliko mamlaka ya Mufti aliyemtengua? Msafara wenye ving'ora na pikipiki iliyomsafishia njia, amepewa kama nani, ikiwa yeye kwa sasa ni maamuma? Polisi ni serikali, kwa mapokezi hayo, serikali inamuunga mkono Alhad Mussa dhidi ya Mufti? Waislam waliompokea na kumkirimu Alhad Mussa mithili ya kiongozi wa darja kubwa lengo lao ni nini?
Kwa maswali hayo, Sheikh wetu, Mufti Abubakar Zuberi, huna budi kutoka na kuzungumza na umma wa Waislam na hata wasio Waislam, ujibu maswali hayo ili Watanzania na mamlaka zake zitambue haki anazostahili Alhad Mussa na ambazo hastahili.
Hitimisho la kila mjadala ni kuwa kitendo cha Alhad Mussa kutengeneza mapokezi yale ni utovu mkubwa nidhamu kwa mamlaka ya Mufti. Amelikosea heshima Baraza la Ulamaa la Bakwata na uongozi wote wa juu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata).
Nakuangukia. Shime Sheikh, toka uongee na umma. Tujue nafasi ya Alhad Mussa. Alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Amani. Nafasi hiyo aliipata sababu alikuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam. Sasa si Sheikh tena. Kwa nini ving’ora vya polisi na kumbatio la waumini tena msikitini?
Wabillahy Ttawafiq,
Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakutu
View attachment 2517441
Hicho kiswahili cha darja badala ya daraja.Nimependa hicho Kiswahili, kama cha Shaaban Robert.
Hahahahaha kitengo wapi weweHuyo alikuwa mtu wa KITENGO ndo maana nchi hii kupata KATIBA mpya ni ngumu sanaa
Alhad TISS. Si mnajua Bakwata Ni CCM (b) na huyu sheikh ndio alikua kiunganishi Cha Bakwata na tiss. Alikua ameandaliwa kua muftih sema tu fitna za hapa na pale.Video ipo wapi sasa mkuu. By the way Alhad bado ana makoti mengine ya uongozi au amevua yote?
Sio Tiss yule sema anajikomba ni informer tuAlhad TISS. Si mnajua Bakwata Ni CCM (b) na huyu sheikh ndio alikua kiunganishi Cha Bakwata na tiss. Alikua ameandaliwa kua muftih sema tu fitna za hapa na pale.
Hatujawahi kuzushaNaona unataka kujaribu kuwafananisha viongozi wa kiislam na akina gwajima, mzee wa upako, mwamposa etc,, lkn inakataa.
Acha unafiki hebu tupia walau picha tuone huo msafara wa ving'ora na pikipiki na sie tuone. Huku kwenye uislam hakuna mbwembwe sijui za misafra mirefu na ving'ora na mapikipiki mengi kama huko kwenu hata uwe msafara wa muft.
Focus kwenye siasa chuki zako binafsi za kidini acha,,,Hatujawahi kuzusha
Atakuwa ameenda Makao makuu ya Chama kumsemelea Dr Mwaka PhDAliyekuwa Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Salum, ametua Dodoma ambako amepata mapokezi Makubwa vikiwemo ving'ora vya Polisi huku akisindikizwa na msafara wa Magari na lundo la Pikipiki.
Haifahamiki ameenda Dodoma kufanya nini.
Bali Malalamiko ya Waislam waliomlima barua Mufti ya kutaka afafanue sababu hasa ya Musa Salum kupokelewa na msafara mzito, yanasema hivi, KWANINI MTU MAAMUMA ASIYE NA CHEO CHOCHOTE KUPOKELEWA KIHESHIMA NAMNA ILE UTADHANI NI KIONGOZI WA DARJA LA JUU? Je hii si dharau kwa Baraza la Ulamaa na Mufti Mwenyewe?
Bakwata siyo dini ni TaasisiDini zime ingiliwa walahi
Bwana Alhadi Mussa Salum kukodisha bodaboda kadhaa kumsindikiza kituo chake kipya cha kazi kina uhusiano gani na dini?Dini zime ingiliwa walahi
Ameteuliwa?Bwana Alhadi Mussa Salum kukodisha bodaboda kadhaa kumsindikiza kituo chake kipya cha kazi kina uhusiano gani na dini?
Kitenge ni nguo ya akinamama.Nani Kitenge ndio Waislamu wote!!? Kitenge ana matatizo yake.