Dodoma: Mtoto wa miaka 6 auawa kikatili na watu wasiojulikana

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mtoto wa mfanyabiashara maarufu jijini Dodoma anayejulikana kwa jina la Jojo, Graison Kanyenye (6), anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani wakati mama yake akiwa matembezini usiku wa kuamkia jana.
1735292270928.png
Mbali na hilo, Jeshi la Polisi limesema mwili wa mtoto huyo ulikutwa ndani ya nyumba ukiwa na majeraha shingoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi amesema jana, Desemba 25, 2024 kuwa tukio litokea saa 1.00 asubuhi katika Mtaa wa Bwawani, Ilazo Extension jijini Dodoma, nyumbani kwa Ofisa Uvuvi wa Mtera, Hamis Mohamed.

Amesema Hamis (anatajwa kuwa mpenzi wa mfanyabiashara huyo) na mama yake walitoka kwenda matembezini na kumwacha mtoto huyo chini ya usimamizi wa dereva bodaboda wa Ilazo Extension, Kelvin Gilbert.

Bodaboda huyo anayetajwa kuwa walimfahamu kupitia huduma ya usafiri wanayoitoa kwa familia, aliachiwa mtoto ili amwangalie kipindi ambacho watakuwa kwenye matembezi wawili hao (Hamis na mfanyabiashara huyo).
IMG_2017.jpeg
 
Attachments

  • IMG_2016.jpeg
    IMG_2016.jpeg
    94.2 KB · Views: 9
Hamis (anatajwa kuwa mpenzi wa mfanyabiashara huyo) na mama yake walitoka kwenda matembezini na kumwacha mtoto huyo chini ya usimamizi wa dereva bodaboda wa Ilazo Extension, Kelvin Gilbert.

Mama mtoto mwenye akili ndogo kapata anachostahili...

Mtoto wa miaka 6 unamuacha chini ya uangalizi wa bodaboda wakati huo wewe na mpenzi wako mnaenda kushenyetana...

Na ajabu mama mtoto hatakuwa na kesi ya kujibu ustawi wa jamii wala popote pale...

Lakini ingelikuwa ni shauri la baba au ndugu wa baba kumtaka mtoto, utetezi ungekuwa yungali chini ya 12 years of age hivyo bado anapaswa awe chini ya mama...
 
Mtoto wa mfanyabiashara maarufu jijini Dodoma anayejulikana kwa jina la Jojo, Graison Kanyenye (6), anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani wakati mama yake akiwa matembezini usiku wa kuamkia jana.
View attachment 3185386
Mbali na hilo, Jeshi la Polisi limesema mwili wa mtoto huyo ulikutwa ndani ya nyumba ukiwa na majeraha shingoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi amesema jana, Desemba 25, 2024 kuwa tukio litokea saa 1.00 asubuhi katika Mtaa wa Bwawani, Ilazo Extension jijini Dodoma, nyumbani kwa Ofisa Uvuvi wa Mtera, Hamis Mohamed.

Amesema Hamis (anatajwa kuwa mpenzi wa mfanyabiashara huyo) na mama yake walitoka kwenda matembezini na kumwacha mtoto huyo chini ya usimamizi wa dereva bodaboda wa Ilazo Extension, Kelvin Gilbert.

Bodaboda huyo anayetajwa kuwa walimfahamu kupitia huduma ya usafiri wanayoitoa kwa familia, aliachiwa mtoto ili amwangalie kipindi ambacho watakuwa kwenye matembezi wawili hao (Hamis na mfanyabiashara huyo).
View attachment 3185379
Wivu wa mapenzi?ubambikiziaji wa baba feki? uzinzi wa mama wa mtoto?
 
Vipi kuhusu baba yake huyo mtoto mkuu?
Mwangalizi mkuu wa familia ni mama. Mama akiwa smart hata libaba liwe takataka familia mambo yataenda bila tatizo. Ila mama asipokuwa smart kuchukua nafasi yake sawasawa naye akaanza kuendekeza starehe na upuuzi mwingi hiyo familia haitoboi.

Mama mwenye akili unamkabidhije mwanao mdogo asiyejua hili wala lile kwa bodaboda ili wewe ukastarehe?
 
Kwa nini huyo baba alizaa na mwanamke asiye smart? Alikuwa anategemea nini?
 
Back
Top Bottom